Nape: Lowassa ni Kunguru hafugiki

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Watasema nini baada ya Lowassa kurudi CCM?

Monday March 11 2019

LOWASAAA+P.jpg

Kwa ufupi
  • Edward Lowassa ambaye amekuwa akibadili mwelekeo wa kisiasa, ambapo Julai 28, 2015 alitoka CCM na kwenda Chadema kisha Machi mosi, 2019 akatangaza kurudi CCM, kumekuwapo na kauli mbalimbali za wanasiasa kumzungumzia, lakini swali linabaki kwa wakati huu watasema nini?

By Kalunde Jamal, Mwananchi kjamal@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Miongoni mwa viongozi wa vyama ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakichafuliwa na kusafishwa na watu haohao ni pamoja na Edward Lowassa.
Wakati akiwa CCM kabla ya kutimkia Chadema Julai 28, 2015 alikuwa akinangwa kwa ufisadi, papo hapo alipohamia Chadema aliendelea kuitwa fisadi na watu wa CCM huku watu wa Chadema wakimsafisha, lakini hivi sasa amerudi CCM watasema nini?
POLEPOLE.jpg

Mnamo Septemba 29, 2015 Humphrey Polepole akiwa kwenye kipindi cha Mada Moto kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Channel 10 alisema Lowassa ni tajiri hana uhusiano na masikini na hahitaji kusafishwa kisheria kama ambavyo Chadema walikuwa wanadai kwamba kama ana hatia ya ufisadi inayosemwa apelekwe mahakamani.
Alitoa kauli hiyo mara baada ya kiongozi huyo kuhamia Chadema na chama hicho kutumia nguvu nyingi kumsafisha kutoka kwenye dimbwi la tuhuma za ufisadi alizokuwa akishutumiwa.
Kwa upande wa katibu mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba alikuwa akieleza udhaifu wa Lowassa katika mikutano ya kisiasa wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015.

makongoro.jpg

Akiwa kwenye kampeni sehemu mbalimbali aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Makongoro Nyerere alisema Tanzania inakabiliwa na tatizo la ufisadi na rushwa.
Alisema kwa kuwa ufisadi bado ni tatizo, wataendelea kuwaeleza Watanzania katika kampeni zao kuwa mgombea huyo wa Chadema ni fisadi.

Lowassa amekuwa na nia ya kugombea urais kwa muda mrefu tangu mwaka 1995 wakati jina lake lilipokatwa, hakuchukua fomu mwaka 2005 wakati Jakaya Kikwete, aliyekuwa rafiki yake wa karibu, alipogombea.
Lowassa alisema walikubaliana na Kikwete kwamba waunganishe nguvu ili awamu inayofuata iwe zamu ya mbunge huyo wa Monduli.
Hata hivyo, mwaka 2015 jina la Lowassa lilikatwa na makada wengine 33 na ndipo akaamua kujiunga na Chadema kuendeleza ndoto yake ya kuingia Ikulu.
Septemba 29, 2015 aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya CCM, Nape Nnauye akiwa kwenye viwanja vya Samora, mjini Iringa alitumia dakika 10 kumshambulia Lowassa.
Alisema Lowassa ni mwizi na fisadi na kwamba hakuna sehemu ambayo alipewa kufanya kazi katika ngazi za CCM na Serikali bila kuiba.
NAPE.jpg

Nape alidai Lowassa alishindwa kukaa CCM kwa kuwa hawezi kufugika "Lowassa ni kunguru, hafugiki."
MUSUKUMA.jpg

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita ambaye sasa ni mbunge wa Geita, Joseph Msukuma naye alimvaa Lowassa alipohamia Ukawa kwa kusema kuwa wanashukuru chama kimetua mzigo.

“Nataka nimwambie ndugu yangu, rafiki yangu Lowassa, huu ni muziki mkubwa,” alisema Msukuma kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea wa urais wa CCM, Dk John Magufuli uliofanyika mjini Chato, mkoani Geita Septemba 21, 2015.

“Tunaomba wachukue na wengine wenye tabia kama hizo. Wenye akili timamu tutabaki CCM...Mgombea wetu (Magufuli) anatosha. Na hapa ndiyo kwao, nimetembea na Lowassa gari moja, ndege moja, tunachagua rais na sio bora rais,” alisema.

“Katika Kanda ya Ziwa, hakuna aliye na siri za Lowassa kama mimi, naomba waniweke kwenye mdahalo nitagharimia, niwapige kavu kavu. Watu wanaokwenda kule (Ukawa) zinatangulizwa hela. Nani anachukia hela?.”
Mara baada ya Lowassa kwenda Ikulu kuzungumza na Rais Magufuli, Msukuma alibadilika na kumuasa kuwa, “Mi nakuomba Mzee Lowassa huku ndiyo kwenu hilo genge la wahuni hutoliweza, Lowassa kwenda kule ilikuwa ni hasira tu.”
MWAKYEMBE.jpg

Naye Dk Harrison Mwakyembe akiwa Waziri wa Afrika Mashariki, alitoa andiko la kujiapiza kupambana kufa na kupona kuhakikisha Lowassa haingii Ikulu.
Katika andishi lake alilolituma kwenye mitandao ya kijamii, Dk Mwakyembe anasema, Lowassa hana sifa ya kuwa Rais.
“Namuona Lowassa kama mtu ambaye anatapatapa huku akiujua ukweli kwamba hana nafasi hata kiduchu ndani ya CCM.”
Alisema anahaha kutumia mabilioni kuhonga na kusafirisha watu kwenye tendo la kutangaza nia tu, hivi unafikiri kamati zote za CCM zina njaa ya pesa zako za kifisadi?

Dk Mwakyembe ambaye sasa ni waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na Michezo alisema
atakuwa wa kwanza kujitafakari na kuitafakari CCM na kuchukua hatua ambayo najua Watanzania wasiouza utu wao kwa dhamana ya fedha.
“Ninakusubiri kwa hamu ili nikusikie utakavyokuwa unabadili jahanam kuwa peponi, kwa manufaa ya Watanzania nitaanika hadharani uozo wako wote kwa ujasiri na bila hata chembe ya woga ili Watanzania wasipotoshwe tena kwa njia ya bwembwe za fedha,” alisema.
zitto.jpg

Kiongozi wa ACT- Wazalendo Zitto Kabwe akiwa Singida kwenye mkutano wa kampeni Agosti 7, 2015 alisema ni kazi ngumu kumsafisha Lowassa kutokana na kuwa na kashfa za ufisadi.
Hizi ni baadhi ya kauli za wanasiasa hawa kuhusu Lowassa, swali linabaki kwa sasa baada ya kurejea CCM watakuwa na kipi cha kusema juu ya mwanasiasa huyu?
 
Mtu anaweza akapoteza mda na lengo katika kuchambua sababu zilizomfanya Lowassa arudi nyumbani.

Kuna mambo yanayoweza kutoa mwelekeo wa kuhama huko.

Kwanza kabisa inaonekana palikuwa na ushawishi mkubwa toka CCM mzee huyo ahame. Matakwa haya sababu zake zinaweza zikafikilrika.
Ni ajabu sana timu yote nzima ya uongozi wa juu wa CCM kuweka mapokezi kiasi kile kwa mtu ambaye walishajua wamemmaliza.
Hapa ndipo palipo siri nzito!
Mapokezi yale yanaonyesha dhahiri, kuhama kule hakukuanzia kwa Lowassa. Walimtaka sana ahame; sababu, hatujui!

Sasa ukifikiria, kati ya Lowassa na Nnauye, ni nani mwenye thamani kubwa ndani hicho chama?
Sina hakika sana kama Nnauye angehama na kurudi chamani angepata mapokezi kama aliyopewa Mzee Lowassa.

Kuna jambo wana hofu nalo linalomhusisha Lowassa kuelekea 2020?
 
Kumbuka kauli ya Kikwete kutaka kulivua gamba. Kulivua gamba ilikuwa ni kuwafukuza ccm mafisadi waliokuwa wanakichafua chama wakiwemo Lowassa, Rostam, Chenge na wengineo. Nape hajawahi kutukanwa ndani ya ccm kama alivyotukanwa fisadi lowassa. Unafiki umepitiliza ndani ya ccm vinginevyo huyu mtu aliyetukanwa na hakuna yoyote yule aliyemtetea ndani ya ccm hawakustahili kumpokea.

Watu tunakosea sana kuwapa watu kama hawa cheo cha "Mwanasiasa". Ni aibu!

Dk Mwakyembe ambaye sasa ni waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na Michezo alisema atakuwa wa kwanza kujitafakari na kuitafakari CCM na kuchukua hatua ambayo najua Watanzania wasiouza utu wao kwa dhamana ya fedha.

Hivi mtu na akili zake timamu anawezaje kuwapa kura watu kama hawa!
 
Unafiki umepitiliza ndani ya ccm vinginevyo huyu mtu aliyetukanwa na hakuna yoyote yule aliyemtetea ndani ya ccm hawakustahili kumpokea.
Hapana, kama nilivyoeleza hapo juu, ni ziada ya "unafiki". Kunajambo mhimu zaidi linaloweka msukumo Mzee arudi nyumbani. Si jambo la kawaida, kama unafiki. Kuna aina ya hofu.
 
Kumbuka kauli ya Kikwete kutaka kulivua gamba. Kulivua gamba ilikuwa ni kuwafukuza ccm mafisadi waliokuwa wanakichafua chama wakiwemo Lowassa, Rostam, Chenge na wengineo. Nape hajawahi kutukanwa ndani ya ccm kama alivyotukanwa fisadi lowassa. Unafiki umepitiliza ndani ya ccm vinginevyo huyu mtu aliyetukanwa na hakuna yoyote yule aliyemtetea ndani ya ccm hawakustahili kumpokea.
ILA nyie wanasiasa ni wanafiki mliotukuka aisee! Hakuna wa CCM wala vyama visivyo na dola a.k.a wapinzani, nyote mmejaa unafiki uliopitiliza.

Lowasa akiwa CCM mlimuona tishio kwa style yake mkaisema ya ufisadi mkubwa mkapiga kelele kila Kona mkijinadi na ushahidi mnao mbinguni na duniani na CCM ikimuweka mtu mchafu kugombea urais ni sawa na kunajisi ikulu, CCM Kwa namna yake wakampiga chini asigombee Kwa chama Chao....

wapinzani kwenu ikawa fursa mkamsafisha Kwa UBATIZO wa Moto hamkutaka kuhojiwa kana kwamba ninyi ndio mitume na manabii na makuhani wenye kutakasa dhambi, amegombea kwenu mmemsafisha Kwa gharama zote ikiwemo kuwapoteza wanachama wenu, sasa CCM wakaanza nao kuwarushia madongo juu ya unafiki wenu lakini mlipotezea kimyaaaa, Leo jamaa kawarudia tena CCM ambao walirithi propaganda zenu za kumdhalilisha lowasa nanyi mmeanza tena kumsema na bahati mbaya sana mnabadilisha magoli kana kwamba hii hoja ni ya CCM hapo awali kumbe miaka zaidi ya nane kabla hamjampokea kuwa mgombea wenu mlimsema vibaya Sana.
Sasa unapo nukuu kauli za Wana CCM waliomnanga lowasa usiwe mnafiki Kwa kuacha kuzinukuu kauli za wanaukawa waliomnanga lowasa kisha wakamsafisha akawa mgombea wao.

Japo wapo mazwazwa wanachezeshwa ngoma zenu ila wenye akili timamu na upeo huru wa kuchanganua mambo hatokaa awape nafasi ya uaminifu tena, ninyi nyote wanasiasa wabinafsi na wanafiki Kwa kiwango kisichoelezeka.

Na hizi siasa zenu za kuchafuana na kukomalia hoja chafuzi hata kama mnajuwa ni uwongo mtupu kuna siku watanzania watazinduka mtawaelewa tu endeleeni kuwatumia mkiwachezesha ngoma zenu haramu.
 
Kumbuka kauli ya Kikwete kutaka kulivua gamba. Kulivua gamba ilikuwa ni kuwafukuza ccm mafisadi waliokuwa wanakichafua chama wakiwemo Lowassa, Rostam, Chenge na wengineo. Nape hajawahi kutukanwa ndani ya ccm kama alivyotukanwa fisadi lowassa. Unafiki umepitiliza ndani ya ccm vinginevyo huyu mtu aliyetukanwa na hakuna yoyote yule aliyemtetea ndani ya ccm hawakustahili kumpokea.
Chadema hawakumtukana lowasa zaidi ya miaka nane walimtaja kuwa ni fisadi papa na kisha wakampokea agombee urais?
Huo unafiki wa chadema huuoni au ndio kujitia upofu Tu kutokana na mahaba ya chama?
Hebu balance unafiki wenu ninyi wanasisa na wapiga debe wa siasa, nyote mko na viwango vya juu Sana vya unafiki bila kumung'unya maneno..
Weka nukuu za wakina lema na msigwa na wengineo waliompaka matope lowasa na kisha ulete walivomsifia akiwa kwao na ulete kauli zao za sasa.
Kuna wakati hao CCM wanaweza kuwa Bora kuliko wapinzani wasiojielewa wanataka nini...labda ni chuki na wivu wakati mwingine zinaendesha hisia zenu kisiasa maana haiingii akilini mtu huyo huyo akiwa kwenu anakuwa msafi akienda upande wa pili anakuwa mchafu sana....hii double standard sijui kama mnaiona na kama si miongoni mwao ulipaswa kuleta uchambuzi wa pande zote zilivoshiriki unafiki dhidi ya lowasa na sio kuona pande moja kwakuwa uko upande huo....wewe pia ni zaidi ya mnafiki tena mnafiki kiwango cha uchawi wa mchana....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungekuwa unajua nilichowahi kuandika humu kuhusu lowassa kuja Chadema mara nyingi tu humu usingeandika huu upumbavu wako.

Kwasababu ya upofu na upumbavu uliokujaa mpaka unyayoni umeshindwa kuelewa mantiki ya nilichoandika lofa wewe...
Nimekuambia uache unafiki balance mipasho yote uliyoitoa wewe na wanasiasa wenzio wa CCM na chadema dhidi ya lowasa kisha uiweke na sio kuusema upande mmoja...
Ikiwa unajisema ulizungumza mabaya ya lowasa kipindi hicho maana yake wewe pia ni miongoni mwa wasio CCM walimsema lowasa na yet lowasa akaja upande wenu mkaona swadakta kabisa ila leo amerudi CCM unajifanya wataka uwasemee CCM pekee kwamba ndio walimsema...Acha hizo wote ninyi mlimsema Kwa mabaya mliyoyaweka hadharani hivyo usiuhukumu upande aliorudi sasa kana kwamba wao hawastahili kumpokea isipokuwa ninyi...acha unafiki
Wanasema haki inadaiwa na walio na mikono safi lakini pia kabla hujatoa kibanzi Kwa jicho la mwenzio hebu ondoa boriti Kwa jicho lako...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sasa ccm hakuna aliye msafi ndani ya ccm by UVCCM
Watasema nini baada ya Lowassa kurudi CCM?

Monday March 11 2019

LOWASAAA+P.jpg

Kwa ufupi
  • Edward Lowassa ambaye amekuwa akibadili mwelekeo wa kisiasa, ambapo Julai 28, 2015 alitoka CCM na kwenda Chadema kisha Machi mosi, 2019 akatangaza kurudi CCM, kumekuwapo na kauli mbalimbali za wanasiasa kumzungumzia, lakini swali linabaki kwa wakati huu watasema nini?

By Kalunde Jamal, Mwananchi kjamal@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Miongoni mwa viongozi wa vyama ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakichafuliwa na kusafishwa na watu haohao ni pamoja na Edward Lowassa.
Wakati akiwa CCM kabla ya kutimkia Chadema Julai 28, 2015 alikuwa akinangwa kwa ufisadi, papo hapo alipohamia Chadema aliendelea kuitwa fisadi na watu wa CCM huku watu wa Chadema wakimsafisha, lakini hivi sasa amerudi CCM watasema nini?
POLEPOLE.jpg

Mnamo Septemba 29, 2015 Humphrey Polepole akiwa kwenye kipindi cha Mada Moto kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Channel 10 alisema Lowassa ni tajiri hana uhusiano na masikini na hahitaji kusafishwa kisheria kama ambavyo Chadema walikuwa wanadai kwamba kama ana hatia ya ufisadi inayosemwa apelekwe mahakamani.
Alitoa kauli hiyo mara baada ya kiongozi huyo kuhamia Chadema na chama hicho kutumia nguvu nyingi kumsafisha kutoka kwenye dimbwi la tuhuma za ufisadi alizokuwa akishutumiwa.
Kwa upande wa katibu mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba alikuwa akieleza udhaifu wa Lowassa katika mikutano ya kisiasa wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015.

makongoro.jpg

Akiwa kwenye kampeni sehemu mbalimbali aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Makongoro Nyerere alisema Tanzania inakabiliwa na tatizo la ufisadi na rushwa.
Alisema kwa kuwa ufisadi bado ni tatizo, wataendelea kuwaeleza Watanzania katika kampeni zao kuwa mgombea huyo wa Chadema ni fisadi.

Lowassa amekuwa na nia ya kugombea urais kwa muda mrefu tangu mwaka 1995 wakati jina lake lilipokatwa, hakuchukua fomu mwaka 2005 wakati Jakaya Kikwete, aliyekuwa rafiki yake wa karibu, alipogombea.
Lowassa alisema walikubaliana na Kikwete kwamba waunganishe nguvu ili awamu inayofuata iwe zamu ya mbunge huyo wa Monduli.
Hata hivyo, mwaka 2015 jina la Lowassa lilikatwa na makada wengine 33 na ndipo akaamua kujiunga na Chadema kuendeleza ndoto yake ya kuingia Ikulu.
Septemba 29, 2015 aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya CCM, Nape Nnauye akiwa kwenye viwanja vya Samora, mjini Iringa alitumia dakika 10 kumshambulia Lowassa.
Alisema Lowassa ni mwizi na fisadi na kwamba hakuna sehemu ambayo alipewa kufanya kazi katika ngazi za CCM na Serikali bila kuiba.
NAPE.jpg

Nape alidai Lowassa alishindwa kukaa CCM kwa kuwa hawezi kufugika "Lowassa ni kunguru, hafugiki."
MUSUKUMA.jpg

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita ambaye sasa ni mbunge wa Geita, Joseph Msukuma naye alimvaa Lowassa alipohamia Ukawa kwa kusema kuwa wanashukuru chama kimetua mzigo.

“Nataka nimwambie ndugu yangu, rafiki yangu Lowassa, huu ni muziki mkubwa,” alisema Msukuma kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea wa urais wa CCM, Dk John Magufuli uliofanyika mjini Chato, mkoani Geita Septemba 21, 2015.

“Tunaomba wachukue na wengine wenye tabia kama hizo. Wenye akili timamu tutabaki CCM...Mgombea wetu (Magufuli) anatosha. Na hapa ndiyo kwao, nimetembea na Lowassa gari moja, ndege moja, tunachagua rais na sio bora rais,” alisema.

“Katika Kanda ya Ziwa, hakuna aliye na siri za Lowassa kama mimi, naomba waniweke kwenye mdahalo nitagharimia, niwapige kavu kavu. Watu wanaokwenda kule (Ukawa) zinatangulizwa hela. Nani anachukia hela?.”
Mara baada ya Lowassa kwenda Ikulu kuzungumza na Rais Magufuli, Msukuma alibadilika na kumuasa kuwa, “Mi nakuomba Mzee Lowassa huku ndiyo kwenu hilo genge la wahuni hutoliweza, Lowassa kwenda kule ilikuwa ni hasira tu.”
MWAKYEMBE.jpg

Naye Dk Harrison Mwakyembe akiwa Waziri wa Afrika Mashariki, alitoa andiko la kujiapiza kupambana kufa na kupona kuhakikisha Lowassa haingii Ikulu.
Katika andishi lake alilolituma kwenye mitandao ya kijamii, Dk Mwakyembe anasema, Lowassa hana sifa ya kuwa Rais.
“Namuona Lowassa kama mtu ambaye anatapatapa huku akiujua ukweli kwamba hana nafasi hata kiduchu ndani ya CCM.”
Alisema anahaha kutumia mabilioni kuhonga na kusafirisha watu kwenye tendo la kutangaza nia tu, hivi unafikiri kamati zote za CCM zina njaa ya pesa zako za kifisadi?

Dk Mwakyembe ambaye sasa ni waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na Michezo alisema
atakuwa wa kwanza kujitafakari na kuitafakari CCM na kuchukua hatua ambayo najua Watanzania wasiouza utu wao kwa dhamana ya fedha.
“Ninakusubiri kwa hamu ili nikusikie utakavyokuwa unabadili jahanam kuwa peponi, kwa manufaa ya Watanzania nitaanika hadharani uozo wako wote kwa ujasiri na bila hata chembe ya woga ili Watanzania wasipotoshwe tena kwa njia ya bwembwe za fedha,” alisema.
zitto.jpg

Kiongozi wa ACT- Wazalendo Zitto Kabwe akiwa Singida kwenye mkutano wa kampeni Agosti 7, 2015 alisema ni kazi ngumu kumsafisha Lowassa kutokana na kuwa na kashfa za ufisadi.
Hizi ni baadhi ya kauli za wanasiasa hawa kuhusu Lowassa, swali linabaki kwa sasa baada ya kurejea CCM watakuwa na kipi cha kusema juu ya mwanasiasa huyu?

In God we trust
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hilo ni pigo kubwa sana kwa Nape,polepole na msukuma kasheku walio mtukana mzee wa watu matusi ya nguoni kisa kahamia upinzani
Mtu anaweza akapoteza mda na lengo katika kuchambua sababu zilizomfanya Lowassa arudi nyumbani.

Kuna mambo yanayoweza kutoa mwelekeo wa kuhama huko.

Kwanza kabisa inaonekana palikuwa na ushawishi mkubwa toka CCM mzee huyo ahame. Matakwa haya sababu zake zinaweza zikafikilrika.
Ni ajabu sana timu yote nzima ya uongozi wa juu wa CCM kuweka mapokezi kiasi kile kwa mtu ambaye walishajua wamemmaliza.
Hapa ndipo palipo siri nzito!
Mapokezi yale yanaonyesha dhahiri, kuhama kule hakukuanzia kwa Lowassa. Walimtaka sana ahame; sababu, hatujui!

Sasa ukifikiria, kati ya Lowassa na Nnauye, ni nani mwenye thamani kubwa ndani hicho chama?
Sina hakika sana kama Nnauye angehama na kurudi chamani angepata mapokezi kama aliyopewa Mzee Lowassa.

Kuna jambo wana hofu nalo linalomhusisha Lowassa kuelekea 2020?

In God we trust
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Magu kaamua kunenga makundi hatari ndani ya ccm lkn kuna watu wana chekelea
Kumbuka kauli ya Kikwete kutaka kulivua gamba. Kulivua gamba ilikuwa ni kuwafukuza ccm mafisadi waliokuwa wanakichafua chama wakiwemo Lowassa, Rostam, Chenge na wengineo. Nape hajawahi kutukanwa ndani ya ccm kama alivyotukanwa fisadi lowassa. Unafiki umepitiliza ndani ya ccm vinginevyo huyu mtu aliyetukanwa na hakuna yoyote yule aliyemtetea ndani ya ccm hawakustahili kumpokea.

In God we trust
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hakuna wanao wapaga kura za kuwawezesha kuongoza nchi bali wanaiba na kuwatishia wananchi
Watu tunakosea sana kuwapa watu kama hawa cheo cha "Mwanasiasa". Ni aibu!

Hivi mtu na akili zake timamu anawezaje kuwapa kura watu kama hawa!

In God we trust
 
Nafikiri anatetea vitega uchumi vyake na kukwepa kikombe cha kuingia kwenye ile mahakama mpya iliyo jengwa juzi kwa mbwembwe
Hapana, kama nilivyoeleza hapo juu, ni ziada ya "unafiki". Kunajambo mhimu zaidi linaloweka msukumo Mzee arudi nyumbani. Si jambo la kawaida, kama unafiki. Kuna aina ya hofu.

In God we trust
 
Neno fisadi siyo tusi bali ni sifa lkn ndani ya ccm wapo walio mtukana matusi ya nguoni kabisa
Chadema hawakumtukana lowasa zaidi ya miaka nane walimtaja kuwa ni fisadi papa na kisha wakampokea agombee urais?
Huo unafiki wa chadema huuoni au ndio kujitia upofu Tu kutokana na mahaba ya chama?
Hebu balance unafiki wenu ninyi wanasisa na wapiga debe wa siasa, nyote mko na viwango vya juu Sana vya unafiki bila kumung'unya maneno..
Weka nukuu za wakina lema na msigwa na wengineo waliompaka matope lowasa na kisha ulete walivomsifia akiwa kwao na ulete kauli zao za sasa.
Kuna wakati hao CCM wanaweza kuwa Bora kuliko wapinzani wasiojielewa wanataka nini...labda ni chuki na wivu wakati mwingine zinaendesha hisia zenu kisiasa maana haiingii akilini mtu huyo huyo akiwa kwenu anakuwa msafi akienda upande wa pili anakuwa mchafu sana....hii double standard sijui kama mnaiona na kama si miongoni mwao ulipaswa kuleta uchambuzi wa pande zote zilivoshiriki unafiki dhidi ya lowasa na sio kuona pande moja kwakuwa uko upande huo....wewe pia ni zaidi ya mnafiki tena mnafiki kiwango cha uchawi wa mchana....

Sent using Jamii Forums mobile app

In God we trust
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom