NAPE ivi inakuaje uzungumzie posho na madokta wakti chama chako ndo serikali?

Chama kinadhamana ndio chenye kutawala serikali kweli, lakini nape hayupo katika huo uongozi wa kiserikali yeye si mmbunge aseme kupeleka hoja bungeni, yeye afanyi kazi ktk wizara ya serikali na wala yeye ausiku wala hana influence katika maamuzi ya serikali. Yupo kwenye chama lakini si upande wa serikali sijui umenielewa kwa maana hiyo kuwasii wale wahusika sii kosa. Vingenevyo na yeye angekuwa direct vocally kama wengine wanao chukizwa na uozo kama vijana wengine waliopo mjengoni wa vyama vyote apparently.

rejea kazi na wajibu wa CC ya CCM
 
Ninachokiona hapa ni siasa za makundi ndani ya CCM.Kuna kundi lililojipambanua ni wapambanaji dhidi ya ufisadi na linaona mwelekeo ndani ya chama ndivyo sivyo.Waliokuwa na tuhuma za ufisadi wanaendelea kupata nguvu ndani ya chama kwa hiyo turufu pekee iliyobaki ni kwa kundi lililo kinyume na watuhumiwa wa ufisadi kujisogeza karibu na wananchi na hata upinzani ili kuzua hisia kwamba kundi linalopambana dhidi ya ufisadi lina sapoti kubwa kwa wananchi na endapo watuhumiwa wa ufisadi watapitishwa ndani ya chama kama wagombea 2015 basi kuna uwezekano kundi lililojipambanua kuwa kinyume na ufisadi linaweza kujiondo hivyo CCM ikakosa ushindi.

Hoja ya Nape ni nzuri na ndivyo inavyotakiwa lakini ni kwa nini Nape na chama chake wasiitishe party caucas kuongelea suala la posho kama ambavyo wamekuwa wakifanya kupitisha maazimio ya pamoja chini ya msimamizi wa shughuli za serikali bungeni yaani Waziri Mkuu? Kama wana nia ya dhati na wana uchungu kweli basi watumie nguvu ya chama katika maamuzi au ajenda zenye maslahi kwa chama through mhimili mwingine wa dola yaani bunge.

Wabunge wa CCM wakikataa hiyo nyongeza,na pia upinzani hasa chadema(ofcourse msimamo wa chama unapinga ongezeko la posho) wakikataa nyongeza ya posho,je hawa wabunge wachache waliobakia wataweza kuleta influence na ku-demand nyongeza?

Tukubaliane kwamba hapa kuna

1.Ajenda ya makundi ndani ya CCM kama nilivyoeleza paragraph ya kwanza

2. Unafiki wa CCM katika kuogopa upinzani dhidi ya serikali kutoka kwa wabunge unaohatarisha kuanguka kwa serikali na hata Rais kuja kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nae in future kutokana na mambo mengi yaliyo mbele yetu na tata kama RICHMOND,MEREMETA nk.
 
Nape ni katibu wa uenezi na itikadi wa Chama Cha Mapinduzi, si mtumishi wa serikali na kwa kuwa CCM ndicho chama tawala ni muhimu kuhakikisha serikali yake inatekeleza ilani ya uchaguzi kama ilivyotolewa wakati wakiomba ridha ya kutawala. Ukielewa haya hutahoji tena... kama hutaki basi!

Acha kupotosha watu wewe! Hivi unafahamu maana ya PARTY CAUCUS? Tunajua umekuwa ni utaratibu wa CCM kuwaita wabunge wake wote kama kamati ya chama ili kuweka msimamo kwenye jambo lolote lile linalopelekwa bungeni.

Kama kweli CCM walikuwa hawaitaki hiyo sitting allowance wangewaita wabunge wake wote kama kamati ya chama na kuweka msimamo wa kuipinga.

Lakini tunafahamu kufuta posho ya makalio sio sera ya CCM bali ya CDM (refer hotuba ya bajeti ya serikali vs Kambi ya upinzani).

Nape kujidai eti leo CCM inapinga ongezeko la posho ya makalio kwa wabunge ni kucheza na akili za Watanzania, wakati anafahamu fika CCM ndiyo champion wa posho za makalio.

Wenye akili ndogo kama wewe ndiyo mnaweza kuwa carried out with that hypocrisy.

Fumbo mfumbie mjinga mwerevu huling'amua. I'm afraid to say that wewe ni mmojawapo katia ya w.a.j.i.n.ga waliofumbia fumbo!

Alamsiki
 
NAPE ATOA TAMKO LA CCM MGOMO WA MADAKTARI,POSHO ZA WABUNGE





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.


Kwa muda sasa nchi yetu imepitia kwenye tatizo kubwa la mgomo wa madaktari katika hospitali nyingi hasa za umma ambao kwa kiasi kikubwa mgomo huo umekuwa na madhara makubwa kwa watanzania masikini ambao ni wengi, kiasi cha kugharimu hata maisha yao.


Chama Cha Mapinduzi kinachukua nafasi hii kuwapa pole sana wale wote walioathiriwa kwa namna moja ama nyingine na mgomo huu. Na kwakweli tunasikitishwa sana na hali inayoendelea!


Chama Cha Mapinduzi kinawapongeza na kuwashukuru madakitari walioonyesha ubinadamu na uzalendo kwa kuamua kurudi kazini na ambao hawakugoma kabisa. Tunawashukuru na kuwapongeza kwani hakuna masilahi yanayovuka thamani ya uhai wa binadamu mwenzako!


Tunachukua fursa hii pia kuwashukuru sana na kuwapongeza askari wetu wa jeshi la wananchi wa Tanzania kwa uamuzi wao wa kizalendo wa kuamua kuitikia wito wa serikali kwenda kwenye baadhi ya hospitali kusadia kuwatibu watanzania wenzao. Moyo huu ni wa kizalendo na wa mfano. Tunajivunia uzalendo wa jeshi letu!


Tunachukua nafasi hii kuwaomba madaktari wanaoendelea na mgomo kurudi kazini huku wakiendelea na mazungumzo na serikali. Tunaamini madai yao yanawezekana kushughulikiwa ikiwa pande zote mbili zitaamua kukaa chini kwa dhati na kuzungumza.


Serikali kwa upande mmoja watafute kwa makini chanzo cha mgogoro huu na kutafuta majibu, na madakitari nao kwa upande wa pili, wawe tayari kukaa mezani na kuzungumza. Tunasisitiza thamani ya maisha ya binadamu ni kubwa kuliko masilahi na madai wanayoyaomba!


Serikali ni vizuri ikajenga utamaduni wa kushughulikia matatizo haya ambayo yanaathiri wananchi wengi kwa uharaka na udharura unaostahili badala ya kusubiri hali inapokuwa mbaya zaidi.


POSHO ZA WABUNGE
Kwa upande mwingine Chama Cha Mapinduzi kinapenda kurudia wito kilioutoa juu ya swala la posho za wabunge. CCM iliwaomba na kuwasihi wabunge na mamlaka zinazohusika na mchakato wa swala hili kuliangalia upya na kutumia busara, ikiwezekana kuachana nalo kwasasa.


CCM inaupongeza na kuunga mkono msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kama ulivyonukuliwa na taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari, kuwa ni vizuri wabunge wakalitafakari upya swala hili kwa masilahi mapana ya wale waliowapa dhamana ya kuwawakilisha bungeni.


CCM inaendelea kuwasihi waheshimiwa wabunge walitafakari upya swala hili na busara itumike katika kuliamua huku wakifungua masikio kusikiliza sauti za Watanzania kwani huko bungeni wana wawakilisha hawa Watanzania, ni vizuri kusikiliza hiki kilio chao! Si busara kupuuza kilio cha waliokupa dhamana ya kuwawakilisha.


Msimamo wa Rais Kikwete kama sehemu moja ya mamlaka inayohusika na mchakato huo ni uthibitisho wa usikivu wake kwa wananchi anaowaoongoza, yeye katimiza wajibu wake, tunawasihi waheshimiwa wabunge wetu nao walitafakari hili na kuona busara ya kuachana nalo kwasasa.


Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM
Itikadi na Uenezi
 
But he's human,can express personal views! Which is positive,je kum-encorage kurecognize ukweli ni vibaya?
 
Amezungumza kama katibu mwenezi kwa hiyo ametoa msimamo wa chama siyo wake.

Sidhani kama amekizungumzia chama, huwa wanaangalia upepo hao. Akichemka utasikia si ya chama ni mtazamo wake binafsi, hukumbuki ishu ya magamba kupewa miezi mitatu. Mbon katibu mkuu alimruka kuwa chama hakijaamua hivyo! Na ni kweli leo miezi mingapi imepita na ishu iko kimya na wala Nape mwenyewe yuko kimya, magamba yanasonga mbele!
 
NAPE ATOA TAMKO LA CCM MGOMO WA MADAKTARI,POSHO ZA WABUNGE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
...
POSHO ZA WABUNGE
Kwa upande mwingine Chama Cha Mapinduzi kinapenda kurudia wito kilioutoa juu ya swala la posho za wabunge. CCM iliwaomba na kuwasihi wabunge na mamlaka zinazohusika na mchakato wa swala hili kuliangalia upya na kutumia busara, ikiwezekana kuachana nalo kwasasa.


CCM inaupongeza na kuunga mkono msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kama ulivyonukuliwa na taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari, kuwa ni vizuri wabunge wakalitafakari upya swala hili kwa masilahi mapana ya wale waliowapa dhamana ya kuwawakilisha bungeni.

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM
Itikadi na Uenezi

Hao wabunge wa ccm ndo waliolikomalia suala hili hadi likafika hapo lilipo. Nashangaa Nape kuwasihi, Why? Unakumbuka Mwalimu Nyerere alipofuta hoja ya Muungano wakati wa Mwinyi, Malecela na Kolimba? Alisema wale ni wabunge wa chama, na chama hakikuwatuma kufanya yale waliyokuwa wakiyafanya. Vipi leo mnawasihi badala ya chama kuagiza waache? Acheni kutudanganya bana! Au ndo mlivyowatuma ila hapa mnatuvunga tu wananchi?

Haya, hata kama mmeshindwa kuwadhibiti wabunge wenu walio wengi humo bungeni ambamo kila walitakalo ni rahisi kwao kulipitisha kwa mtaji wa idadi waliyonayo. Kwa nini rais asisubiri kulitumia rungu lake la kuto-sign hilo pendekezo la kuongeza hizo posho? Its OK raisi kasema watumie busara kuamua, basi busara ya wabunge wenu ndo hiyo wameitumia, sasa kelele za nini? Angalieni chama kinajikaanga kwa mafuta yake. Nawe Nape, hivi ndo tuseme bado u mtoto? Hapa nishapato moto mie Nimie!
 
Back
Top Bottom