kapotolo
JF-Expert Member
- Sep 19, 2010
- 3,727
- 2,213
Nape Moses Nnauye ambaye siku za hivi karibuni alikuwa akipita huku na kule akiwananga mapacha watatu kwamba ni magamba, ndio yamechangia kuipa CCM ushindi mdogo, na kwamba lazima waondoke CCM. Moja ya magamba hayo ni Rostam Aziz.
Katika hatua inayoonyesha unafiki wa Nape na uongo wake uliotukuka wa kuwahadaa wananchi wa Igunga, Nape ameanza kumsifia Rostam Aziz huku akiomba watu wasimbeze kwa kuwa amefanya makubwa huko Igunga. Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania la leo, Nape amesema kazi aliyoifanya Rostam ndio kigezo cha ushindi wao huo Igunga.
Naomba watu wa Igunga msidanganyike tafadhali, huu uongo wa CCM wa kujipendekeza siku za uchaguzi unatakiwa ukataliwe kwa vitendo kwa kuwakataa huko Igunga. Nape anawafanya watanzania ni wajinga, kwamba anaweza kusema chochote leo na kesho akasema kingine na watu wakamsikiliza. Nape siasa za kuhadaa watu hazina nafasi kwenye dunia ya sasa, acha unafiki wako.