Nape kabala ya kutafuta mafisadi chadema malizana na wa ccm kwanza. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape kabala ya kutafuta mafisadi chadema malizana na wa ccm kwanza.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Japhari Shabani (RIP), May 13, 2011.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nape Mnauye ni mategemeo yangu ya kwamba sababu kubwa ya kuteuliwa kwako na viongozi wapya katika kamati kuu ni uamuzi uliofikiwa na CCM baada ya kubaini mapungufu katika chama na moja kati ya hayo ni UFISADIni mategemeo yangu-Natamani niamini hivyo-Walitegemea wewe na viongozi hao(kama walikua na nia nzuri)Uwasaidie kupambana na MAFISADI ndani ya chama kama mlivyolibatiza zoezi hilo "KUJIVUA MAGAMBA"Ni mwezi wapili tangu kuchaguliwa kwenu hatujaona matunda yoyote mbali na ngonjera na usanii katika majukwaa.Kabla ya kuwashughulikia mafisadi waliomo katika chama CCM ambao tayari wanafahamika ambapo ndiyo sababu kuu ya kuchaguliwa kwenu mnaanza kutafuta mafisadi CHADEMA.Kama ningelikua wewe ningelianzia pale ulipoishia baada ya kufukuzwa umoja wa vijana CCM baada ya kuibua UFISADI sakata la miradi ya majengo ya umoja wa vijana na baadae mafisadi wengine.Kwa hali ilivyo hivi inadhihirisha ya kua kelele zako wakati ule zilikua vita ya kugombea madaraka umeyapata sasa usanii na ngojera.TUNATAKA VITENDO KILA KITU KIKOWAZI!
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  alienda chadema akatoa sharti la kugombea ubunge akanyimwa.huyu dogo ni mroho wa madaraka hana lolote.
  leo amepa alichokitaka anaanza kuchonga,oo mafisadi chadema wakati anapokea mishahara miwili.
  fisadi namba moja.
   
 3. K

  Kaseko Senior Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  anatafuta utajir kupitia domo lake hana dhamira ya kweli.
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mfa maji aachi kutapa; Nape ni dhahiri amejipalia mkaa, katika kikao cha NEC kijacho uenda akawekwa kiti moto na kuhenguliwa kwenye ukatibu kwa madai ya kupotosha maazimio ya NEC. Hivi sasa anahahakutafuta njia ya kujinasua kabla bomu haijamlipukia. Mkama tayari amekwisha jitenga kado. Chiligati kwa upande wake naye tayari amekwisha badilisha mwelekeo. Hivi sasa anasema CCM itashughulikia suala la ufisadi katika uchaguzi mkuu ujao. Sijui hayo yameamuliwa na kikao gani!
   
 5. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Usisikilize habari ya upande mmoja tu...

  ..........Kuhusu suala la kuhamia katika chama hicho, Nape alisema: "Tena uandike kabisa, mimi ndiyo ninao ushahidi wa wao kunitaka nikagombee kupitia chama chao nikakataa, kwa sababu siwezi kuhamia chadema, kile ni chama cha ukoo," alisema Nape.
   
 6. s

  smz JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama kweli Nape ana ubavu wa kupinga ufisadi, safari yake iende hadi Shinyanga na Mwanza. Na akifika Shy asisahau kwenda Bariadi kwa mzee wa Vijisenti, akaseme hayo ya kuwavua gamba wenzake akiwemo AC. hapo ndo tutajua kweli anatekeleza yaliyoamriwa na chama chake.

  Vinginevyo nawaambia huyu dogo hana lolote. Ameanza kusema haya mambo yatajadiliwa kwenye nec ijayo. Mara chiligati anasema mamabo haya yata angaliwa kwenye uchaguzi wa CCM unaokuja mwakani. Hawa watu wanawafanya WaTZ wavivu wa kufikiri kama wao. Wamesahau kule Iringa walivyosema, na hasa Chiligati, labda tumkumbushe: "Ndani ya siku 90 kama hawatajitoa wenyewe tutawataja hadharani na tutawatoa kwenye chama chetu". Aseme kama amesahau, sisi bado tunasubiri siku 90 zikifika tuone kweli sekretariati ina meno. Siyo kutuchezea akili yetu.

  Tekelezeni kwanza ahadi yenu ya siku 90 acheni blaa blaa
   
 7. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Amepigwa Mkwara akashika Breki za Mbuzi za kusotea miguu ya nyuma. Ufisadi wa RACHEL unacheza nao! Alijifanya siku 90 Sasa anataka kutufanya tumeshasahau? Sisi tunangoja hizo siku 90 zifike ndo tutajua kweli anayoyasema Nape na tutamkubali kuanzia hapo, vinginevyo aende tu akaendelee kuwaramba miguu Mapacha watatu kama Mabosi wake wanavyofanya.

  Wewe Mtoto mdogo unajifanya Utawaondoa akina Mzee Chenge kwenye Chama chao! Wewe, Chiligati, Mkama pamoja na Baba yenu JK hamna ubavu wa kuwaondoa hao.
   
Loading...