Nape: Kampuni za simu acheni kutuma ujumbe ambao mteja hajaomba, hii tabia ikome

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Nape.jpg
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ametaka makampuni ya mawasiliano nchini kuacha mara moja tabia ya kuendelea kutuma ujumbe ambao wateja hawajaomba na kueleza kuwa kwa kufanya hivyo ni kuwapotezea muda wateja wao.

Nape ametoa agizo hilo Mei 31, 2022 wakati akipokea taarifa ya maboresho kutoka kwa timu ya mtandao wa Vodacom ambao walizunguka kwa baadhi ya mikoa kufanya uchuguzi wa malalamiko ya wateja ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri huyo kutaka kero za mitandao zitatuliwe haraka.

Amesema kitendo hicho kimekuwa ni kero kwa wananchi kwani kinapoteza muda wa kutafakari jumbe hizo ambazo kuna wakati hazina faida kwa watumiaji husika wa mtandao na kusema kuwa hakipaswi kuendelea kuvumiliwa.

"Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa wananchi ambao wanalalamikia suala la kuendelea kupokea jumbe mbalimbali ambazo hawakuziomba katika huduma na hivyo kugeuka kuwa ni kero badala ya huduma,naomba tuliangalie hili," alisema.

Kutokana na hali hiyo, Waziri huyo wa Mawasiliano aliyataka makampuni yote yakae na watoa huduma kujadiliana kuhusu jambo hilo na kuona namna ya kuondoa tabia hiyo (ujumbe) kwa mtu ambaye hakuomba.

"Naagiza tabia hiyo ikome mara moja huu ni usumbufu kwa wateja, niseme wazi kuwa agizo hili halikulenga Kampuni ya Vodacom pekee bali kwa watoa huduma za mawasiliano wote," alisisitiza.

Mbali na hayo alitoa maelekezo kwa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kusimamia kwa nguvu zote agizo hilo ili kuondoa kero.

Amesema ni wakati kwa TCRA kwa kushirikiana na makampuni ya kutoa huduma waendelea kufanya maboresho hususani katika mfumo wa data na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa uelewa kwenye mitandao.

"Pamoja na changamoto hiyo ya kutumiwa meseji, TCRA wanatakiwa kukaa meza moja na makampuni ili kutafuta njia bora itakayowezesha Watanzania wengi kumiliki simu janja ikibidi hata kwa kukopesha na kulipa kidogo kidogo kwa kuwa Serikali inahitaji watu wengi kutumia mifumo ya data," amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Sitho Mdlalose alisema kampuni yao ilipokea agizo la Waziri na kuamua kuzunguka katika baadhi ya mikoa kutafuta maoni ya wateja wao ambao walibaini kuna mambo mengi yanayofanyika na kuwa kero kwa watumiaji wa mtandao wano.

Ametaja baadhi ya mikoa waliyotembelea katika utafiti wao ni Mbeya, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na Dodoma.

"Tumezunguka mikoani na kukutana na wateja wetu wengi wakilalamika suala la bando kuisha hata kama mteja hakutumia lakini muda ukifika linaondolewa , jambo hili tayari tumelipatia ufumbuzi," amesema Mkurugenzi huyo.


Chanzo: Malunde
 
Kabisa mkuu,kuna kipindi Vodacom walikuwa wananikasirisha sana.

Wanatuma jumbe mara wakukopeshe baada ya dakika tano ujumbe wa huna salio.Hapo akili inawaza utakuwa ujumbe wa maana kwa sababu haiingii akilini itume jumbe kwa intervals za dakika tano tano hadi kero.

Nilikuwa nataka nimpigie mtoa hudumu niwachane makavu .

#Maoni yangu.
 
Ngoja tufike 2025 wakati wa kampeni

20220522_215052-jpg.2247879
 

Attachments

  • 20220522_215052.jpg
    20220522_215052.jpg
    78.7 KB · Views: 100
Kabisa Ukikaa kidogo unaona meseji imeingia ukisoma Sasa ndio mambo ya kubet na sijui simulizi mara huna salio mara saizi yako mara umeshinda sijui nini nini inshort inakera mpaka tumekosa imani ya kusoma ata text muhimu ikiingia tu unajua mambo ya saizi yko kumbe text baba mkwe 😄
 
...Voda Wamezidi! Kila siku Asubuhi ninaamshwa na Meseji Yao ya 'Leo hujashinda Nini Sijui'....Wakati Sijacheza Mchezo Wao Wowote....!! Wanaudhi!
 
Sijui kama elekezo hili linagusia na matangazo ya miito wakati wa kupiga simu...Hilo ndio linakera zaidi maana badala wakuunganishe na mtu unayempigia wanakuwekea kwanza tangazo hadi liishe ndio wanaunganisha...Hii ni kero kubwa mnoooo. napongeza jitihada hizo za waziri
 
Sijui kama elekezo hili linagusia na matangazo ya miito wakati wa kupiga simu...Hilo ndio linakera zaidi maana badala wakuunganishe na mtu unayempigia wanakuwekea kwanza tangazo hadi liishe ndio wanaunganisha...Hii ni kero kubwa mnoooo. napongeza jitihada hizo za waziri
Airtel sasa ndio wananza hotuba kabisaaaa hawajui wakati mwingine simu ni ya dharura
Well done nape
 
Nape akasome Consumer's regulation ya TCRA ambayo inamruhusu Mtoa huduma (Tigo, Zantel, Airtel, Vodacom na wengine) kutuma promotional messages/contents I think ni Moja Hadi tatu kwa siku. Asikurupuke nashangaa na TCRA nao na Vodacom wameitikia tu kama mbuzi vile.

Sheria mnatunga wenyewe then mnakuja kutukera huku, niliwahi kuwashtaki Tigo kwa TCRA na nikashinda "kidogo" ila baada ya kusoma hizo sijui consumer upumbavu Gani nikaona Tanza-nia tuna safari ndefu
 
mumeshindwa kushugulikia swala la vifurushi kubadilishwa mnatuletea unafk 😏
Kero ya SMS ni kubwa mno.
Bei ya vifurushi vya kuperuzi mitandao ni kubwa sana na bei hizi kubwa zimeanza kabla ya vita vya Ukraine. Sasa sijui tatizo nini?
 
Back
Top Bottom