Nape hana kumbukumbu nzuri kwa kile anachosema

mwinukai

JF-Expert Member
May 3, 2011
1,447
630
Hivi juzijuzi Nape alisikika akitaka CHADEMA kiombe radhi kwa matamshi aliyotoa Mbunge wa Arumeru Mashariki kwa kauli inayofikiriwa au tafsiriwa ni maneno ya ubaguzi.

Huku akisahau kuwa naye amewahi kutoa kauli za kibaguzi za ukabila pale aliposema " mimi si mchaga mpaka nifikirie kujiunga Chadema" maneno haya aliyasema baada ya kuwapo tuhuma kuwa alitaka kugombea kupitia CHADEMA katika jimbo la Ubungo baada ya kutemwa nadani ya CCM katika kura za maoni.

Na wala hajaomba radhi mpaka leo, kwa kinywa chake aliyazungumza haya leo kinywa hikihiki kinazungumza umuhimu wa radhi ili hali NAPE mwenyewe hakuomba msamaha. Bila shaka Nape anachukulia hili kinafiki na kisiasa uchwara kama ilivyodaiwa kuzifanya na Rostam Aziz.
 
Nape keshatolewa posa ndo maana hakumbuki kama alitaka kugombea ubunge jimbo la Ubungo na kuzidiwa sifa na J.J.Mnyika.........Kaliwaaaaaaaaa!!!!!!
 
alichosema nassari kina mantiki hii nchi bora kila mkoa ujitawale,kwani kuna faida gani sasa hivi?
 
Wanaopinga utawala wa majimbo ni watawala walafi ambao kwao wanakotoka hakuna rasilimali za kuiba hivyo wanalilia utawala wa jumla ili waibe madini, mazao yauzwe kwenye vyama vya msingi ili watumie bodi za mazao kuuza nje wale dola(USD) na vyama vya msingi vibaki vinadaiwa na mabenki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom