Nape Nnauye ajiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Maliasili na Utalii

  • Thread starter Mwanahabari Huru
  • Start date

Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Messages
13,950
Likes
30,768
Points
280
Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2015
13,950 30,768 280
Mhe Nape amejiuzulu uenyekiti wa kamati ya mali asili baada ya kuwekwa kitimoto na chama. Habari zinasema ni baada ya kukataa kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji kinyume na sheria.

--------------

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amejiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii. Kujiuzulu kwake, kunatokana kile kinachodaiwa ni “Kugoma kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji, kinyume na sheria.”

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii zinasema, Nape amejiuzulu baada ya kutofautiana na serikali kuhusu ripoti ya Kamati yake.

“Nape alitaka ripoti ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii, iliombe Bunge kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge ili kuchunguza utaratibu uliotumika wa kufuta mashamba ya watu,” ameeleza mjumbe mmoja wa kamati hiyo.

Ameongeza, “Serikali haitaki kuundwa kwa Kamati hiyo. Hivyo imeamua kuitumia Kamati ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumlazimisha Nape kujiuzulu.”

Taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii zinasema, tayari Nape amemuandikia barua rasmi ya Spika kumjulisha kujiuzulu kwake.

Nape alihuhutubia waandishi wa habari leo akiwa chini ya vyombo vya usalama na kutetea msimamo wake.

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja siku moja kabla ya Kamati yake kuwasilisha ripoti yake na zinaeleza kuwa Kamati hiyo ilikuwa inaleta mapendekezo ya kuundwa kwa Kamati Teule, jambo ambalo lilihofiwa kuwaumbua baadhi ya wakubwa.

Machi mwaka 2017, Nape aling’olewa kwenye nafasi ya uwaziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo.

Mbunge huyo wa Mtama mkoani Lindi, alivuliwa wadhifa wake siku moja baada ya kupokea ripoti ya Kamati ya uchunguzi juu ya tukio uvamizi wa kituo cha televisheni cha Clouds kwa kutumia silaha uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Ripoti ya kamati aliyoiunda Nape kuchunguza tukio hilo, ilithibitisha kuwa Makonda alivamia kituo hicho majira ya saa 5 usiku wa Ijumaa ya tarehe 17 Machi 2017 na alifanya uvamizi huo akitumia askari wenye silaha. Nape aliahidi kulifikisha ripoti yake kwa mamlaka ya juu yake. Haijajulikana mpaka sasa, ripoti hiyo amekabidhiwa nani.

Nape ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Idara ya Uenezi ya CCM, amesema atapata nafasi nzuri ya kutumikia wananchi wa jimboni wake baada ya kuachia nafasi hii.
 
Kisoda2

Kisoda2

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2008
Messages
1,822
Likes
479
Points
180
Kisoda2

Kisoda2

JF-Expert Member
Joined May 30, 2008
1,822 479 180
Mwenyekiti wa CCM hana mamlaka ya kumlazimisha Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge asitoe ripoti.

Especially ripoti ambayo imeshakamilika (Wabunge ndani ya kamati wameshakubaliana).

Especially Mwenyekiti kama Nape Nnauye ambaye mpaka kesho hajasamehe mnyuko wa kudhalilisha aliopewa kutoka na serikali aliyolala misituni kuiweka madarakani.
wewe unatakaje/kusema nini katika hilo?
nakuona kiswahili kinaanza kuwa mureefu tu.
kama hutaki hilo jibu weka la kwako.
 
K

Kwameh

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2011
Messages
1,089
Likes
822
Points
280
Age
39
K

Kwameh

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2011
1,089 822 280
wewe unatakaje/kusema nini katika hilo?
nakuona kiswahili kinaanza kuwa mureefu tu.
kama hutaki hilo jibu weka la kwako.
Jibu lako hali make sense.

Eti “Nape amejiuzulu baada ya kutofautiana na serikali kuhusu ripoti ya Kamati yake.”

Serikali inawezaje kutofautiana na ripoti ambayo bado haijafika bungeni?

Serikali imekataa mambo kibao ambayo yalikuwa kwenye ripoti ya Tume ya Sheria na Katiba i kuhusiana na sheria ya vyama - ripoti ilipofika bungeni.

Kwa nini hiki ki ripoti cha umiliki wa mashamba ya wawekezaji ndio serikali iogope kufika bungeni?
 
taamu

taamu

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Messages
5,952
Likes
1,881
Points
280
taamu

taamu

JF-Expert Member
Joined Dec 11, 2012
5,952 1,881 280
Baada ya Mo Dewji kunyang'anywa mashamba kule Tanga! Siku kama mbili Mh Rais akawa ana hutubia sehemu fulani akasema "Kuna watu wanaangaika kutaka kufanya Robbing ili yale mashamba warudishiwe..!, Jamani mimi nikishafuta ndiyo basi hayarudi" Uenda kweli wale watu walitaka kulitumia Bunge kama sehemu ya kufanya yao! Lakini kweli shamba aliendelezwi nalo liundiwe tume..! Shamba linalo onekana kweli?
Kwanini asingefuta bila kutumia mbinu ya kisenge vile.
 
Kisoda2

Kisoda2

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2008
Messages
1,822
Likes
479
Points
180
Kisoda2

Kisoda2

JF-Expert Member
Joined May 30, 2008
1,822 479 180
Jibu lako hali make sense.

Eti “Nape amejiuzulu baada ya kutofautiana na serikali kuhusu ripoti ya Kamati yake.”

Serikali inawezaje kutofautiana na ripoti ambayo bado haijafika bungeni?

Serikali imekataa mambo kibao ambayo yalikuwa kwenye ripoti ya Tume ya Sheria na Katiba i kuhusiana na sheria ya vyama - ripoti ilipofika bungeni.

Kwa nini hiki ki ripoti cha umiliki wa mashamba ya wawekezaji ndio serikali iogope kufika bungeni?
Muulize aliye leta UZI au unamuogopa?
 
Mpinzire

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Messages
1,390
Likes
1,336
Points
280
Mpinzire

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined Jan 18, 2013
1,390 1,336 280
Kwanini asingefuta bila kutumia mbinu ya kisenge vile.
Haya mashamba MeTL ilipewa bure na sharti lilikuwa ayaendleze kwa kuyafanyia kazi wananchi wa eneo husika wapate ajira! Alipewa mashmba 21 lakini 12 yapo ni mapori tu na sheria usipo yaendeleza unanyang'anywa anapewa mtu mwingine anayeweza kuyafanyia kazi au wanapewa wananchi walime..! Sheria ni msumeno ila nakushangaa unapinga wananchi wa kawaida kabiba wasipewe ayo maeneo wafanyie shughuli za uzalishaji..? We wa wapi? Mtu anamiliki mashamba kila shamba lina ekari 12,000+ ..! Sasa 6 kanyang'anywa na sita kapewa onyo kama asipoyaendeleza yanarudishwa kwa wananchi.
Over
 
JustDoItNow

JustDoItNow

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Messages
2,707
Likes
636
Points
280
JustDoItNow

JustDoItNow

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2013
2,707 636 280
Sisi tulio nje hatuoni mambo vizuri kama walipo ndani. Tuache ushabiki nchi imepigwa na wawekezaji hewa katika mashamba. Wamechukua mikopo wamewekeza nje ya nchi sisi tunapiga kelele. Rais songa mbele kitaeleweka tu.
Naunga mkono kabisa. Magufuri songa mbeleeee
 
taamu

taamu

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Messages
5,952
Likes
1,881
Points
280
taamu

taamu

JF-Expert Member
Joined Dec 11, 2012
5,952 1,881 280
Haya mashamba MeTL ilipewa bure na sharti lilikuwa ayaendleze kwa kuyafanyia kazi wananchi wa eneo husika wapate ajira! Alipewa mashmba 21 lakini 12 yapo ni mapori tu na sheria usipo yaendeleza unanyang'anywa anapewa mtu mwingine anayeweza kuyafanyia kazi au wanapewa wananchi walime..! Sheria ni msumeno ila nakushangaa unapinga wananchi wa kawaida kabiba wasipewe ayo maeneo wafanyie shughuli za uzalishaji..? We wa wapi? Mtu anamiliki mashamba kila shamba lina ekari 12,000+ ..! Sasa 6 kanyang'anywa na sita kapewa onyo kama asipoyaendeleza yanarudishwa kwa wananchi.
Over
atekwe
 
jebs2002

jebs2002

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2008
Messages
5,933
Likes
3,765
Points
280
jebs2002

jebs2002

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2008
5,933 3,765 280
Anatapatapa, aende CDM apate cheo...
 
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
1,356
Likes
1,901
Points
280
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
1,356 1,901 280
Nape hata ajidai Mwema namna gani, simsamehi kosa la kukataa Bunge kwenda live kwa sababu za kijinga sana!
Hivi unaamini kabisa kwamba ni Nape ndie alikataa?! Kilichomponza Nape kwenye lile suala ni kuwa "speaker" ya serikali kuelezea issue husika! Lile suala ni Jiwe mwenyewe kwa 100%, na ndio maana ingawaje Nape kaondoka, lakini bado issue iko pale pale!
 
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
1,356
Likes
1,901
Points
280
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
1,356 1,901 280
jogi mshukuru Sky Eclat maana jamaa walishataka kuigeuza hoja.

Wengine walikuwa wadogo wakati baadhi ya ndugu wa Nape walipokuwa wanatumiwa na baadhi ya wana CCM kusema Nape si ndugu yao na wala si mtoto wa Marehemu Mzee Mussa (Moses) Nnauye.

Lile kasheshe lilikuwa kubwa sana kiasi kwamba na Kikwete naye aliingilia kati kuokoa Jahazi.
Tena siasa ilivyo ujinga, mmoja wa hao wana-CCM ni Mzee Yusuf Makamba! Nape alipomuuliza Mzee Makamba ikiwa yeye sio mtoto wa Mzee Nnauye ilikuwaje aliwezeza kwake (kwa mzee Makamba) lakini Mzee Makamba hakuwa na jibu!
 
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
1,356
Likes
1,901
Points
280
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
1,356 1,901 280
Kalazimishwa kuachia ngazi,huko si kujiuzulu.
Kuna jambo la msingi,limetegeshewa wanamfanyia timing wamfunge kwa goli la kichwa,ili kumaliza utata wa goli la mkono.Dead end.
Unaambiwa alilazimishwa baada ya KUGOMA kuondoa ambacho serikali walitaka aondoe! Alikuwa na uwezo wa kuendelea kubaki katika nafasi yake endapo angekubali! Ni vile tu watu mnajitia upofu, manake hata uwaziri aliupoteza kwa sababu tu aliamu kuunda tume dhidi ya Makonda wakati Jiwe alishatoa mwelekeo wa kupingana na hiyo tume lakini Nape hakusalimu amri!
 

Forum statistics

Threads 1,262,487
Members 485,588
Posts 30,123,570