Nape: Kinachoendelea ni mateso kwa wakulima wa korosho, hakiwezi kumaliza tatizo

Acha tuisome namba tu, nahisi na bado tena naombea waendelee hivihivi na ilifika uchaguz mwingne waichague kwa kishindo ili tuisome vizur kbs. Wakiweza waiongeze mashairi kweny wimbo wao ule, hii nchi ni ya watu wachache watakavyoamua tunafuata.
 
Nape ni mnafiki yeye na baba yake Membe ndiyo wafanyabiashara wa kangomba. Yeye aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya masas mkoani mtwara na wakati huo serikali iliweka dhamana kwa vyama vya msingi kukopa bank kwa ajili ya kuwalipa wakulima malipo ya awali.sasa atupe changamoto zilizojitokeza wakati huo ili atuambie hoja yake hiyo ambayo kimsingi siyo mpya na namna ya kuitekeleza.mimi nasema suluhisho la kangomba Zitto kabwe Nape na mzee wako membe waache kununua korosho za kangomba ili mkulima auze mwenyewe ghalani na apate bei nzuri.waache tamaa
 
Dawa ya Kangomba ni kubadili mfumo wa malipo ya Korosho kwa wakulima, kwa kuviwezesha Vyama vya Ushirika kupitia TADB kulipa sehemu ya malipo Mara tu korosho inapofika ghalani. Hichi kinachoendelea sasa hakiwezi kumaliza kangomba, ni mateso tu kwa wakulima! Nape Moses Nnauye on Twitter

View attachment 964028
Kuna aina tatu za vitenzi
1.kitenzi kikuu
2. " kisaidizi
3. " kishirikishi
Sasa tangu 2015 CCM wametuletea kitenzi KIKURUPUSHI
"Ukiona choo ndotoni usikitumie"
IMG_20181230_130606_641.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye sakata la korosho wengi hapo hawatetei wakulima kama wanavyojinasibu bali wanatetea maslahi yao. Zitto ameacha kutetea wakulima wa mawese kule Kigoma anakuja kutetea miche yake 400 ya mikorosho mtwara na kudai anatetea wakulima. Nape wewe tunajua yule jamaa mwenye kiwanda chake mbagala ambaye kwa sasa amekifunga aliyekuwa anakupa posho kwa ajili ya kumtetea na kujidai unatetea wakulima huku ukijua kwamba anawakandamiza wakulima.
 
Kasema ukweli mchungu ila ataambiwa katumwa na mabeberu.
Kinachotafutwa ni haki ya mkulima alietaabika shambani siyo middle men wanaokwenda kuwalalia wakulima kwa bei chee halafu wanakuja kuiuzia Serikali au wanatoa korosho msumbiji anakuja kuiuza Tanzania. Ukiona mtu analalamikia mfumo unaotumika ujue anafanya moja kati ya hayo mambo mawili niliyoyataja. Sisi wengine mbona kuchele tu tushaongeza na wake miguu juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
maajabu ya SIASA...
Usishangae Kusini kumuona NAPE ndio shujaaa Wao! Washasahau alivowaapia juu ya bao la Mkono!
 
Back
Top Bottom