Nape: Mleteni Slaa Arumeru, Asema CCM wanakesha wakiomba aruhusiwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape: Mleteni Slaa Arumeru, Asema CCM wanakesha wakiomba aruhusiwe

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by TONGINDI, Feb 18, 2012.

 1. T

  TONGINDI Senior Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]Nape: Mleteni Slaa Arumeru
  • Asema CCM wanakesha wakiomba aruhusiwe

  na Mwandishi wetu


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, kusema ni ruksa kwa Katibu Mkuu wao, Dk. Willibrod Slaa, kugombea ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki, Chama cha Mapinduzi (CCM), kimejibodoa kuwa kinamsubiri kwa hamu.
  Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, alisema kuwa CCM wanaomba usiku na mchana Dk. Slaa agombee katika jimbo hilo ili wamalize kazi ya uchaguzi mkuu 2015.
  Kwa kujiamini, Nape alisema kuwa Dk. Slaa akitia mguu Arumeru Mashariki, haponi, hivyo utakuwa mwisho wake kisiasa na umaarufu wa CHADEMA.
  “Dk. Slaa ndiye jembe la CHADEMA, akija Arumeru Mashariki, tutahakikisaha tunalikata makali na tukishafanya hivyo hawezi tena kuwa maarufu mwaka 2015 na chama kizima hakitakuwa na nguvu, hapo kazi yetu ni nyepesi kama kumsukuma mlevi,” alisema Nape.
  Alipoulizwa endapo kauli hiyo ni ya woga dhidi ya Dk. Slaa ili kiongozi huyo asiende Arumeru, Nape alijibu kwa kujiamini kuwa CHADEMA ikitaka kuthibitisha hilo, imlete kigogo huyo katika jimbo hilo.
  Aliongeza kuwa umaarufu wa CHADEMA unatokana na mtu mmojammoja kama Dk. Slaa na kutamba kuwa kiongozi huyo ni maarufu awapo bungeni, hivyo watahakikisha anashindwa ili uwe mwisho wake kisiasa na chama chake.
  Hata hivyo, pamoja na kauli hizo za majigambo ya Nape, Dk. Slaa amekwishatoa msimamo wake kwamba hakakuwa tayari kuwani ubunge katika jimbo lolote kwa wakati huu.
  Tangu kuanza kwa harakati za kuwania ubunge katika jimbo hilo, Dk. Slaa amegusa hisia za wasomi wanaharakati na makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo wafuasi wa chama chake, wakimtaka agombee kiti hicho.
  Matakwa hayo ya kumtaka Dk. Slaa agombee, yanatokana na imani kwamba kulingana na umaarufu aliojijengea na rekodi yake ya utendaji wenye audilifu, CHADEMA haitapata ushindani mkubwa toka kwa CCM.
  Itakumbukwa kuwa Dk. Slaa aligombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita na kukonga nyoyo za Watanzania wengi ambao hadi sasa wanaamini kuwa aliibuka mshindi ila kura zake zilichakachuliwa.
  Hisia za wanaotaka Dk. Slaa agombee ubunge katika jimbo hilo, zimechochewa zaidi na kauli ya Mbowe, aliyekaririwa na gazeti moja akisema kama kiongozi ataamua kuwania kiti hicho, CHADEMA itaheshimu uamuzi wake.
  Mbowe pia alisema kama Dk. Slaa hatakuwa tayari, chama vilevile hakiwezi kumlazimisha kugombea. Akitamba kuwa hana shaka ya kukubalika kwake na imani aliyojijengea mwanasiasa huyo kwa Watanzania.
  Mwenyekiti huyo alifafanua kuwa katika kuteua mgombea, CHADEMA inazingatia vigezo na si suala la uteule.
  Na wakati akisema hivyo, aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo katika uchagzu mkuu uliyopita, Joshua Nasari, alisema endapo Dk. Slaa ataamua kugombea na chama kikampitisha, ataridhia.
  Uchaguzi huo unaotarajia kufanyika Aprili mosi mwaka huu, umetokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Jermiah Sumari (CCM).
  Tayari harakati za kuchukua fomu zimeanza ndani ya vyama vya siasa huku kila kimoja kikitamba kulinyakua hasa mchuano mkali uko kwa CCM na CHADEMA vinavyopewa nafasi kubwa ya ushindi.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  aende yeye arumeru na sisi tumpeleke Slaa..tunakesha tukiomba
   
 3. r

  rZiKY Member

  #3
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmh nape hamna k2 apo..izo ni dalili waza anajua Slaa akigombea anapita so anatanguliza vitisho jembe lisigombee...
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  sijawahi kuona vijana hovyo kama hawa watu wawili:
  1) Nape
  2) Jussa
   
 5. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Atakufa na presha Dr Slaa kwani kupigwa ni lazima Arumeru
   
 6. REBEL

  REBEL Senior Member

  #6
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  umemsahau lusinde,makamba senior
   
 7. Nyamburi

  Nyamburi JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nnauye Nape!gambaz vp wahusika washavuliwa gambaz,au ulimaanisha wamepewa miaka 90 na si siku 90?
   
 8. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nape ni mmoja wa watu wanaoamini wasichokiamini.
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Mnamuongelea nnauye yupi?

  Kama ni yule mtoto wake wa singida hana kitu ila kama ana mwingine tuanze kujadili.
   
 10. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mie sipo nilikuwa napita, HATAHIVYO DR Slaa alishasema hawezi kurudi nyuma, HIVI Leo anapokea m,ilioni 12 pasipo kodi, ubunge atapokea hizo na kodi juu
   
 11. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu naye mropokaji akifuatiliwa anakana ID yake humu.
   
 12. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Ndg yangu Nape chunga kauli zako za kuropoka, unajishushia heshima. Hii inakuongezea nini kwenye kazi yako ya itikadi na uenezi wa CCM? Watch it out brother!
   
 13. O

  Omr JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nape amesema ukweli kabisa, na Slaa alishaona hii lasivyo angejitokeza kugombea hicho kiti.
   
 14. Higash

  Higash JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  kauli ya woga hii
   
 15. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Nape nina nafasi moja ya kazi ya Upishi, Send your CV please....
   
 16. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kwanini huyo nape asigombee kwa tiketi ya ccm?
   
 17. SAMMY DANNY

  SAMMY DANNY Member

  #17
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape ajui kuwa Slaa ana kisimat umaarufu wake hauwezi kushuka kwa ubunge wa Arumeru, anaogopa kiama cha si si em iwapo Dr. atagombea 2015. Tayari homa ya uchaguzi 2015 ishampanda na anajua kitakachotokea ktk chama chake ndio maana anajihadhari mapema.
   
 18. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #18
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Dr anaimarisha chama na kupika vijana kuwa viongozi.
   
 19. g

  greenstar JF-Expert Member

  #19
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nape anafanya kazi yake ya kichama tuache dharau na matusi....hata SIMBA na YANGA huwa wanatambishiana hivyo hivyo .Binafsi sipendi matusi na dharau kwa bwana NAPE. NAPE amethubutu kupambana na LOWASA wazi wazi ,huku wengine tukiishia kusema MAFISADI.Je Mafisadi hawana majina? Pia NAPE ameweka ID yake humu JF bila kificho huku wengine tukijificha nyuma ya PAZIA,je hapa nani MNAFIKI ?????????????????

  NAPE anaweza kujenga chama akipewa rungu bila kuhofia usalama wake...BRAVO NAPE
   
 20. C

  Chief mangi Member

  #20
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape amepinda kweli. Hebu aende yeye na sisi tumpeleke slaa aone moto wake.kumbe nnape sio katibu mwenezi wa sera ma itikadi tu. Pia ni mwenezi wa uzush na propaganda ccm mhh amekwisha.
   
Loading...