Nape chukua kioo ujitazame kwa nyuma

GlorytoGod

Senior Member
Sep 8, 2012
158
50
Katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Nnauye kwa sasa anajiona anaweza yote hatambui kuwa watu wanajua alikoanguka huko nyuma, lakini leo ananyoosha vidole ili aonekane kwenye kundi la wale wanaostahili kuwa humo.

Miaka michache nyuma Nape alianza kujulikana kwenye siasa za umoja wa vijana wa CCM pale alipojitokeza kwa kuwania nafasi ya uenyekit.

Kwa kuwa mizengwe ilikuwa mingi kutoka kwa washindani wake, alilazimika kuingia na gia ya kupinga mradi wa ujenzi wa jengo la kitega uchumi cha umoja huo akidai uliingiwa mkataba kinyume na uamuzi wa vikao vya juu vya chama hicho.

Mmoja wa watu waliovaliwa njuga na nape kuwa walipindisha mradi huo ni edward lowassa ambaye alikuwa mlezi wa UVCCM. Hapo ndipo ndipo mtifuano ulianza juhudi za funika kombe mwanaharamu apite zikafanyika na kweli watu wakamwona kada huyo ni mtu safi na makini.

Lakini kama wasemavyo wahenga kuwa mkubwa hakosei, aliyekuwa katibu mkuu wa CCM wakati huo yusuph makamba aliiminya hoja hiyo na kisha kutoa taarifa kwa umma kuwa wamemteua andrew chenge kuupitia mgongano huo wa mradi.

Wakati uamuzi huo ukifikiwa, vikao vya wakubwa vikamchinjilia mbali Nape asigombee nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM.

Huku tunaambiwa Chenge anachunguza mradi huo, hapo hapo ujenzi unaendelea ghorofa linaendelea juu nape kimya. Baada ya muda mfupi rais Jakaya Kikwete akamzawadia Ukuu wa Wilaya na madai yake yakaishia hapo.

Baada ya muda si mrefu, Nape akateuliwa kushka wadhifa wake huo wa itikadi na uenezi. Lakini wakati huu hataki kuona kama kuna ufisadi kama ule aliyokuwa akiuona ndani ya CCM wakati huo akitafuta uongozi.

Kumbe kiu ya Nape ilikuwa ni madaraka wala hakuwa na umakini wowote wa kupigania mali za vijana wenzake, ndiyo maana alipoyapata akasahau tuhuma za ufisadi alizokuwa ameziibua awali kuhusu mradi wao.

Nape hatambui kama wananchi wana rekodi yake ya ubabaishaji katika kusimamia mambio ya msing yanayogusa maisha ya watu. Huyu hawezi kusimamia vita ya ufisadi ndani ya CCM kama anavyojitapa leo.

Ndiyo maana hata falsafa ya kujivua gamba ilimshinda mapema kwani alikuwa na siasa zake zile zile za visasi vya kukosa madaraka hivyo akadhani magamba ndani ya CCM ni matatu akapoteza muda kuzunguka na kujitapa kuwa lazima yang'olewe ndani ya siku 90.

Nape hajui kama anapambana na mfumo ndani ya chama chake wale anaopigana kuwaondoa ndiyo roho ya chama, hao ndiyo wamewekeza katika kutengeneza marais wanaowataka.

Alipaswa na anapaswa kuelewa kuwa ndiyo maana hata wakati ule akijitutumua kuupinga mradi wa UVCCM alipozwa na Chenge kuwa Chenge anachunguza mradi, lakini wakati huo ujenzi unaendelea kama kawaida, kumbe tuhuma zake zilikuwa sawa na kilio cha samaki ndani ya maji.

Nape badala ya kupoteza muda wetu kujadili hoja zisizo na mashiko ni bora ukachukua kioo ukajitazama nyuma ulipotoka ili uone ulikosea wapi kiasi kwamba wananchi makini hatuwezi kukwamini hata kidogo katika siasa za uzalendo na utetezi wa watu.

Kwa hiyo ninakwambia nape kama unataka kupambana na ufisadi kubali kujivua gamba wewe kwa kuungana na wapambanaji wa kweli waliotayari kupoteza uhai, mali, familia na hata madaraka yao ili wengine wapate.

Nape tafakari, chukua hatua
 
Nape "ndumilakuwili" anan'gata na kupuliza anawazia tumbo lake 70% na 30% ndio anatumia kuwaza kawaida!
 
Nani ajivue gamba!? Nape??? thubutuu, kama kuna mchumia tumbo namba moja CCM ni Nape, hana uzalendo,utu wala uchungu na nchi hii hata chembe, anachojali yeye ni chama chake na ulaji wake tu
 
nani ajivue gamba!? Nape??? Thubutuu, kama kuna mchumia tumbo namba moja ccm ni nape, hana uzalendo,utu wala uchungu na nchi hii hata chembe, anachojali yeye ni chama chake na ulaji wake tu

huyu anapiga makelele kama mwizi tu hana lolote ili anatafuta ubunge kama fisi anayesubiri mkono wa mtu udondoke naye auokote hiyo ndo kazi ya nape analitaka jimbo la ubungo angali anajua fika yeye na mnyika ni mbingu na ardhi hili jamaa lina dharau sana sijui lilitoka wapi ila yana mwisho kitambi utadhani ana mimba ya miezi 9 anajiandaa kuingia labour kujifungua
 
Dalili ya mvua ni mawingu, hivi Nape mnadhani ubongo uko sawa? Yaani baada ya kupewa ukuu wa wilaya mradi wa UVCCM ukawa hauna kasoro!
 
dalili ya mvua ni mawingu, hivi nape mnadhani ubongo uko sawa? Yaani baada ya kupewa ukuu wa wilaya mradi wa uvccm ukawa hauna kasoro!


haya ndiyo madhara ya vyeo vya kupewa, huyu si chochote wala lolote
 
Back
Top Bottom