Nape! Ccm ni mzigo uliolowa maji, shida sana kuubeba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape! Ccm ni mzigo uliolowa maji, shida sana kuubeba!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Chimunguru, Jul 14, 2011.

 1. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Ndugu yangu Nape! nimefurahi sana kukuona ndani ya JF ukijibu hoja mbali mbali humu, ingawa sina uhakika 100% kama ni wewe maana wajanja wengi wanaweza wakagushi ID na kujifanya ndio wewe. Kama unavyofahamu siasa zetu si ugomvi binafsi ni za kiitikadi zaidi na binafsi hatuchukiani, lakini itikadi zetu zinatofautiana na yote ni katika kulifikisha taifa hili kwenye muelekeo sahihi.

  Kwanza nianze kwa kuwauliza CCM, hivi mnaliona gari lenu linavyokwenda mrama? au kwa sababu mpo ndani ya gari hilo basi mnajiona mpo salama tu kwa vile linakwenda kwa huo mwendo wa kusuasua, breki hakuna ilimradi mfike kituoni 2015 mtushushe tukiwa hoi?
  Nape! CCM yenu ya sasa hivi inafuata itikadi ipi? Ujamaa, Ubepari au kuna itikadi CHOTARA hapo katikati? mnaimba Ujamaa na kutenda ubepari?
  Dhambi mbaya ya UFISADI inaitesa CCM, Mlianza kwanza kujiibia wenyewe! usishangae SUKITA mliifanya nini, bado ipo pale ilipokuwa? mlipomaliza kujitafuna wenyewe, mkahamia kwenye mbuga zetu, LOLIONDO huko mkagawa kwa mwarabu, sijajua ni faida gani tunapata zaidi ya wanyama wetu kuhamishiwa uarabuni. Unamkumbuka Stan Katabalo? maskini mlimtoa kafara kisa muarabu yule shame on you CCM! ingawa Nape unaweza bisha sana kwa vile hukuhusika moja kwa moja lkn huo ndo mrengo wa chama chako, kuuza maliasili za nchi bila kunufaisha wa Tanzania.

  Pili nani kawaambia CCM ina hati miliki ya hii nchi? CCM imeonekana kuwa na nguvu zaidi ya Serikali na hata ukiangalia bunge kipindi hiki utagundua kwamba wabunge wote wa CCM wapo pale kwa maslahi ya chama zaidi kuliko nchi. Mbunge wenu ni rahisi kutetea hoja hata iwe mbovu namna gani ilimradi iliyeileta ni mbunge wenu basi itapigiwa kura kwa wingi, makofi kwa wingi na kupitishwa ili mradi muonekane mmeshinda, yaani km watoto wadogo wanaoshindana kuangua maembe ilhali wakijua kabisa yale mawe yanaweza kuwarudia wao wenyewe na kuwaumiza. Hoja za msingi za wapinzani kwenu ni shubiri! kuna haja gani ya mbunge kwenda bungeni na kuunga mkono hoja asilimia mia halafu anaelezea jinsi umaskini ulivyo katika jimbo lake, miradi haijakamilika, shule hakuna walimu, hakuna zahanati, na kama ipo basi hakuna madawa, wajawazito wanajifungulia barabarani, maji ya bomba hakuna! umeme ndo ndoto za alinacha, lkn CCM ni ya maana zaidi kuliko hawa wananchi wanaowapatia hizo posho na kulipa kodi. Mimi kwa mtazamo wangu CCM nyumba yenu si shwari ndo maana mnaitetea kwa udi na uvumba.

  Tatu hivi Ndugu yangu Nape! miaka 50 ya uhuru inasheherekewa kwa mbwembwe, mnatukumbusha mafanikio ya TANU sijui misingi ya mwana TANU, hebu nileleze leo hii kati yenu nani anayeishi katika misingi hiyo? CCM imekosa mvuto namna hii ndo maana sasa mnakumbushia mazuri ya TANU ili mpate huruma za wananchi? Miaka 50 ya uhuru mji mkuu wa kibiashara hauna maji, hakuna umeme, barabara mbovu za hapa tu mjini wacha mikoani na wilayani. Kile chanzo cha maji cha RUVU miaka yote tunapita toka kwetu kuja Dar yaani kipo vile vile tu! inayojaliwa ni CCM na viongozi wake! Nilidhani katika miaka hii 50 mngetuonesha mafanikio katika viwanda, Kilimo, sayansi na technolojia na si kutukumbusha mambo ya nyuma. Ukikutana na mtu ambaye anatukuza sana maisha yake ya nyuma, yaani kila kitu utasikia zamani bwana, ujue ya leo yamemshinda ndivyo CCM ilivyoshindwa. nakumbuka nikiwa darasa la nne nilisikia kwenye taarifa ya habari kwamba serikali ina mpango wa maji kwa wote ifikapo mwaka 2000. hiyo ilikuwa 1985 na najua waliona 2000 ni mbali saaana lkn ilifika na KIU iliendelea kutukamata zaidi hayo maji hatukuyaona kwa wote kama mlivyoahidi.

  Nne CCM ni mzigo, tena uliolowa na kufyonza maji na kuwa mzito mara mbili ya awali na hivyo kutuelemea vibaya mno. Lini mtakuwa na tabia ya kuwajibika kwa wananchi? mlipewa dhamana na wapiga kura(km hamkuiba kura) lkn hamuwatendei haki yao ipasavyo, waziri mwenye dhamana ya ulinzi mabomu ya mbagala na GOMZ raia waliuawa bure na mali zao kuteketea, lkn hakuna aliyewajibika, mmeona kule Cyprus? waziri na mkuu wa majeshi wote wamejiuzuru! uzembe ukitokea lazima mtu anayehusika na kile kitu awe wa kwanza kupisha uchunguzi! nyie ndo kwanza mnaunda tume ili muendelee kula kodi zetu vizuri. CCM mna kiburi sana, mmeunda kikundi cha maslahi yenu binafsi mnagawa vyeo, mnalindana hata pale penye uozo. Hakuna viongozi waadilifu tena ndani ya CCM, kila mmoja ana skendo yake! Baba wa taifa alitoa wosia wa baadhi ya viongozi wasiofaa akatunga na kitabu kabsaa juu yao na wengine akasema hawajakomaa kutuongoza na kweli sasa imekuwa asiyesikia la mkuu huvunjika guu na majuto yetu saa ni mjukuu!

  Tano ndugu yangu Nape ni Katiba! naomba msicheze juu ya Katiba mpya, tunahitaji katiba mpya tuutue huu mzigo uliolowa maji! kwa sheria za sasa mtaendelea kutuibia kura zetu, tunataka 2015 kwenye uchaguzi mpya tuingie na katiba mpya. Mwambie mwenyekiti wako katiba ni ya wananchi na si ya CCM! wananchi ndo tutaandika katiba juu ya vile tunataka nchi yetu iendeshwe na si NYIE CCM mtuandikie katiba. hapa napandwa na Hasira sababu hii katiba mbovu tuliyonayo, ndiyo chanzo cha haya yote tunayoyaona sasa, kuna mambo mengi sana yanahitajika kuwekwa kwenye katiba, ikiwapo TUME HURU ya uchaguzi ambayo haichaguliwi na Rais, tume ambayo itakuwa na mchanganyiko wa watu wa rika na kada tofauti tofauti. Tume ambayo itakuwa na uwezo wa kisheria wa kuendesha shughuli zake bila shinikizo toka kwenu CCM. Mueleze waziri wa katiba na sheria yeye hayuko pale kutuamulia sisi juu ya katiba yetu! mtuache tuandike katiba tunayoitaka, tena liundwe bunge la katiba na si hili RUBBER STAMP yenu mnayotumia kutukandamiza kwa kupitisha mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi. kwa leo haya matano yanakutosha Nape! Kesho ntakuja na suala la MUUNGANO mungu akijaalia, KAZI NJEMA!
   
 2. t

  tumpale JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 201
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hiyo ni kweli tupu,ona ujinga wao wanakosoa vitu vyote mwisho wanaunga mkono hoja asilimia mia kwa mia, sijui ni wendawazimu.
   
 3. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  upo sawa kabisa atajibu nini nape akijitahidi atakupachika jina mchochezi hawa wenzetu ukisema kweli utaitwa mdini mkanda au unahatalisha amani iliyo dum kwa mda tz
   
Loading...