Money Maker
Senior Member
- Jul 11, 2011
- 146
- 31

HIVI NI kweli tukisema kwa ujumla KUWA hakuna kilichofanyika nchini toka tupate uhuru toka kwa wakoloni Mwaka 1961?

Tumefanikiwa kununua VX, GX, V8 nk nyingi sana

HIVI NI kweli tukisema kwa ujumla KUWA hakuna kilichofanyika nchini toka tupate uhuru toka kwa wakoloni Mwaka 1961?

hivi umekosa kazi ya kufanya tukupe mpunga uuze.. Tunajua kwamba wanaowapa kura ni akina mama sababu wana shida na kanga. Yan ccm inanuka,hakuna mwenye akili timamu anaethubutu kuitaja. Wewe unafikiri nyerere angekuwepo wewe na aliyekuweka hapo mngekuwa kama mlivyo.? C mngekuwa mnauza vinyago mwenge ss hv. Huna cha kutuambia ss hv,wkt hujui kama kuna watu wanakula mlo 1/day,
[h=3][/h]NA MWANDISHI WETU
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kitahakikisha katika mabadiliko yake ya sasa kinawarejesha katika kuujua ukweli vijana waliopotoshwa na wapinzani hadi kufikia hatua ya kudhani hakuna mazuri yaliyofanywa tangu uhuru.
Mikakati hiyo ilisemwa jana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye wakati akizungumza na baadhi ya viongozi na watangazaji wa Clouds Media Group, Mikocheni Dar es Salaam, alipofanya ziara ya kujitambulisha katika wadhifa wake huo na kueleza mabadiliko yaliyofanywa na Chama, mapema Aprili mwaka huu.
Alisema, wakati wapo vijana ambao hawakuipigia kura CCM katika uchaguzi mkuu uliopita kwa sababu zinazoonekana kuwa za msingi, lakini ipo idadi kubwa ya vijana ambao walifanya hivyo kutokana na chuki tu kutokana na kushibishwa na uongo na baadhi ya vyama vya upinzani.
Nape alisema katika miaka ya karibuni hasa baada ya kupevuka kwa kiwango kikubwa mawasiliano kwa njia ya mitandao kwenye kompyuta, baadhi ya vyama hivyo vimetumia na vinaendelea kutumia mawasiliano hayo kueneza uongo kwa njia hiyo na kufanikiwa kuwanasa vijana wengi kwa kuwa ndio wanaopendelea zaidi kutumia mawasiliano hayo ya mtandao.
"Baada ya vyama vya upinzani kujua kwamba vijana wengi wanapenda zaidi upashanaji habari kwa njia ya mitandao kwenye kompyuta, kuliko mikutano ya hadhara na njia nyingine za kawaida, baadhi ya vyama hivi vimetumia sana njia hii kuwajaza uongo vijana", alisema Nape.
"Na kwa sababu uongo ukizidi kuenezwa bila kupingwa huweza kuonekana ndiyo ukweli, baadhi ya vijana wameamini uongo huo, na matokeo yake wamejenga chuki kiasi cha kutoyaamini hata mambo ya maana na ya msingi wanayoambiwa na CCM na serikali yake jambo ambalo ni hatari kwa hatma ya taifa", alisema Nape.
Alisema katika mikakati yake ya sasa CCM itahakikisha inawapa ukweli kupitia njia hiyo ya mawasiliano ya mitandao ya kwenye kompyuta kama 'face book' na kueleza matumaini yake kwamba hatua hiyo itazaa mafanikio kwa kuwa yameanza kuonekana katika hatua za awali ambazo CCM imeanza kufanya.
Nape alisema, CCM inafanya hivyo kwa kuwa bado kina uwezo wa kuongoza huku kukiwa hakuna chama cha upinzani ambacho kinaweza kujitapa kuwa kinaweza kuongoza nchi kwa uhakika ikilinganishwa na hali inayojionyesha katika vyama hivyo hadi sasa.
Alisema, mbali ya kuyaendea makundi ya vijana, CCM pia imejipanga kuyafikia kwa ufanisi zaidi makundi yote, kwa kutumia njia mbadala, ikiwemo kufuatilia kwa karibu maoni ya vyombo vya habari hasa vile vinavyoonekana kuwa makini zaidi katika kutoa habari zake.
Nape aliahidi CCM kutoa ushirikiano mkubwa kwa vyombo vya habari katika kuhakikisha vinapata habari za ukweli, sahihi na kwa wakati kuhusu chama na hata za ndani ya serikali.
"Tunaamini sisi CCM tukifungua masikio yetu vilivyo kwa vyombo vya habari tuyaweza kuongoza nchi kwa usahihi zaidi, kwa sababu ninyi vyombo vya habari ndiyo mliopo mitaani wakati mwingi, hivyo mnaweza kuwa mnayajua mengi kuliko sisi, ni vizuri tukawa tunawasikiliza na kufanyia kazi mnayosema", alisema Nape.
Katika ziara hiyo, Nape alizungumzia kwa kina dhana ya mabadiliko ndani ya Chama na utekelezwaji wake unavyoendelea na baadaye waandishi wa Clouds Media Group walipata fursa ya kuzungumza na kumuuliza maswali yaliyoona yanafaa.
Baadaye Nape akiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni hiyo ambayo ni walimiki wa vituo vya Clouds FM, Choice FM na Clouds TV, Ruge Mutahaba alipata fursa ya kutembelea baadhi ya vituo hivyo kuona kazi zinavyofanyika.
Source: fullshangwe.blogspot.com
Kaka nape 'habari chowani'
hapo nape andika ameumia sisi siyo mazuzu kufuata upepo,
nasema tena , kwanza hatukuwahi kuwa ccm na kuwa na kadi za ccm. Acha dharau. Uturejeshe kwani sisi tumekuwa mizigo? Tatizo lenu ccm mnakuwa kama bi kirembwe katika nchi ya giningi. .....nyeusi mansema nyeupe na nyekundu mnasema njano, basi na sisi mnataka tuamini hivyo. Hizo zama zimepitwa na wakati, sasa hivi vijana tunajua nyekundu ni nyekundu na nyeusi ni nyeusi. Rudi masasi nape ukainue wakulima wa korosho. Kwa taarifa yako nape ujue kuwa vijana wengi siku hizi hawasikilizi hyo redio, imekosa mvuto kupitia mtangazaji wake yule mc wa ccm, ephraim kibonde.
Naichukia clouds fm
Habari chowani, kaka kwa taarifa hatujawahi kuwa wanachama wa ccm hivyo hatuwezi kurejea au kurejeshwa sehemu ambayao hatjawahi kuwepo hapo awali. Tataueni kero za wananchi. Nafurahi wewe ni wa nyumbani kabisa... Hivi kaka unajisikiaje kwa serikari inayoongozwa na chama chako kutokuwa na msimamo na maamuzi magumu? Pia elewa kuwa radio clouds fm vijana wengi hasa wanaopiga kura huwa hawasikilizi...... Wamwchoshwa na yule mc wenu mnayempa tenda, ephrahim kibonde, kwa hiyo andika hautafanikiwa kwa hili. Toeni vibanzi machoni penu kwanza ndipo ujaribu hilo unalodhamiria.
HIVI NI kweli tukisema kwa ujumla KUWA hakuna kilichofanyika nchini toka tupate uhuru toka kwa wakoloni Mwaka 1961?
Nazipokea kwa unyenyekevu MKUBWA kejeli na kasha zote...LAKINI naheshimu sana pia wale waliojaribu kujadili HOJA ...
Wametaja hapa idadi ya wanafunzi walio vyuoni KUWA NI zaidi ya 70000.... Hivi wakati tunapata uhuru wanafunzi WA Elimu ya juu kwa takwimu ZENU walikuwa zaidi ya ho NADHANI NDO MAANA Leo twasema inashuka idadi BADALA ya kuongezeka.....
Nani kawatukana vijana.? Nilichosema vijana wengi Mwaka jana walionekana mutiny ga mkono CCM, na hii NI kwa MUJIBU WA matokeo ya utafiti SI NAPE.... SABABU NYINGI ZINAZOTOLEWA KWAKWELI NYINGI SI ZA KWELI JUU YA SABABU ZA UAMUZI HUO WA VIJANA.... SASA HAPA TUSI LIKO WAPI?
Hapa namtetea Nape naona mnamuonea kijana mwezenu. sikiliza kauli hii" Mzee Nyerere akuyamaliza akaja Mzee Mwinyi Miaka 10 akuyamaliza akaja Mzee Mkapa miaka 10 hakuyamaliza na mie nitamaliza miaka 10 sitoyamaliza". mwe!
Hapa sioni tatizo la Nape liko wapi! kama Rais wa nchi hajui kwa nini Tanzania ni maskini mnategemea nini hapo? katika zile ajila millioni moja alizoahidi Rais Kikwete mojawapo ni hiyo aliyopata Nape Nnauye. sasa tumuacheni kijana mwenzetu nae atengeze maisha yake kumbukeni ana familia inahitaji matunzo yake, Nape hawezi kuiga uadilifu wa Baba yake kwa sababu anajuwa matunda ya uadilifu ndani ya ccm = kufa maskini, wafananishe Timoth Apiyo na Philemon Luhanjo je maisha yao ni sawa? wote hawa wametumikia cheo kimoja pale ikulu.
Nape nakuomba ongeza ziara za kichama kwa kadili ya uwezo wako ili uvune posho za nguvu kwa haraka, mwakani ni uchaguzi mkuu ndani ya ccm huenda ukatupwa nje ya uongozi huu, ndio wakati wako sasa, kumbuka mwenyekiti wako ni kinyonga huwa hajulikani langi yake kamwe. na ningeshauri kama haujawahi kufika Marekani huu ndio wakati wako, ongea na William Malecela pangeni dili umwambie Wilson Mukama kwamba Vijana wamekualika Marekani ukafunguwe matawi kwenye majimbo 20 ili litakuongezea posho zaidi na siku za kukaa Marekani. ukipuuza ushauri huu utakuja kunikumbuka na utajuta.