Nape Nnauye ahojiwa na TAKUKURU kwa masaa 5

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
NAPE 'MBARONI': Takukuru yamshikilia Katibu Mwenezi CCM Nape Nnauye, yamhoji kwa saa 5 Lindi, adaiwa kutaka kuwahonga wajumbe Mtama, anakoomba kugombea ubunge.

Chanzo: Mwananchi


UPDATE:

USAHIHI

Kamanda wa Takukuru Lindi, S. Chami afafanua kuwa walimhoji Nape Nnauye, yabainika fedha alizochukua benki zilikuwa ni kwa ajili ya mawakala.
 
kweli nimeamini ndani ya ccm hakuna wa kumnyooshea mwenzake kidole,

nape huyu huyu alie kua anamnanga lowassa?

Wachenitu mh lowassa aende zake maana ndani ya ccm hakuna msafi kabisa,
 
90% ya wabunge wa CCM wanategemea rushwa kushinda uchaguzi wao.
TAKUKURU ingekuwa na meno hasa wangefungwa wengi sana mwaka huu.
 
Habari kutoka Lindi zinasema Katibu mwenezi wa CCm Nape Nnauye amehojiwa kwa masaa 5 na maafisa wa Takukuru wa Lindi kwa kutaka kuwahonga wajumbe wa uteuzi wa CCM katika jimbo la Mtama.

CCM bana!!!
 
Utatoaje Rushwa bila kuandaa mazingira ya utoaji Rushwa? sasa Laana ya Lowassa inamwandama huyu kijana,, hata huo Ubunge sijui kama ataupata....hivi upinzani hapo Mtama upoje? nani anagombea?
 
Back
Top Bottom