Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,506
Mbunge wa Mtama kwa tiketi ya (CCM) Nape Nnauye amefunguka na kusema kuwa hivi sasa kwenye sekta ya mifugo hali imekuwa mbaya zaidi ukilinganisha na kipindi cha nyuma na kudai kuwa alitegemea mabadiliko makubwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2015.
Nape Nnauye amesema hayo bungeni wakati akichangia hoja ya taarifa ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyowasilishwa bungeni, mjini Dodoma ambapo Nape Nnauye amesema kitendo cha kufunikwa funikwa matatizo ya sekta hiyo ni kutoa kafala kwa wananchi zaidi ya asilimia 50 ambao wanategemea sekta ya mifugo.
"Kwa takwimu sekta hii ya mifugo inasemekana inahudumia kaya zaidi ya milioni nne ambazo zinajumlisha watu zaidi ya milioni 25 ambao ni zaidi ya asilimia 50% ya idadi ya watu wa nchi yetu lakini kwa takwimu hizo hizo sekta hii ya mifugo inachangia zaidi ya asilimia nne kwenye pato la taifa ambalo linashindana karibia sawa na madini katika nchi yetu. Lakini hali inayoendelea kwenye sekta hii ya mifugo ni mbaya sana na kwa bahati mbaya kwa miaka sasa limekuwa linakuja na kuzungumzwa hapa bungeni moto unawaka halafu zinakuchukuliwa hatua za kufunika ule moto watu wananyamaza halafu dhuruma na hujuma zinaendelea pale pale"
Nape Nnauye aliendelea kusema kuwa
"Mwaka 2013/15 moja ya kazi nilizofanya ni pamoja na kupita kwa wafugaji nchi nzima kuwasikiliza na kusikia manung'uniko yao na mimi nikategemea baada ya uchaguzi wa 2015 hali itabadilika bahati mbaya sana juzi mimi nikiwa Mjumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii tumekutana na wafugaji walikuja hapa Dodoma hali ni mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa mwanzo na kama tutaendelea na hatua hizi za kuzima moto kila unapowaka maana yake ni moja tunatoa kafala asilimia 50% ya population ya nchi yetu ambayo inahudumiwa na sekta ya mifugo na kuwaacha hali yao ikiwa mbaya sana" alisisitiza Nape Nnauye.
Muungwana