Nape hajui Augustino Mrema ni wa chama gani, CCM au TLP | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape hajui Augustino Mrema ni wa chama gani, CCM au TLP

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Technician, Jul 25, 2011.

 1. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nape ampiga vijembe Mrema  na Rodrick Mushi, Moshi
  KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ametupa vijembe vingine kwa Mbunge wa Vunjo Augustine Mrema, akisema hatambuliki kuwa ni wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) au ni Chama cha Mapinduzi (CCM).

  Nape alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo lililoko karibu na stendi kuu ya mabasi mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
  “Licha ya upinzani kujigamba kuwa wana nguvu ya umma…lakini tukiangalia bado tunaongoza kwa kila kitu, mkoa wa Kilimanjaro tuna wabunge watano wa CCM na watatu wa CHADEMA lakini huyo mmoja wa TLP yeye hajulikani wa CCM au TLP,” alikejeli Nape.
  Akijibu tuhuma hizo Mrema alisema hiyo ni mipango michafu ya kumchafua na kumtaka Nape kutolea ufafanuzi kuhusu kutajwa kwake kuwa mwanzilishi wa Chma cha Jamii (CCJ).
  “Sisi tunajua Nape amekuwa akitajwa kuwa muanzilishi wa CCJ lakini amekuwa akishindwa kukanusha tuhuma hizo…yeye inakuwaje anitaje mimi kama siyo kukashifiana kusingiziana na kunivurugia?” alisema Mrema.
  Mrema alieleza kuwa Nape anataka kumharibia chama chake na lengo la kusema maneno hayo dhidi yake ni hatua ya mikakati mibovu iliyowekwa kwa ajili ya kuhakikisha jimbo la Vunjo linarudi CCM kitu ambacho alisema hakitafanikiwa.
  “Mimi ni mwanachama wa TLP tena mwenyekiti na mbunge; Nape mdomo ni wake wa kusema anayotaka..sasa naona ameamua kulipizia kwangu kama yeye alivyokuwa akitajwa muanzilishi wa CCJ..kama anataka kujua mimi ni mbunge wa chama gani akawaulize wapiga kura wangu Vunjo,” alisisitiza Mrema.

  MY PIC:
  Nape kakosea kumtaja Mrema kama mshirika wa Kikwete.
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hata kama nimshirika wake wa kweli haya nimakosa nakubaliana na wewe mkuu! sijui kwanini ccm hawaoni mambo anayofanya nape na wakamrekebisha, MAGAMBA YANAENDELEA!
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Kwa hili Nape hajakosea hata chembe, alichokiongea Nape ndio ukweli wenyewe, hata kama sikubaliani na baadhi ya upuuzi wa Nape lakini kwenye hili namuunga mkono kwa 100%
   
 4. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ina maana Nape anapingana na M/Kiti wake?
  Kitendo cha Nape kuwazodoa washirika wa bosi wake kwa mgongo wa upinzani kinamkera sana?....
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mbona hata yeye hajulikani ni CCM au CCJ.
   
 6. F

  FUSO JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,857
  Likes Received: 2,333
  Trophy Points: 280
  Mzee Mrema tulikwambia ukatubishia sasa angalia aibu hii - kijana wa juzi juzi tu anakwambia maneno haya? mzee inabidi siasa uachane nazo kabisa. Huyu kijana wakati unaanzisha ulinzi shirikishi yaani sungu sungu jijini na wakati huo ukiwa Naibu waziri mkuu kama sikosei huyu kijana alikuwa O'level - hata analysis ya mambo ya siasa alikuwa bado kabisa.

  Nakushauri mzee wangu uachane na hizi siasa hawa vijana hawana nia njema na wewe, mpe ujumbe Kingunge pia, wakati umeshawatupa - Pumzikeni muwe washauri tu.

  Na wewe Nape mbona hata sisi hatujui upo chama gani, CCM au CCJ ?
   
 7. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  ccm wamekitumia kibabu hiki sasa hivi wamekiona sio mtaji tena,wanamdump kama maalim seif,..msiwe wabishi kukubali,nape ni mdomo wa JK,kwa kuwa hana guts za kufanya maamuzi magumu,jk anamtumia nape kuongea,...kwanza alimpa udc masasi ili baadae akija kumpa hii kazi ya uvuvuzela asiweze kuikataa..,ccm ina permanent interest not permanent friends,..ila ina permanent enemy,..CDM,hawaongeki kwa miafaka ya kipumbavu,..nape hongera kwa kuwachana hao wasaliti wa wananchi(mrema,seif)ingawa wewe pia ni msaliti wa ccm kwa kuasisi CCJ
   
 8. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mzee wa kiraracha sasa kwishney
   
 9. p

  politiki JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  "Licha ya upinzani kujigamba kuwa wana nguvu ya umma…lakini tukiangalia bado tunaongoza kwa kila kitu, mkoa wa Kilimanjaro tuna wabunge watano wa CCM na watatu wa CHADEMA lakini huyo mmoja wa TLP yeye hajulikani wa CCM au TLP," alikejeli Nape
  hapo ndipo akili ya Nape inapoishia kuganga politics tu. haya unao hao wabunge watano wewe ndio mwenye nguvu tumekubali sasa basi umetumia vipi uwingi wa wabunge kutatua matatizo yetu, yako wapi maji ? , huko wapi umeme? wako wapi waalimu? viko wapi vitabu na maabara mashuleni? hayo ndio matatizo ya msingi ya mtanzania na siyo kushindania idadi ya wabunge ina msaada gani kwa mtanzania hiyo??
   
 10. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  Kweli Nape kaishkia akili sisiemu- hata hawajiulzi uhalali wa kile akiongeacho kwa kfup Nape anafkri kwa niaba ya sisiemu.
   
 11. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Mkuu hili jibu linatosha kabisa
   
 12. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2011
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Hili nalo NENO mkuu senkyuuu...!
   
 13. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Majibu mazuri Mrema. Nape i, uropokaji wako utakufilisi kisiasa na ipo siku utajikuta upo kijiweni, yetu macho kwasasa. Waswahli walisema mbio za panya huishia sakafuni.
   
 14. N

  Ntambaswala JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nape Bwana Mdogo,
  Unakumbuka Oktoba 2010 ulipotembelea Mangaka nilikushauri nini? Punguza sana kuongea maneno ambayo hayana mashiko. Tatizo naona zile stori unazopiga na JK off record wewe unazimwaga majukwaaani. Hebu acha hizo usije kuta watu wakikuona umeingia mahali wananyamaza ili usije kuliyapua mazungumzo yao majukwaani.

  Otherwise kijana una moyo.........................................
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Very intelligent point.

  Siasa za uchaguzi hizi, ukiuliza mtu, ushachaguliwa sasa, unafanya nini, anakwambia nina viti vingi bungeni!!!!
   
 16. j

  jembe afrika JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2017
  Joined: Jan 15, 2014
  Messages: 7,108
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  Kweli alikua hajui
   
 17. M

  Mkwaruu JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2017
  Joined: Mar 13, 2017
  Messages: 1,913
  Likes Received: 963
  Trophy Points: 280
  Ukweli unauma
   
Loading...