Nape Moses Nnauye; Shujaa wa awamu kandamizi

Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
11,254
21,275
Hongera sana Nape, binafsi sijawahi kukupenda ila kwa hili nimekupenda sana na umejiwekea heshima ya hali ya juu. Maisha sio uwaziri. Maisha popote tu, wao wako wawili, sisi tuko wengi na tupo nyuma yako.

Tangu Juzi watu walikua wanakushauri ujiuzulu ili kulinda heshima yako ila nadhani wewe ulikua unaamini Magufuli ni yule yule ulimuhangaikia na kumpigania mpaka akafika hapo alipo. Ila sasa nadhani umeona rangi yake.

Sasa kabla hawajakuletea zengwe lingine fanya hivi, jitoe huko CCM, njoo CDM, trust me Ubunge unaupata tena asubuhi tu.

You did that for us.. yes sisi wanyonge.

Mungu akubariki na kukuinua zaidi.
 
Huu ujasiri wa Mhe. Nape wa kumgusa mtoto wa mtukufu kutetea utawala wa sheria bila kuhofia chochote kitakachompata amejijengea heshima vizazi vingi vijavyo. Tumezoea kuona viongozi wanafiki wanaojipenda nafsi zao na kupindisha ukweli ili kumpendeza rais. Nape ametumbuliwa kwa heshima kuu na ataenziwa na watanzania wapenda demokrasia na utawala wa sheria.
 
IMG-20170323-WA0049.jpg
 
Hana lolote zaidi ya visasi
 
.
MY HERO OF THE SEASON

Katika hili, ninamtangaza rasmi Nape Moses Nnauye kuwa SHUJAA WANGU wa msimu.

Usiponielewa sasa, utaelewa baadaye......
Hongera sana Nape!!!! Wewe ni Shujaaaa sana, umesimama kwenye ukweli na Jamii nzima inajua!!!!!!…
tmp_13249-Screenshot_2017-03-23-09-14-03-115561217.png
 
EL hakuwahi kuwa critcise waliokuwa wakiwapiga mabomu wapinzani lakini alipogundua makosa yake na kutubu alisamehewa, hivyo hivyo kwa hili makosa ya Nape yaweza kusamehewa pia.
Kikubwa kaitendea haki nafsi yake, sometimes it's better to swallow your pride and realize the fact that we are all equal before our creator ...hence tell the TRUTH!
 
Nape siyo aina ya viongozi wa kujipendekeza kama Mabashite.. Nape Nnauye big up brother Taifa zima la Tanzania lipo nyuma yako.. Achana na hao wazee wa shilawadu

Tangu awamu hii ya tano Nape amebadilika sana cjawahi kumkubali lakn this time nimemkubali hongera sana

Maisha siyo uwaziri tu
 
Huu ujasiri wa Mhe. Nape wa kumgusa mtoto wa mtukufu kutetea utawala wa sheria bila kuhofia chochote kitakachompata amejijengea heshima vizazi vingi vijavyo. Tumezoea kuona viongozi wanafiki wanaojipenda nafsi zao na kupindisha ukweli ili kumpendeza rais. Nape ametumbuliwa kwa heshima kuu na ataenziwa na watanzania wapenda demokrasia na utawala wa sheria.
Makosa yote ya nyuma yanafutwa na ujasiri aliouonyesha wa kupigania utawala bora na demokrasia. Hii ni zaidi ya toba, hasa katika kipindi hiki cha kwaresma. Bravo!.
 
Mara hii watu wamesahau aliyoyasema kuhusu Bunge Mubashara !!!
Daaaaa.... Hakuna fadhila dunia hii...... Katika uchaguzi alifanya mangap uyu bab jaman..... Atumbuliwe penye kosa basi sasa hata ili kweli... Halafu jumapili watu wataenda kupiga magoti kanisan wakisali. Unafki wa hali ya juu. Ila Mungu ni wetu sote
 
Tumuunge mkono na kutia moyo NAPE kwa kutumia HASHTAG#SALUTENAPE#HASHTAG Katika kula post hapa jf kwenye forums zote!
Nguvu iko kwa wananchi wala si kwa mtu mmoja! Nape uwe na amani, tulia, usijibu, chukua mfano wa utulivu wa Lowasa!
Elekeza nguvu zako jimboni na elekeza hekima yako bungeni! Mchango wako bungeni ni muhimu!
Usiwaze kuhama chama maana tunakuhitaji bungeni!
Ikifika 2020 baada ya bunge kuvunjwa akili kichwani! Jimbo tutakupa kwenye chama chochote utakachokuwa isipokuwa magamba!
 
Back
Top Bottom