Nape, ndoto zako za kuwang'oa MAFISADI hazitatimia

Dec 11, 2010
3,321
6,328
Nape Mnauye baada ya kupewa jukumu la kuwa katibu mwenezi alianza kazi kwa moto na nguvu nyingi za soda huku akiamini anaweza kurudisha imani na taswira ya matumaini kwa chama chake, imani ambayo imeporomoka kuliko wakati wowote katika historia ya miaka 50 baada ya uhuru.

Kila alipopita alidiriki kujipa jukumu gumu na zito la kuhubiri kuwang'oa mapacha watatu kwa kibwagizo cha kujivua gamba ndani ya siku 90 ambazo bila shaka hata yeye mwenyewe anajua kuwa zimesha kwisha na hajafanikiwa kufanya chochote huku nguli hao wakiendelea kupeta.

Hivi karibuni alipofanya ziara kwenye vyombo vya habari, alipotembelea freemedia alisema "Ccm isipojivua gamba itajimaliza" ukumbuke wanao onekana magamba na wanaodhamiriwa kung'olewa ili kurejesha imani ya chama ni El, RA, na AC. Wengine wanao hisiwa ni zuga tu za kisanii ili kutengeneza urali kujifanya wanavuana magamba. Nasema ni zuga na usanii maana wenye magamba ni wengi si hao mapacha 3 tu.

Nani hajui kuwa Meremeta, Epa, Kagoda, Tangold na mikataba mibovu imebeba magamba mengi yanayohitaji kuong'olewa?!

Siku 90 zimesha kwisha na Ndoto ya Nape haijatimia kama alivyo ahidi huku akiamini kama alivyosema kuwa ccm wasipojivua gamba wamejimaliza, kujimaliza kuna tafsiri pana ambapo pia unaweza kusema ni kujiua. Siku zimeshafika na zinapita huku ndoto ikiwa haijatimia. Naweza kusema kama Nape aliamini kuwa ccm isipojivua gamba itajimaliza na yeye akiwa ni m-ccm aliyetaka kusimamia maamuzi magumu ya siku 90 na ameshindwa kufanya hivyo, basi ki mantiki na yeye anakufa bila ndoto zake kutimia. Chama kikifa kinazikwa kisiasa, lakini kwa vile chama ni pamoja na jumuiko la wanachama na viongozi basi hata ndoto za wanachama pamoja na viongozi zinapokwama nazo zinatumbukia kwenye shimo la mkwamo (kaburi la kisiasa) ambalo tayari Nape ameshatumbukiza miguu.

Buriani Nape Moses Mnauye, upumzishe ndoto zako kwa Amani mpaka siku zitakapo fufuliwa mbele ya haki.
Bwana ametwaa, bwana ametoa.
 
Tumeanza kumkopesha leo tunahesabu siku ya kwanza baada ya siku 90 kwisha (-1).
 
uandishi mbovu mno huu....

halafu kuwa sensitive,neno buriani linafaa zaidi kwenye kifo na sio
chuki za kisiasa.....

NAPE kwa position yake hawezi kubadili ccm....

katibu mwenezi ni msemaji tu.....

lakini huwezi kumshutumu kwa kushindwa kuibadili ccm
 
Ndugu yangu Ccm ni maneno no vitendo, wangekuwa watimiza maazimio na ndoto zao Tz ingekuwa juu sana in all aspects!
 
simply NAPE hana ubavu wa kumsurubu EL, wakati yupo primary watu walishajipanga.

In short NAPE + SITTA + Mwakyembe ( CCJ founders) hawawezi kupambana na wana mtandao ndani ya CCM.
 
Nape hawezi kufanya yaliyomshinda Mwenyekiti wake. Nape alikuwa anatafuta namna ya kujitafutia umaarufu. EL keshatuma salamu kwa JK kuwa aache usanii bali achukue hayo maamuzi magumu anayokusudia. Jk kagwaya kakaa kimya, sasa Nape aibu tupu!
 
kwani walitaja siku? inawezekana walisema 90units, so haijulikani ni masaa, siku, wiki, mwz au mwaka.
 
nape nilikuambia wewe ni matairi ya mbele ya gari angalia wenzako wameshafunga breki lazima usimame tu
 
Duuh, kumbe zimeisha siku tisini!!!!?
Ipo sababu lakini magamba lazima yaondolewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom