Nape: CCM kuwarejesha kwenye ukweli vijana waliopotoshwa na wapinzani

Nape said:
Nazipokea kwa unyenyekevu MKUBWA kejeli na kasha zote...LAKINI naheshimu sana pia wale waliojaribu kujadili HOJA ...
Wametaja hapa idadi ya wanafunzi walio vyuoni KUWA NI zaidi ya 70000.... Hivi wakati tunapata uhuru wanafunzi WA Elimu ya juu kwa takwimu ZENU walikuwa zaidi ya ho NADHANI NDO MAANA Leo twasema inashuka idadi BADALA ya kuongezeka.....
Nani kawatukana vijana.? Nilichosema vijana wengi Mwaka jana walionekana mutiny ga mkono CCM, na hii NI kwa MUJIBU WA matokeo ya utafiti SI NAPE.... SABABU NYINGI ZINAZOTOLEWA KWAKWELI NYINGI SI ZA KWELI JUU YA SABABU ZA UAMUZI HUO WA VIJANA.... SASA HAPA TUSI LIKO WAPI?

Nape,

..unacheza na maneno na data.

..ni kweli tuna vijana wengi ktk vyuo vya elimu ya juu kuliko wakati wowote ule, which is a +ve thing.

..sasa nakuomba uende mbele na kujaribu kulinganisha kama kweli vijana hao wamepikwa kitaaluma kulinganisha ni miaka ile tulipokuwa na UDSM peke yake.

..pia kuna fahari gani kuwa na vijana wengi ktk vyuo kikuu wakati hali hiyo haiambatani ni hatua zozote zile kuhakikisha kwamba wanaajiriwa kwa kazi za kitaalamu mara wanapomaliza masomo?​


 
Safi sana,
Nape unasema kuwa hakitatosha mpaka unakufa, maana yake haiwezekani kwa lugha rahisi ndio kikomo cha maarifa chako au CCM. Mwanafalsafa mmoja alisema, ukiona haiwezekani ni mwisho wa uwezo wako kufikiri na kutenda wapo kwao kinawezekana. Umesema kuwa wezi na mafisadi mlikuwa nao tangia azimio la arusha, kumbuka bado unaongelea mfumo ulioshindwa wa Tanu/CCM. Mmeshindwa kwenye ngazi zote ungozi na usimamizi wa mali ya umma na kuinua uchumi wa nchi kwa rasilimali zilizopo.

Tukisema CCM imeshindwa tunamaana gani.
Kwa rasilimali tulizo nazo, Tanzania ingekuwa mbali sana kiuchumi kwa miaka 50. Ukumbuke Mwl Nyerere ilimlazimu kuachia ngazi baada ya kuua uchumi wa nchi, aliondoka nchi ikiwa taabani. Miaka ya 84 kulikuwa na hali mbaya sana ya uchumi, viwanda vingi alivyoaanzisha kwa kipato kilichotokana na uwekezaji wa wakoloni, kama, mkonge, pamba , kahawa vilikufa vyote. Kwa miaka hamsini hakuna kitu TANU?CCM imekifanya zaidi ya kuua vilivyokuwepo.

Mipango miji ilikuwa mizuri miaka ya sitini/sabini/na themanini na hii ni kwa sababu tulirithi ya wakoloni baada ya CCM kushika hatamu mlianza kugawa viwanja hata sehemu za kujenga shule, vyoo, maeneo ya wazi nk. Leo miji iko shaghalabala. Tumeshindwa kuendesha nchi kuendana na ukuaji na ongezeko la watu. Matokeo ya uosefu waajira, hali mbaya za huduma za afya ni kutokujiaandaa kwa miaka zaidi ya 50 iliyopita.

Ukiwa mfanyabiashara ukashindwa kujua unakokwenda lazima biashara yako ife. Viongozi wa Tanzania wamekosa vision kwaq miaka hamsini. Yanayotokea leo ni kushindwa kwa tawala za Nyerer/mwiny/mkapa na hatimaye JK.

Nape tukiwa wa wazi na wakweli bila kujali itikadi za vyama, tukichora jedwali la maendeleo la Tanzania mstari utaanza kushuka kuanzia 1975 mpaka leo, hakuna kukua kwa uchumi wala kuendelea kwa nchi.

Uchumi kukua ni pamoja na kukidhi huduma za jamii na kupamabana na changamoto zilizopo. Ni pamoja na kujiandaa na misukosuko ya uchumi.
Nape leo kunawanafunzi zaidi ya 70000 kwenye vyuo vikuu Tanzania ni nini mpango wa serikali yako kuwapatia ajira au kutengeneza mazingira ya ajira zaidi ya kuandaa bomu la vijana wasomi wasio na ajira?

Nape ukiachana na Vijana jaribu kutembelea wazee uwaulize je maisha ya leo na miaka 25 iliyopita ni yapi mazuri?
Hapa namtetea Nape naona mnamuonea kijana mwezenu. sikiliza kauli hii" Mzee Nyerere akuyamaliza akaja Mzee Mwinyi Miaka 10 akuyamaliza akaja Mzee Mkapa miaka 10 hakuyamaliza na mie nitamaliza miaka 10 sitoyamaliza". mwe!

Hapa sioni tatizo la Nape liko wapi! kama Rais wa nchi hajui kwa nini Tanzania ni maskini mnategemea nini hapo? katika zile ajila millioni moja alizoahidi Rais Kikwete mojawapo ni hiyo aliyopata Nape Nnauye. sasa tumuacheni kijana mwenzetu nae atengeze maisha yake kumbukeni ana familia inahitaji matunzo yake, Nape hawezi kuiga uadilifu wa Baba yake kwa sababu anajuwa matunda ya uadilifu ndani ya ccm = kufa maskini, wafananishe Timoth Apiyo na Philemon Luhanjo je maisha yao ni sawa? wote hawa wametumikia cheo kimoja pale ikulu.

Nape nakuomba ongeza ziara za kichama kwa kadili ya uwezo wako ili uvune posho za nguvu kwa haraka, mwakani ni uchaguzi mkuu ndani ya ccm huenda ukatupwa nje ya uongozi huu, ndio wakati wako sasa, kumbuka mwenyekiti wako ni kinyonga huwa hajulikani langi yake kamwe. na ningeshauri kama haujawahi kufika Marekani huu ndio wakati wako, ongea na William Malecela pangeni dili umwambie Wilson Mukama kwamba Vijana wamekualika Marekani ukafunguwe matawi kwenye majimbo 20 ili litakuongezea posho zaidi na siku za kukaa Marekani. ukipuuza ushauri huu utakuja kunikumbuka na utajuta.
 
...............Nami NAKUBALIANA NANYI KUWA KILICHOFANYIKA HAKITOSHI, NA KWA NIJUAVYO HAKITATOSHA MPAKA NINAKUFA, ISIPOKUWA RELATIVELY NI KWELI KUWA PENGINE SPEED HAIRIDHISHI SANA. LAKINI KWAMBA VIONGOZI WASASA KWA UJUMLA WANABOMOA KILICHOJENGWA HILI SIJALIELEWA..........

Well, ukiangalia kwa undani maelezo hayo hapo juu......utagundua kuwa yanawiana na ile statement ya "Sijui kwanini Watanzania ni Maskini"..........trust me with these type of minds.............we are doomed..........
 
Nazipokea kwa unyenyekevu MKUBWA kejeli na kasha zote...LAKINI naheshimu sana pia wale waliojaribu kujadili HOJA ...<br />
Wametaja hapa idadi ya wanafunzi walio vyuoni KUWA NI zaidi ya 70000.... Hivi wakati tunapata uhuru wanafunzi WA Elimu ya juu kwa takwimu ZENU walikuwa zaidi ya ho NADHANI NDO MAANA Leo twasema inashuka idadi BADALA ya kuongezeka.....<br />
Nani kawatukana vijana.? Nilichosema vijana wengi Mwaka jana walionekana mutiny ga mkono CCM, na hii NI kwa MUJIBU WA matokeo ya utafiti SI NAPE.... SABABU NYINGI ZINAZOTOLEWA KWAKWELI NYINGI SI ZA KWELI JUU YA SABABU ZA UAMUZI HUO WA VIJANA.... SASA HAPA TUSI LIKO WAPI?
<br />
<br />
Na ndiyo maana wewe na chama chako mnachimbia kaburi elimu.kila siku utetezi wenu kwenye elimu ni kulinganisha takwimu za sasa na zilizopita.kwa nini mnajali quantity zaidi ya quality?Hizi propaganda ni bora ukazihubiri kwa wasioelewa,na ambao ndo mtaji wenu uliobaki.Serikali ya CCM imegeuza Education iwe ni schooling!
 
Nape, mbona wajisumbua na kukazana kuvuta suka wakati kisiasa Tanzania tayari kumekucha???????? Too late to catch a moving bus; kahifadhi hizo nguvu kwa kazi nyingine mkuu!!!!!!!!!!!!!
 
Nape bwana...kwel maendeleo yapo mfano hakuna walimu wa UPE, lakini Umri wa miaka50 haulingani na maendeleo tuliyokuwa nayo mkuu...angalia nchi nyingine tulizopata nazo uhuru sasa hivi zipo wapi mkuu..mfano angalia Kenya...umeme kwa miaka 50 tupo gizani mkuu
 
Nazipokea kwa unyenyekevu MKUBWA kejeli na kasha zote...LAKINI naheshimu sana pia wale waliojaribu kujadili HOJA ...
Wametaja hapa idadi ya wanafunzi walio vyuoni KUWA NI zaidi ya 70000.... Hivi wakati tunapata uhuru wanafunzi WA Elimu ya juu kwa takwimu ZENU walikuwa zaidi ya ho NADHANI NDO MAANA Leo twasema inashuka idadi BADALA ya kuongezeka.....
Nani kawatukana vijana.? Nilichosema vijana wengi Mwaka jana walionekana mutiny ga mkono CCM, na hii NI kwa MUJIBU WA matokeo ya utafiti SI NAPE.... SABABU NYINGI ZINAZOTOLEWA KWAKWELI NYINGI SI ZA KWELI JUU YA SABABU ZA UAMUZI HUO WA VIJANA.... SASA HAPA TUSI LIKO WAPI?

Nape nafurahi unapojibu na nakushukuru kwa kuendelea kuwepo,
Ndugu yangu, wakati tunapata uhuru tulikuwa wachache sana sidhani kama tulizidi 15milioni. Shele zinaendana na idadi ya watu. Ila kwa sasa tuna shule nyingi sana na vyuo vya kumwagwa kwa majengo mabovu na elimu mbovu. Nape Elimu sio uwingi ni ubora ya unachozalisha. Soko la ajira linakuwa tabu na bidhaa tunazozalisha hazipati soko nje kwani sio bora (Elimu). Nape ni kwanini miaka ya 50 na tukiwa na vyuo vingi na sekondari nyingi bado tunaajiri wataalaamu kutoka nje? Kwa nini leo tukitaka kuchimba madini, kujenga madaraja , kujenga viwanja vya mpira kuwa na wakaguzi wa mahesabu lazima tuite wageni? unajua tatizo ni nini? Kwa nini leo tuna vyuo vua udaktari ila hakuna mkurugenzi, wala Raisi anayekubali kutibiwa hapa Tanzania?

Ni kweli kuna vyuo vingi ila havina tija, hakuna viwango wala hakuna washindani? Kwa nini leo kila mtanzania anataka kupeleka mtoto wake kwenye hizi academy? Ubora wa shule za kata uko wapi? Ni kweli academy zinaweza kuandaa watanzania wote?

Nape mimi sipendi kukupinga kama kasuku ila nataka kujua nini ninyi bado mnacho ili kuweza kutatua matatizo ya msingi tuliyonayo. Nchi za wenzetu wanashindana kwenye sayansi na kuzalisha wasomi ambao wanaweza kupambana kwenye dunia ya leo. Sasa kama uwingi wa vyuo ambavyo wanasoma nusu mhula namihula mingine wamefukuzwa ndio unaita ongezeko hiyo ni balaa. Kama ongezeko ni shule za kata ambazo wewe huwezi kubali mtoto wako aende ndio unaita elimu hongera. Nape sisi sote tulisoma shule za serikali na zilikuwa zinatoa elimu bora, ni wakati ule private ilionekana sio bora. Dunia nzima shule za serikali zina imarishwa kwani ni kimbilio la wengi, isipokuwa Tanzania.

Twende kwenye ajira, wakati tunapata uhuru soko la ajira liliendana na uzalishaji wa wasomi. Sasa ni wapi tumekosea, tuache visingizio. Nchi makini duniani zinaratibu shughuli za maendeleo na ongezeko la watu, na kuweka uwiano wa rasilimali najinsi ya kuzitumia. Tanzania sasa imekuwa kichaka cha wawekezaji wezi na ninyi viongozi mnaonekana kukosa suluhisho.

Nape kitwakimu nchi inafanya vibaya sana ukilinganisha na miaka 30 iliyopita. Sababu kubwa ni kukumbatia wazembe, wezi, na mafisadi. Hatuna sababu ya kukosa hospitali mbili kubwa na bora Tanzania. Hatuna sabau ya kukosa vyuo vikuu vyenye hadhi ya kimataifa walau viwili.

Nape sababu za kukosa umeme ni za kutengeneza. Matatizo ya umeme yakianza miaka ya mwanzoni mwa 90, watu mbali mbali walitoa mapendekezo ya nini kifanyike, leo tupo gizani na majibu kibao ya kisiasa. Ni nchi gani inaweza kukuza uchumi bila nishati??? Je huoni huu ni uzembe wa serikali kwa lugha yeyote ile?

Serikali makini makini duniani, zinzotaka kukuza uchumi wake zinazingatia mambo makuu matatu. Nishati, usafiri wa ardhini, maji, anga na reli, kukuza mawasiliano na kuhakikisha huduma za jamii zinafika popote. Then mwananchi anaachiwa achacharike. Kamanda vyote hivyo hakuna tutajengaje nchi??

Tanzania ya leo ni bora kuliko ya jana?????
 
HIVI NI kweli tukisema kwa ujumla KUWA hakuna kilichofanyika nchini toka tupate uhuru toka kwa wakoloni Mwaka 1961?
Ingependeza ungetuambia kilichofanyika ni kipi na ni uongo upi tulioshibishwa. Iyo ndo namna pekee ya kujibu hoja.
 
Asante Nape!

Sisi Vijana ( Hasa tunaotumia mitandao ya Kijamii ambao kimsingi tunaweza kupata bahati ya kuhudhuria darasani kwa miaka kadhaa) tunasikitika sana maana Wapinzania wamekuwa wakipotosha sana na sisi kwa Uelewa wetu Finyu hawa wapinzani tumekuwa tukipelekeshwa kama Tiara. Wenzetu wa Vijini (Ambao wana uelewa Mkubwa) wameukataa Huu upotoshwaji wa Wapinzani na wameendelea kuwa watiifu kwa CCM.

Kaka yetu Nape hawa wapinzani ( Wajukuu kama nunavyopenda kuwaita katika Mikutano yako) wamekuwa wakipotosha sana mfano eti wanasema kwamba

1. Bei ya Sukari imepanda sana kiasi kwamba eti ni Watanzania wachache wanaoweza kumudu kunywa chai. Eti kaka Nape kuna ukweli wowote jamani

2. Wanasema eti wabunge wetu wapendwa wa CCM kwa kushirikiana na Serikali yetu Tukufu inayoongozwa na Rais wetu Mpendwa ( Ambaye wewe hupenda kumwita Jemedari) walipendekeza eti Bei ya Mafuta ya Taa ipandishwe ili kupambana na Wachakachuaji. Hii habari ya Kweli kaka Nape? Mimi sijawaamini hawa Wapinzani mpaka nisikie kauli kutoka kwako na maana umesema leo utakuwepo basi nitakusubiri unieleze ukweli ni Upi? Kwamba sasa bei ya Mafuta ya Taa inalingana na bei ya Dizeli. Mh Ama kweli wapinzani wamezidi kwa Uongo maana mimi najua mwezi wa sita nilinunua mafuta ya Taa kwa shilingi 1,100 leo wanatuambia eti mafuta ya taa ni shilingi 2100 kwa lita

3. Halafu juzi nimewasikia eti wanasema yule Katibu wa Wizara ya Nishati aliyechangisha Pesa kuhonga Wabunge wetu ili ile Bajeti ya Nishati ipite eti Hana kesi ya Kujibu. Wapinzani bwana kwa nini wanatupotosha sisi vijana hivi? Eti Waziri Ngeleja hajui ule Mpango dah.

4. Juzi ndio nikachoka kabisa na uongo wa hawa Wapinzani. Eti wanadai Nchi iko kwenye Mgao wa Umeme, kwa nini mnawaacha wanapotosha hivi jamani! Eti wanadai watu wamefunga salon, wamefunga stationery zao na wengine wamefunga viwanda vidogo. Hawa wapinzani waongo sana. Eti ni kweli kaka nape Kuna Mgao? Hata kama upo kwani umeathiri nini ? mbona maisha yanaendelea kama kawaida. hebu utupe Ukweli juu ya huu Upotoshaji

5. Juzi nilimsikia Mmoja akisema eti Kujivua Gamba ni Chuki na Mbio za kuelekea Urais? eti ni kweli? kwamba Sitta anamuogopa Lowasa kuwa Raisi wa Tanzania 2015? Wanasema eti List of Shame ya Dr. Slaa ( Wewe unapenda kumwita Padre aliyeasi) ilikuwa na watu 11 na Mwenyekiti wetu alikuwa namba kumi na Moja sasa mbona Tunakomaa na Lowasa , Chenge na Rostma. Kaka Nape Naomba utuambue Ukweli ni kweli Mwenyekiti wetu anahusika na Mkataba wa Kinyonyaji wa IPTL ambao unalifilisi shirika letu la TANESCO? Mh mimi siamini kwa kwelu tunaomba ukweli wa hili na kama Mna mpango wa kumvua Gamba Mwenyekiti

6. Eti ni kweli kwamba mwaka jana Waliohitimu kidao cha nne 88% walifeli? mimi siamini ukizingatia kwamba Serikali yetu imejitahidi sana kutengeneza walimu ingawa Wapinzani wanawaita Vofa Fasta.

7. Eti wanasema kwamba Tumegawa machimbo ya Madini kwa wawekezaji na sisi tunapata Asilimia 3%. ni kweli nape? mbona hawa jamaa ni waongo hivi kaka nape?

Ninayo mengi ya Kizushi yaliyozungumzwa na Wapinzani naomba kwanza Unifafanulie hayo hapo juu moja baada ya jingine
 
Nashukuru KUWA tunakubaliana SASA at least kwa nyinyi WACHACHE KUWA. SI KWELI KUWA HAKUNA KILICHOFANYIKA! Hii NZURI , ! Nami NAKUBALIANA NANYI KUWA KILICHOFANYIKA HAKITOSHI, NA KWA NIJUAVYO HAKITATOSHA MPAKA NINAKUFA, ISIPOKUWA RELATIVELY NI KWELI KUWA PENGINE SPEED HAIRIDHISHI SANA. LAKINI KWAMBA VIONGOZI WASASA KWA UJUMLA WANABOMOA KILICHOJENGWA HILI SIJALIELEWA.... TUKISEMA BAADHI WAMEKUWA WEZI SI JIPYA LILIKUWEPO HATA ENZI ZA AZIMIO LA ARUSHA NA ENZI ZA UHUJUMU UCHUMI, SASA MJADALA HAPA UTAKUWA JE HATUA ZINAZOCHUKULIWA ZINATOSHA KULINGANA NA HUJUMA ILIYOFANYIKA......

Bwana Nape mimi sikupigia kura CCM kutokana habari nilizoshibishwa, habari zenyewe ni issue ya MEREMETA,EPA,RADA na ufisadi kwa ujumla. Je hizi ndo habari za uongo unazosema vijana tunashibishwa ?
Pia nitaendelea kuhamasisha vijana na wazee wote kutokupigia kura CCM kwa sababu dhahiri kama HOJA YA KUJIVUA GAMBA,SHULE ZA KATA,UMEME, MAJIBIZANO BAINA YA VIONGOZI NDANI YA CCM na MWENENDO WA WABUNGE WA CCM KWENYE UCHANGIAJI WA HOJA BUNGENI.
Kila mwezi December nitahakikisha nitamdokeza kila mchaga ninayemfahamu na anayekwenda KILIMANJARO kuhesabiwa afikishe ujumbe kwa koo sii chini ya saba kwa kila kitongoji kuwa BWANA NAPE amesema hawezi kushiriki jambo na Wachaga so wachaga hawapaswi kuipigia kura CCM ili kutojumuika na Bwana Nape.
 
HOJA ipi? Twende moja BAADA. Ya nyingine

Hoja ya kwanza: Mnafahamu kuwa CCM pamoja na Viongozi wake wanaamini waTz si watu wa kuaminika hadi inafikia Rais na mwenyekiti wake anabariki wawekezaji kuwaleta tungu zao kuja kufanya kazi hata za Kufanya usafi humu TZ? Kama jibu lake ni hapana tuazishe Post itakayo waunganisha vijana wote TZ kwajili ya kuwataja hawa wageni wanaofanya kazi hadi za usafi tanzania kwa kisingizio cha uwekezaji?

Pili: Unafahama kama wananchi wengi wanaumia na uzembe wa CCM/Viongozi wake kiasi cha Nchi inakuwa kwenye giza ile hali watu wakichukua madini na rasilimali zetu bure? mfano Umeme mwingi ukitumika katika machimbo ya madini huku sisi tukiwa gizani?

Tatu: Tangu 1st July wauza Mafuta walikaidi amri ya kushusha bei ya mafuta na waTZ tukapa usumbufu pasipo na msingi wowote mpaka sasa? Na hadi sasa hakuna hatua iliyochukuliwa na CCM/Serikali kwa wale walokaidi?

Nataka majibu.
 
katibu wa itikadi na uenez hicho ndio cheo chako, kiuhalisia vijana wanajua wanalolifanya mana wana utashi nakufikiri kwa mapana wala si kwamba wamedanganywa ila ni utofauti wakimaisha uliopo kati ya walionacho hasa viongoz na wasionacho wananchi wakawaida. Vijana hawahitaji kurejeshwa ila wanataka viongoz waadilifu,wawajibikaji,na watakao waletea maendelea wananchi.Zama za ushabiki wavyama zimepitwa na wakati sasa hivi kuleta maendeleo ndio mtaji.
 
Huyu kijana akili timamu lakini tatizo lake ni moja tu, huwa anatumia upumbavu wake kufikiri badala ya akili, na ndio maana kila siku anaonekana anaongea upuuzi mtupu, na hii haitokani na akili yake mwenyewe bali ni akili za kushikiwa na viongozi wa juu. Hii mnaweza kudhibitisha wenyewe si mnakumbuka kipindi kile alipowadandia kina Lowasa kuhusu ufisadi ndani ya ccm alivyokuwa anatema mawe! Sasa leo vipi anaongea nonsenses tupu au mnaweza kuniambia ni huyu si Nape bali ni mwingine?
 
Wazo lake ni zuri, huo ni mtizamo wake lakini je (1)ccm imewasaidiaje wasomi wanaodhurura na kushida kijiweni na digirii zao posipo na ajira baada ya kuipata elimu hiyo kwa mbinde (fedha kiduchu ya kujikimu mikopo ya ada inayotoka kwa kushinikizwa na maandamano ilhali ni haki yao hasa watoto wa walala hoi?).(2)Nape utawarudishia vipi machiga mali na mbio mlizowapora na kuwageuza wakimbizi wavunja sheria ndani ya nchi yao?.(3)utavunja magereza kuwaokoa kuwalipa fidia vijana lukuki walioelemewa na ugumu wa maisha na kujitosa ktk wizi wa kijiko wakahukumiwa ilhali mabilini yamechotwa na wajanja km mnavyowaita?(4) vipi kuhusu makundi ya vijana walioamua kujitumbukiza ktk biashara haramu ili kujikwamua na ugumu wa maisha? (5)ccm ipo tayari kuwaanzisha shule wale wote ambao ugumu wa maisha ulisababisha wasipate haki yao ya msingi na sasa ni sayansi na teknolojia hawajui kusoma wala kuandika tunapoingia miaka 50 ya uhuru? (6) Nape utaweza kufika ktk maskani ya waliojiona hakuna wanachokifanya bora kulowea ktk uvutaji wa madawa ya kulevya na sasa hawana tena thamani nguvu kazi ya taifa inateketea na bado humo humo mnawaingizia madawa bila kufikiria athari zake?(7) hakuna kijana anaependa kumuona dadake au mamake akibebwa na bajaji ambyulesi kwakuwa sio salama ilhali serikali ikitetea posho na mashangigi ya kifahari kwa gharama yoyote.(8) how about bunge la viroja kupongezana kupiga makofi kupinga hoja zenye tija ubabe mabavu na miongozo ya kudhoofisha upinzani? bunge la ccm. (9)vpi kuhusu mikataba feki, elimu duni, giza, mauaji ya raia na ukimya wake, msd madawa yameharibika zahanati hazinadawa, maisha bora Je?(10) Ushauri jitahidi sana kuzima mitandao yote ili tusipate habari uwe unatutangazia media group zenye maslahi na ccm kuhusu mazuri tupu ya chama chako. Watanzania chini ya utawala wa ccm tulikuwa mtaji na zulia lenu jekundu la kukanyagia ila mwisho upo jirani.
 
NAPE NAKWAMBIA UKFANIKIWA KUWARUDISHA LISU, ZITO, MNYIKA, MDEE, MBOWE NA HATA SLAA bado hauna lugha yakunieleza juu ya uzuri wala mafanikio ya chama chako cha mfu. Npo radhi ku'join CHAUSTA nakuanzsha movt.
 
hakuna kijana aliyeshibishwa uongo ila hali halisi ya maisha inatosha kukufanya uichukie ccm(chukulia mfano yanayoendelea bungeni sasa kwa wabunge wa ccm)

maneno yenye rangi nyekundu ndo kila kitu kwanini ccm inaandamwa na shutuma za kila kona hamna haja ya kumwambia mtu ubaya wa kundule la nyani wakati akitembea tu linaoonekana ,bul shit chama cha magamba!!!

I hate ccm with all ma heart and i do regret why it do exist til this time!


"Mungu ana akili sana kumuua Nyerere mapema maana kama angekuwepo sasa na kuyashuhudia haya tuyaonayo angejiua mwenyewe kwa kujitundika"
 
Back
Top Bottom