Nape: Kubadili ukomo wa madaraka ni ushetani, unafaa kupingwa kwa nguvu zote na vijana

Mwambieni Nape ccm ilete ile katiba ya Warioba yenye ukomo wa wabunge muone kama atatokwa hilo povu...
 
Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amefunguka na kuwataka vijana wa kiafrika kuamka na kupinga baadhi ya viongozi wanaotamani kubadili ukomo wao kuwa madarakani kwani wasipofanya hivyo tabia hiyo itazoelekea na kuwa ya kawaida.

Nape ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii asubuhi ya leo ukiwa umeambatana na picha iliyokuwa inawaonesha baadhi ya wabunge wa nchi ya Uganda wakiwa Bungeni wakitaka kupigana.

"Huu ulevi wa baadhi ya viongozi wa Afrika kutamani na kubadili ukomo wa wao kuwa madarakani ni ushetani na lazima upingwe kwa nguvu zote hasa na vijana kabla utaratibu huu haujaota mizizi na kusambaa. Hii ni zaidi ya kansa", amesema Nape.

Kauli hiyo ya Nape imekuja baada ya kuonekana kwa baadhi ya viongozi Afrika wakibadili vipengele vichache ndani ya Katiba ya nchi yao ili imuwezeshe kukaa madarakani zaidi ya alivyotakiwa kwa mara ya kwanza kuongoza.

View attachment 705241
Huyu Nape ni sehemu ya haya madhila tunayoyapitia,Arudishe bunge live kwanza
 
Natamani tungebaki na mfumo wetu wa zamani wa jadi wa machifu.. ule ndo tuliouasisi sisi na unafaa kwa mazingira yetu.. wazungu walituvuruga sana na sasa hatujui tufanye nini..
 
Natamani kuwe na ukomo wa mihula pia kwa wabunge na madiwani; pia ukomo wa umri.
Tuone maoni ya hao akina Nape, Mbowe, ....
 
Huko ndiko anakotupeleka Sizonje. Ndiyo maana anatumia nguvu zake zote kuua upinzani ili miaka ya baadaye awageuzie wananchi kibao kwa kuondoa vipengele vya katiba ambavyo vinamzuia kutawala milele na kuviweka vile vitakavyomwezesha kuwa rais wa kudumu asiye na ukomo. Kipindi hicho, bunge litakuwa la maCCM watupu, hivyo hakuna atakayethubutu kumpinga Sizonje. Hapo ndipo tutakapolia kwa machozi ya damu huku tukisaga meno na tayari itakuwa "too late"
 
Ndio maana nikasema nchi nyingi sio nchi zote, pia Rwanda iko stable kwa sababu wananchi wanampenda rais au kwa sababu anayempinga kagame anawekwa ndani?
Rwanda imefanikiwa kuwamaliza wahutu wote maarufu na kuwatia hofu wote ili Kagame akose mpinzani. Huo ndio ushetani.
Ni ustable wa utawala wa shetani.

Haiwezekani Wahutu ndio wengi Rwanda halafu kagame ashinde kwa 97% ni ustable wa kutumia mtutu wa bunduki.
Madaraka ya damu na hofu kwa wengine ndio nguzo kuu ya utawala usio na ukomo. Huo ndio ushetani anaoutaja mh. Np.

Nchi yetu ilikua inakwenda vizuri sana kiuchumi kidemokrasia ,kisiasa ,kijamii, na kidiplomasia na pia mihimili ya dola ilikua inazidi kuimarika. Tulikosa katiba tu yenye kuwawajibisha watawala wanaokiuka sheria wawapo madarakani. Na hili tulikua tumeshaanza kulikamilisha ,jambo ambalo lingeifanya Tanzania kuwa nchi bora kabisa duniani.

Haiwependezi kwa nchi kuwa na watawala wanaotuma vijana kuwatolea wabunge na mawaziri wastaafu bastola hadharani na wakaachwa bila kukemewa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Mungu pekee ndiye mwenye utawala wa milele lakini sio binadamu. Huu ni moja ya kumkosea Mungu na wanadamu wengine wenye ndoto za kutawala.

Nchi yetu imeundwa na makabila 125 + na kila kabila lina koo za kichifu zenye uzao wa kutawala ivyo Tanzania ina koo zaidi ya 125 zenye vijana wenye ndoto ya kuja kutawala siku moja kwa ridhaa ya wananchi. Hivyo ni vyema tukatoa fursa za kukuza demokrasia ili tuwapime kwa hoja na sio kusimika kabila moja madarakani milele na kuua ndoto za wengine kutawala kidemokrasia.
Tanzania ni Taifa kubwa lenye makabila na duni nyingi sio kama Kanchi ka Rwanda kalikojengwa kwa misingi ya mafuvu na damu za bindamu huku wakijali na kutukuza uhai wa ng'ombe na mbuzi wakiua wanadamu wenzao kwa uroho wa madaraka na utawala wa kudumu.

Hatutaki kurudi nyuma badala yake twende tukajifunze huko kwa wenzetu waliofanikiwa kuwa na demokrasia isiyo na vurugu wanavyofanya chaguzi zao.
 
Tangu kunyofolewa, nape kawa kama msemaji msaidizi wa Kambi ya upinzani.
 
Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amefunguka na kuwataka vijana wa kiafrika kuamka na kupinga baadhi ya viongozi wanaotamani kubadili ukomo wao kuwa madarakani kwani wasipofanya hivyo tabia hiyo itazoelekea na kuwa ya kawaida.

Nape ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii asubuhi ya leo ukiwa umeambatana na picha iliyokuwa inawaonesha baadhi ya wabunge wa nchi ya Uganda wakiwa Bungeni wakitaka kupigana.

"Huu ulevi wa baadhi ya viongozi wa Afrika kutamani na kubadili ukomo wa wao kuwa madarakani ni ushetani na lazima upingwe kwa nguvu zote hasa na vijana kabla utaratibu huu haujaota mizizi na kusambaa. Hii ni zaidi ya kansa", amesema Nape.

Kauli hiyo ya Nape imekuja baada ya kuonekana kwa baadhi ya viongozi Afrika wakibadili vipengele vichache ndani ya Katiba ya nchi yao ili imuwezeshe kukaa madarakani zaidi ya alivyotakiwa kwa mara ya kwanza kuongoza.

View attachment 705241
Huyu asipotekwa wiki hii sijui !
 
Rwanda imefanikiwa kuwamaliza wahutu wote maarufu na kuwatia hofu wote ili Kagame akose mpinzani. Huo ndio ushetani.
Ni ustable wa utawala wa shetani.

Haiwezekani Wahutu ndio wengi Rwanda halafu kagame ashinde kwa 97% ni ustable wa kutumia mtutu wa bunduki.
Madaraka ya damu na hofu kwa wengine ndio nguzo kuu ya utawala usio na ukomo. Huo ndio ushetani anaoutaja mh. Np.

Nchi yetu ilikua inakwenda vizuri sana kiuchumi kidemokrasia ,kisiasa ,kijamii, na kidiplomasia na pia mihimili ya dola ilikua inazidi kuimarika. Tulikosa katiba tu yenye kuwawajibisha watawala wanaokiuka sheria wawapo madarakani. Na hili tulikua tumeshaanza kulikamilisha ,jambo ambalo lingeifanya Tanzania kuwa nchi bora kabisa duniani.

Haiwependezi kwa nchi kuwa na watawala wanaotuma vijana kuwatolea wabunge na mawaziri wastaafu bastola hadharani na wakaachwa bila kukemewa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Mungu pekee ndiye mwenye utawala wa milele lakini sio binadamu. Huu ni moja ya kumkosea Mungu na wanadamu wengine wenye ndoto za kutawala.

Nchi yetu imeundwa na makabila 125 + na kila kabila lina koo za kichifu zenye uzao wa kutawala ivyo Tanzania ina koo zaidi ya 125 zenye vijana wenye ndoto ya kuja kutawala siku moja kwa ridhaa ya wananchi. Hivyo ni vyema tukatoa fursa za kukuza demokrasia ili tuwapime kwa hoja na sio kusimika kabila moja madarakani milele na kuua ndoto za wengine kutawala kidemokrasia.
Tanzania ni Taifa kubwa lenye makabila na duni nyingi sio kama Kanchi ka Rwanda kalikojengwa kwa misingi ya mafuvu na damu za bindamu huku wakijali na kutukuza uhai wa ng'ombe na mbuzi wakiua wanadamu wenzao kwa uroho wa madaraka na utawala wa kudumu.

Hatutaki kurudi nyuma badala yake twende tukajifunze huko kwa wenzetu waliofanikiwa kuwa na demokrasia isiyo na vurugu wanavyofanya chaguzi zao.
Unataka mtu kama Humphrey Polepole aishije ?
 
Hapo naona umeshamaliza kila kitu, hence thread closed.
 
Back
Top Bottom