Nape Hujui hali Ngumu ya Vijana, Nyamaza Basi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape Hujui hali Ngumu ya Vijana, Nyamaza Basi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ukombozi Sasa, Mar 25, 2012.

 1. U

  Ukombozi Sasa Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  View attachment 50108
  Nape akiongea na waandishi wa habari kuhusu itikadi za CCJ

  Moja, sikufahamu kumbe NAPE alikuwa Msemaji wa CCJ. Hii ni tabia ya kukimbilia madaraka na ajira ya huhakika wala si kwa kuwa anachukia anayo mapenzi ya nchi yake..Ukimwona mtu mwenye tamaa hizi za madaraka muogope sana, alipopewa V8 na CCM akatulia kimya. Sasa amebaki na sera za kujivua gamba ambazo ni unafiki mtupu na zimepoteza umaarufu kwa watanzania, nani CCM ni msafi. Na pia tukubali huyu NAPEY anachuki binafsi na EL na wala si lingine...kila Lowasa akisema hakosi hila, kama waswahili wanavyosema hasidi hakosi hila. Kama vile ni katibu wa itikadai kwa CCM anapaswa kuelezea jinsi gani CCM italeta maendeleo kwa wananchi hususani Elimu Bora, Makazi Bora, Ajira, Usalama wa Raia, Huduma Bora za Afya, na mengineyo na si kukurupuka rupuka na kusema tatizo la ajira ni dogo hapa nchini.. Lowasa aliongea vema kuhusu tatizo la ajira, hapa mzee huyu hakutenda baya hata kidogo..

  Juzi nimesoma gazeti kuhusu NAPE kupinga kauli ya EL kwamba hakuna tatizo la ajira kwa vijana na eti EL angetoa data kusema hivyo, kwa hili unahitaji prove gani kama si uwendawazimu- kweli ufikiri wake ni wa kutosha. Hebu aangalie vijana wanaomaliza vyuo ambao hawana kazi, hebu hajaribu kufanya utafiti binafsi halafu useme ajira zipo. Tumedoda mtaani hatuna kazi hata kama unayo elimu ya chuo kikuu hamna kazi! Nape ni kheri angenyamaza kwenye hili....kuropoka ropoka saa nyingine hakufai- si kila analosema au kufanya Lowasa ni baya.. Mimi si CCM lakini kuhusu usemaji wa EL kuhusu ajira namuunga mkono 100%
   
 2. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapo umenena,Please please Nape Magamba acha kutuhadaa wananchi!.Ujue kuwa hatuna ajira,na ukae ukijua kuwa kwa hali hii ya vijana kukosa ajira nchi inaelekea kwenye vita na machafuko,na mtaji wenu magamba haupo kwa vijana hadi sasa uko kwa wazee ambao ni wachache kuliko sisi vijana na tena 2015 jiandaeni kuimbia nchi kwa maana siyo ya kwenu tena na lazima tuwape mvua za kutosha!.What we need in this rich and blessed nation is employment na siyo poroja na kuropoka kisiasa,Nape kwa leo ni hayo tu.
   
 3. L

  LULENGO Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilitegemea Nepi angefika hata hapa Mwanza kirumba kumbe mavi kwenye chupi hayashikiki hana jipa aje ajionee tena hapa mjini peoples power wanavyoangamiza ili aamini kabisa.
   
 4. M

  Matunyengule JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 701
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Nape ni limbukeni wa madaraka. Awaulize waliomtangulia kwenye hiyo nafasi kina Tambwe Hizza, Chiligati na wengine kama wanasikika. CCM kimechanganyikiwa kila mmoja na kauli yake.
   
 5. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa Nchi yetu unataka yasemwe. (Ukurasa 61)

  Mwalimu hakuishia hapo, bali aliongezea namna hii:

  Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata Chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha Chama cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona Chama makini cha upinzani; na wala dalili zo zote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini hili si jambo la kutarajia bila hofu na wasi wasi! (Ukurasa 66) haya silo mane no yangu ni ya mwenye nayo CCM, sasa NAPE WEWE HUJITAMBUI TUUU??:mullet::mullet:
   
 6. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #6

Loading...