Nape kaondoshwa na sekeseke la kuvua " magamba "

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,035
164,307
Ili kuipata CCM mpya ni lazima magamba yapukutishwe.Hii ni dhana iliyoasisiwa na JK na kuratibiwa na Nape, dhana hii bado inaishi.Alichosahau Nape ni kwamba dhana hii inawahusu wanaccm wote na si kikundi cha wachache fulani ndani ya chama.Kupunguza idadi ya wajumbe wa CC na Nec ni sehemu ya kuvua gamba kama ilivyo kwa kuwafukuza wanachama wasaliti.Nyakati hizi haijalishi ni wapi unaisalitia ilani ya chama iwe serikalini au chamani utavuliwa tu.Mwisho niwakumbushe tu wadau kuwa kimtokacho mtu ndio kimtiacho unajisi hivyo hata vyombo vya habari vimekuwa vikijinajisi vyenyewe kwa kuwakumbatia baadhi ya wanasiasa kwa malengo binafsi.Tuwe makini kila mara CCM itakapojitikisa ni lazima magamba yatapukutika na chama kitazidi kuwa kipya.
 
Back
Top Bottom