Kwani nafasi ya uvuvuzela inagombaniwa ama anapachikwa tu?
Mh! lipo jambo nyuma ya pazia, sio bure.
Ukiona hayo yanatokea kwenye TAASISI ujue imekaribia kufa.mbona kinana amesema amewaachia vijana?sasa vijana wanasema wanasimamia uchaguzi!hiki ni kizungumkuti.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
karibu cdm uje utubu
Nape ameamua kutogombea ujumbe wa NEC kwenye uchaguzi wa ndani ya chama hicho mwaka huu, baada ya kugombea kwa miaka kumi mfululizo na kushinda, sasa ameamua kutogombea ILI APATE MUDA WA KUSIMAMIA UCHAGUZI HUO VIZURI NDANI YA CHAMA..........." si rahisi kuwa refa na mchezaji kwa wakati mmoja, ukatenda haki ipasavyo, hivyo nimeona bora kutogombea ili nipate muda wa kutosha kusimamia mchakato, ili haki itendeke zaidi" alisema Nape.
Source. Habari Leo
Ni lazima awe M-NEC ili aweze kuendelea na nafasi hii aliyonayo ambayo kwa maoni yangu ameimudu sana. Sidhani kama JK halioni hili akashindwa kumteua kuwa MNEC kupitia zile nafasi za Mwenyekiti ambazo ni mahsusi kwa ajili ya wasaidizi wake wa karibu ndani ya CCM.Hivi asipokuwa mjumbe wa NEC nini hasara na faida yake?
Nape ameamua kutogombea ujumbe wa NEC kwenye uchaguzi wa ndani ya chama hicho mwaka huu, baada ya kugombea kwa miaka kumi mfululizo na kushinda, sasa ameamua kutogombea ILI APATE MUDA WA KUSIMAMIA UCHAGUZI HUO VIZURI NDANI YA CHAMA..........." si rahisi kuwa refa na mchezaji kwa wakati mmoja, ukatenda haki ipasavyo, hivyo nimeona bora kutogombea ili nipate muda wa kutosha kusimamia mchakato, ili haki itendeke zaidi" alisema Nape.
Source. Habari Leo
Unaongopa sana tu. Kwa nafasi yake ya sasa, Nape angeweza kugombea kupitia vile viti kumi vya Bara na angepita kwa kishindo kwa kuwa kura za mkutano mkuu wa CCM zinapigwa kiitifaki miaka yote ya chaguzi zao. Nape atateuliwa na Mwenyekiti mpya wa CCM ambaye tayari anajulikana.Nape hana jimbo la kugombea. Asiwadanganye. Alitaka kugombea ujumbe wa NEC kupitia wilaya ya Kinondoni – akajipima akaona hawezi kupenya. Hapa yupo Londa na mwanachama mmoja yule mwizi wa TRA.
Akataka kwenda Masasi, nako akakumbana na kizingiti kutoka kwa familia ya Mosesi Nnauye ambaye yeye anajiita mwanawe. Wale watoto wake na baadhi ya ndugu wa NNauye wamegoma kumtambua. Wanasema Nape siyo mtoto wao, bali ni mtoto wa yule waziri …..wa JK
Ndiyo sababu akajifanya ameamua kutogombea ili kusimamia uchaguzi.
Ndiyo kisingizio ambacho ameona aje nacho. Katibu mwenezi na kusimamia uchaguzi wapi na wapi? Uchaguzi unasimamia na ofisi ya katibu mkuu? Hata yeye naye akiamua hugombea. Ndivyo Makamba, Chiligati na wengine wote walivyofanya. Nape acha kuweweseka. Umeogopa muziki wa kamanda Lowassa.