Nape kushtakiwa kwa JK kwa matusi Mwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape kushtakiwa kwa JK kwa matusi Mwanza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Oct 18, 2011.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Viongozi wa CCM mkoani Mwanza wamesikitishwa na lugha ya matusi iliyotumiwa na katibu wa itikadi na uenezi Nape Nnauye alipokuwa anahutubia mkutano wa hadhara juzi jumapili.

  Wamedai kwamba hata vurugu kubwa zilizozushwa na wafuasi wa chadema ni kutokana na kuudhiwa na lugha hiyo ya matusi.Imedaiwa kwamba viongozi hao wanaandaa ujumbe mzito kwenda kwa mwenyekiti wa ccm Rais Kikwete kulalamikia mwenendo wa Nape usioridhisha.

  Wameendelea kulalamika kwamba Wasukuma hawapendi matusi na njia watakayotumia kukiadhibu CCM ni kukinyima kura kwenye uchaguzi mdogo wa kiti cha udiwani unaotarajiwa hivi karibuni hapo Mwanza.

  SOURCE MTANZANIA.  Updates:
  Mhariri wa Tanzania Daima anasemaje kuhusu tukio hili:

  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Upendeleo wa polisi utachafua nchi

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  MWENENDO wa Jeshi la Polisi katika kulinda amani kwenye matukio ya kisiasa nchini unatia shaka na iwapo hatua stahiki zisipochukuliwa basi nchi inaweza kujikuta ikiingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo chanzo chake kitakuwa ni Jeshi la Polisi kukipendelea Chama cha Mapinduzi (CCM) na kukandamiza wafuasi wa vyama vingine.
  Tunasema hivyo tukizingatia tukio baya na la kusikitisha lililotokea majuzi jijini Mwanza la wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupigwa na vijana wa ulinzi wa CCM, baada ya Katibu wao wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, kuwaagiza kufanya hivyo, huku polisi waliokuwepo wakibariki kitendo hicho kwa kutochukua hatua yoyote ya kudhibiti agizo hilo.
  Tunatoa tahadhari hii, tukikumbuka tukio jingine baya na la kusikitisha lililotokea katika uchaguzi mdogo wa Igunga uliomalizika hivi karibuni ambapo wafuasi na viongozi wa CHADEMA walifuatwa kwenye kambi yao na kushambuliwa na vijana wa ulinzi wa CCM, lakini polisi walipotaarifiwa badala ya kuwakamata vijana hao wa CCM wao walikimbilia kuwafukuza wafuasi wa CHADEMA wakitumia mabomu ya machozi.
  Kuhusu tukio la hivi majuzi, agizo la Nape, la kutaka wafuasi wa CHADEMA wapigwe, huku akiwaita ‘Manyani wa CHADEMA" lilitokana na mwanasiasa huyo kuzomewa na sehemu kubwa ya hadhira iliyokuwa ikimsikiliza katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Magomeni, kata ya Kirumba, jijini Mwanza.
  Wananchi wa kata hiyo iliyokuwa ikiongozwa na diwani wa CHADEMA aliyefariki hivi karibuni, walimzomea Nape katika mkutano huo baada ya kukerwa na siasa zisizo za kistarabu za Nape, za kutoa matusi na kejeli chafu dhidi ya viongozi wa chama hicho cha upinzani, huku akimbeza diwani huyo (marehemu) kuwa hakufanya kitu na walikosea kumchagua.
  Ni vema ikazingatiwa kuwa haki ya kushangiliwa ni sawa kabisa na haki ya kuzomewa, kwa hiyo kitendo cha kuzomewa alichofanyiwa Nape na wananchi hao, hakikuwa kosa hasa tukipima uzito wa matusi na kauli alizotoa mbele ya wananchi hao waliofiwa na diwani wao hivi karibuni.
  Na hata kama kuzomewa kungekuwa kosa, bado haikuwa halali kwa Nape kujichukulia sheria mkononi na kuagiza vijana wawapige wale aliowaita ‘Manyani wa CHADEMA" na wala haikuwa halali kwa Jeshi la Polisi kufumbia macho kitendo hicho.
  Hatua ya polisi kutochukua hatua yoyote ya kudhibiti hali hiyo, inatoa picha mbaya na ya waziwazi kuwa jeshi hilo halifanyi kazi ya kulinda usalama wa raia bali linafanya kazi ya kutii maagizo ya viongozi wa CCM pindi kunapojitokeza upinzani wa kisiasa dhidi ya chama hicho.
  Mwenendo huu wa Jeshi la Polisi kuipendelea CCM kwa kila kitu tena hasa inapofanya vitendo vya ukatili dhidi ya wafuasi wa vyama vingine vya siasa, unaashiria hatari kubwa ya kuvunjika kwa amani ya nchi yetu, huko tuendako, maana kwa vyovyote vile hatuamini kama vijana wa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani vitaendelea kuvumilia ukatili huo, huku taasisi ya dola wanayoilipia kodi ilinde usalama wao, ikiwa mstari wa mbele kuwakandamiza.
  Tunalionya Jeshi la Polisi tukilitaka liache mara moja kutumika vibaya kisiasa, kwani uvumilivu wa uonevu, dhuluma na ukatili, una mwisho na mwisho wake huwa mbaya na wenye madhara makubwa kwa watu wote wa taifa zima, bila kujali huyu ni polisi au huyu ni CCM. Aidha, tunawataka askari polisi waache kutii amri katili na haramu kutoka kwa makamanda wao, wajue kuwa ni ujinga na ni dhambi kubwa kutii amri ya kuwapiga na kuwaua Watanzania wenzao, kaka zao, mama zao, wazee wao, eti kwa sababu tu ya kukibeba chama kimoja cha siasa.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. l

  luckman JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Bado!god at work!
   
 3. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,680
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  na leo anatarajiwa kuendeleza matusi yake kwenye kata ya igoma, mwanza! chama kilikaa kikapata bora kiongozi.
   
 4. Ungana

  Ungana JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 358
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bora kiongozi!
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Igoma kuna nini ? Maana CCM kuingia mahali baada ya uchaguzi ni wakati wa kutafuta kura pekee baadaye wanarudi Dar kula kuku .Je kuna nini huko nako ?
   
 6. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Igoma huko ndo ngome ya chadema chini ya naibu meya charles chinchibela sasa sijui atatambia wapi huyo nape yetu macho wana mwanza.
   
 7. M

  Marytina JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Nape ameshaweuka
   
 8. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Akitukana matusi apopolewe mshmba huyu anakiri Mwanza bado mteremko kwa magamba
   
 9. nzitunga

  nzitunga Senior Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mie nawashangaa hao wazee kumshtaki Nepi kwa JK. Matusi ni jadi ya magamba, wao wakiishiwa sera huanza kutukana. Hata Baba January alikuwa hivyo, katukana watu wengi sana. Alitoa matusi ya nguoni kule Tarime mpaka mtu unajiuliza kama waliyemwamini kuwa katibu mkuu wa Taifa (sio wilaya) anatoa matusi ya nguoni basi chama chote kinamuelekeo huo na kinanuka.
  Nawashauri hao wazee, kama matusi ya Nepi yanawakera, basi wajue hiyo ndiyo jadi yao, waamie tu vyama vingine kuliko kudhalilika kila wakati.
   
 10. Adolph

  Adolph JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  safiiiiiiiiii nepi.....poromosha matusi blazaaaaaa watu hawakujui hao....
   
 11. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,680
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  igoma si ya chinchibela ni diwani wa nyakato,
   
 12. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,595
  Likes Received: 4,709
  Trophy Points: 280
  Mtoto wa haramu ni wa haramu tu.
   
 13. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kweli nape ni mlevi..
   
 14. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  kata ya igoma iko chini ya adamu chagulani
   
 15. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  jamani labda mfupa hauna ulimi. Lol
   
 16. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,303
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa anaendele kukishushia hadhi chama chao.
   
 17. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 180
  Hivi alitukanaje tena?
   
 18. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Hajui alifanyalo.
   
 19. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sio mlevi tu, ni mlevi wa mataptap maana walevi wa whisky na bia huwa wanakuaga makini.
   
 20. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  mbona hata mwenyekiti wake nae huwa anaropoka tu
   
Loading...