Nape, Mchemba washtakiwa kwa Pinda bungeni

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
na Tamali Vullu, Dodoma

MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid (CUF), amemshtaki Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwa kumkejeli Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, na muundo wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Alisema hivi karibuni Nape alikaririwa katika vyombo vya habari akimkejeli Maalim Seif wakati Rais Jakaya Kikwete alipongeza juhudi hizo zilizofikiwa na viongozi hao huko Zanzibar.

Katika swali lake, mbunge huyo wa Zanzibar alitaka kujua serikali itatoa kauli gani kuhusu suala hilo.

Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu alieleza kushangazwa na mbunge huyo kutomweleza suala hilo, kwani ni rafiki yake sana na wamekuwa wakikutana mara kwa mara.

Hata hivyo Pinda aliwashangaa Watanzania wanaokejeli hatua hiyo na kueleza kwamba Mtanzania yeyote aliyekuwa akifuatilia siasa za Zanzibar, hawezi kukejeli hatua hiyo.

"Hatua iliyofikiwa ni mfano wa kuigwa na watu hao ni viongozi wa serikali; kama kuna mtu anakejeli ninong'oneze," alisema Pinda na hivyo kumfaya mbunge huyo kumtaja Nape na Mwigulu Mchemba (Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM) na kusema kuwa wamekaririwa kwenye magazeti wakikejeli hatua hiyo.

Hata hivyo Pinda alipotajiwa majina hayo alionekana kugwaya na kusema kama suala hilo liko kwenye magazeti si la kutiliwa maanani.

"Mimi naamini sana runinga kwa sababu namuona mtu mwenyewe, lakini kwenye magazeti inategemea ni gazeti gani. Magazeti mengine yana ajenda zao," alisema na kuahidi kulifuatilia suala hilo.

Hivi karibuni Nape alikaririwa na vyombo vya habari akimmbeza Maalim Seif kuwa njaa yake ndiyo iliyomfanya aitambue Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na hatimaye kukubali kuingia kwenye serikali ya mseto.

Nape ambaye alikuwa akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wenye lengo la kuelezea maana ya CCM kujivua gamba uliofanyika jijini Mbeya, alisema baada ya Hamad kubanwa na njaa kali aliamua kurudi kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kudai alipwe mafao yake kama Waziri Kiongozi wa serikali hiyo, wakati haitambui SMZ.

Naye Mwigulu Mchemba, alisema viongozi wengi wa kisiasa nchini hawana moyo wa kuwatumikia wananchi kwa dhati na badala yake wanafikiria maslahi yao binafsi huku, akimtolea mfano Maalim Seif kuwa ni mfano wa viongozi hao.
 
Lakini huo ndiyo ukweli aliongea Nape wadanganyika tu ndiyo hawajui hilo
 
hivi bado kuna watu wanaamini muafaka na kama huyohuyo m/kiti wenu anaulizwa na mwandishi wa itv kwa mfano unaambiwa ujiunge na ccm utakubali jamaa anasema ndio nakubali ila wanipe uenyekiti tu afu mh wa wawi hamad rashid bado unakuwa na imani nae..ni hayo tu!
 
huyu nchemba tuna wasiwasi kuanzia majina yake, mnyiramba kuwa na majina yote ya kisukuma.
 
Hamad, hayo mlijitakia wenyewe, ccm wanafiki wakubwa! Hawawezi kuwa waaminifu kwa lolote, ni jeuri siku zote. Walikuwa na sababu gani kumtukana sefu hamadi? Nilimsikia Nape, akitukana kwenye mkutano wa hadhara Ruanda Nzovwe mbeya bila ya aibu yoyote.
 
Hii habari jinsi ilivyokuwa inatangazwa kutwa nzina jana na TBC inapotosha ukweli nani alikebehi huu mwafaka; maana habari inasema Waziri Mkuu amesikitishwa na vyama vinavyokebehi mwafaka......badala ya kutaja kabisa nani alikebehi
 
Back
Top Bottom