PISTO LERO
JF-Expert Member
- Mar 8, 2011
- 2,819
- 1,454
SIKU chache baada ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, kumtaka Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Itikadi na Uenezi ya CCM kuacha kupiga mayowe na badala yake awaeleze wananchi hatua zinazofanywa na serikali yao kuondoa umaskini, ni dhahiri sasa kada huyo ameanza kuweweseka kisiasa.
Nape ambaye aliibua mjadala ambao hata hivyo alishindwa kuuthibitisha kuhusu madai kuwa Dk. Slaa anamiliki kadi ya CCM na anaendelea kuilipia ada ya uanachama, ameamua kuhamishia siasa za uzushi na matusi kwenye mtandao wa kijamii.
Katika maoni yake aliyoandika kwenye ukurasa wa mtandnao wa Jamii Forum, Nape ameendelea kuupotosha umma kwa kuwaponda waliomtetea Dk. Slaa katika uzushi huo na kuzua uongo mwingine kuwa gazeti la Tanzania Daima linamilikiwa na operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) inayoendeshwa na CHADEMA.
Nazitambua juhudi za wafuasi wa babu (akimaanisha Dk. Slaa) na mashabiki wake katika kujaribu kumtetea ionekane ni jambo la kawaida sana kwake kuwa na kadi ya CCM mpaka leo.
Juhudi za kutumia social media na magazeti mengine hasa gazeti la M4C (TanzaniaDaima) kujaribu kumtetea Dk. Slaa na wakati huo kunikejeli na kunitukana japo kuwa kwa matusi ambayo lazima nikiri si mapya, aliongopa Nape.
Katika utetezi wake huo, Nape anajikologa akisema katika matamshi yake hakuna mahali alipohusisha kuwa na kadi na uanachama wa mtu.....hivyo wanaojaribu kubwabwaja kuwa sijui katiba ya CCM, wanakurupuka kwa sababu ndogo sana.
Kukaririshwa lazima kumtukana Nape hata bila kupima kwa makini hoja....nilichosema Dk. Slaa na baadhi ya vigogo wa CHADEMA wana kadi za CCM na baadhi yao wanazilipia mpaka leo, alisema.
Aliongeza kuwa hajazungumzia uanachama wao, kwamba anajua kuwa kwa katiba ya CCM ukishakuwa mwanachama wa chama kingine uanachama wako CCM unakufa hapohapo.
Ni kweli kuwa hakuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya kuwa na kadi ya CCM kwa Dk. Slaa na maendeleo ya wananchi maskini, lakini Dk. Salaa anatafuta kuwa kiongozi wa nchi anapaswa kuishi yale anayoyasema na kuwa mwaminifu kwa nafsi yake mwenyewe, alijitetea.