barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,863
Kijana na Mbunge wa Mtama,Waziri Nnape Nnauye na washirika wako,ina maana gani bunge kuonyeshwa usiku wote huu wakati watu tunatakiwa kulala ili kuwahi kesho kazini?Lengo lenu ni nini hasa na ni kitu gami mnakificha?
Kibaya zaidi ni kuwa mnakata kata sana vipande vya Wapinzani wanapoongea,kama leo ameonekana Mwanasheria mkuu akijibu hoja tu za Wabunge,tena inaonakana ni hoja za wabunge vyama vya upinzani tu.Na wala hatuoni wakati wabunge hao wakiuliza au wakitoa hoja zao,Editing ya Bunge inayoonekana ni ile tu Serikali,Mwanasheria na Baadhi ya Wabunge wa CCM wakijibu tu hoja
Hoja na michango ya wabunge haionekani ila tunaona tu Naibu Waziri Kijazi akijibu hoja za Wabunge bila sisi wananchi kuona hoja za pande zote mbili
Hili la kutuoonyesha bunge "live" haliwajengei sifa nzuri,haya mambo mnaweza kuyaona ni madogo lakini yana nafasi zake,tunamuunga mkono Rais wetu lakini kwanini anatufanyia hivi?Woga wa nini??
Tunajitahidi kurudisha nidhamu na uwajibikaji serikalini,tusiache nyuma demokrasia,Uwazi na utawala bora.Utawala bora na maendeleo huenda pamoja.Nchi inayoendelea bila mfumo wa utawala bora si lolote si chochote.Tunaporudisha misingi ya kufikia maendeleo ya watu wote,basi tuende pamoja na utawala bora
Turudishieni Bunge,acheni bunge tuone yanayojadiliwa...Yanayofichwa yasijulikane siku yakijulikana mtapoteza imani zaidi ya kama yengejulikana kwa uwazi na ukweli
#JPM Bring back Bunge Live Coverage!!