tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,500
- 17,729
Moja ya tatizo ambalo limepelekea Wizara ya TAMISEMI ya Hawa Ghasia kuonekana mzigo, ni mtandao wa wizi katika halmashauri nyingi nchini. Lakini inasikitisha kwamba kamati kuu ya ccm IMEKEMEA tu wizi huo badala ya kupendekeza/kushauri wezi hao wafungwe jela. Hii kwa mujibu wa maelezo ya Nape Nnauye alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari.
Kwa kweli kamati kuu haijawatendea haki wananchi wanaokosa huduma za jamii kufuatia ufisadi mkubwa unaofanyika ktk halmashauri. Ni afadhali hata wangelimshauri Rais awaagize hao wezi wamrejeshee fedha walizoiba kama alivyofanya kwa wale wezi wa EPA aliowaagiza wakamrejeshea mabilioni ya fedha za umma walizokuwa wamezikwapua! Ijapokuwa njia hii nayo sio nzuri sana lakini ni nafuu kuliko 'kuwakemea' tu wezi na kuwaachia waendelee kutumbua pesa za umma.