Nape iangalie kesho zaidi usiyoijua kuliko leo. Badilika na usonge mbele

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
2,370
3,148
Ninampongeza Nape Moses Nnauye kwa kurejeshwa kua waziri katika wizara yake ya habari
Wakati Nape alipokua waziri wa habari ndio kipindi ambacho Uhuru wa vyombo vya habari uliminywa,zilipitishwa sheria ambazo hazikua rafiki kwa wadau wa habari,vilifungiwa vyombo vya habari kama redio na magazeti.

Haikutosha hata Bunge Live lilipigwa pini kwasababu eti watanzania wasiangalie kwa kua huo ni muda wa kazi.

Pamoja na hayo yote Nape ana tatizo la kufanya propaganda zaidi kuliko uhalisia. Haitazami zaidi kesho.

Nakumbuka alitumia maneno makali kumpinga Lowassa wakati wa uchaguzi mkuu. Hakukua na hekima

Nape waige akina Makamba,Ridhiwan,Awesso,Mavunde nk. Siasa za uanaharakati,ubabe,rohombaya nk achana nazo hazina tija. Hata suala la Makonda ulilibeba kama mwanaharakati wala sio kama waziri.

Nape nakutakia utulivu na mafanikio yaliyo mema na ninakuombea Mungu akuongoze

Msaidie mama Samia kuandika historia yake vyema wakati huo nawewe ukiandika yako
 
Back
Top Bottom