Nape: Ikishindikana kukisafisha Chama NIKO TAYARI KUFUKUZWA KWENYE CHAMA KWA HILI

Acha unafiki wewe hata umri wa unafiki hujaufikia kama kweli una unaamini unachosimamia si ujiuzuru tu kwa nini unasubiri hadi ufukuzwe??!!! Kwa mantiki hiyo basi na the so called mafisadi wanasubiri muwafukuze harafu ndiyo mtajua kama kweli kitunguu kina gamba.
 
Nape, huwezi kufunga injini ya Toyota Prado kwenye Ford Mondeo. Chama unachokitumikia na wewe mwenyewe ni tofauti kubwa sana, sijui unafanya nini CCM. Kwa kukuangalia tu naona huna raha ndani ya CCM pamoja na madaraka makubwa uliyopewa, kwanini uipe shida nafsi yako?, toka ndani ya CCM na timiza kile ambacho nafsi yako inakutuma. Ulipotaka kuanzisha CCJ ambayo kwa kweli ilikuwa tishio kubwa na huenda ingeiua kabisa CCM na Watanzania wengi wangepata matumaini makubwa, wajanja wa CCM wakaamua kukupa hicho cheo ili kukupoza na kuiua CCJ, na usipokuwa makini watakumaliza kisiasa muda si mrefu.
 
Back
Top Bottom