Nape: CCM kutoa tamko juu ya katiba leo mchana

Status
Not open for further replies.

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
Source BBC Kwa mujibu wa taarifa ya habari bwana Nape Nnauye kasema atatoa tamko la chama juu ya rasimu ya katiba kwani wao kama chama tawala na wana wabunge wengi na wanauwezo wa kukaa kama kamati na kuamua wapendavyo wataamua wapi walalie juu ya katiba. Na tamko hilo lonatolewa leo mchana mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichoanza jana
 
Wasithubutu kuichakachua rasimu ya katiba hii. wakubali tu kutega kalio watulie mpaka dawa ihingie
ril tusimame pamoja kuwa kuwapinga kwa uhuni wao
 
Source BBC Kwa mujibu wa taarifa ya habari bwana Nape Nnauye kasema atatoa tamko la chama juu ya rasimu ya katiba kwani wao kama chama tawala na wana wabunge wengi na wanauwezo wa kukaa kama kamati na kuamua wapendavyo wataamua wapi walalie juu ya katiba. Na tamko hilo lonatolewa leo mchana mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichoanza jana
tutegemee tamko litakaloimaliza ccm,maana sioni kama kuna mtu wa kusoma nyakati
 
yote haya yatakawa sawa tu mda si mrefu wananchi bado nafasi yao ipo kuamua msimamo wa katiba mpya.
 
Kama wataikatalia hiyo rasimu na kuwaagiza wajumbe wao wa mabaraza waliowachakachua,basi wajue ndio watakuwa wamejimaliza kabisa!

Kwa kuwa National referendum,ndiyo itakayowapa aibu ya karne,na hapo ndipo CCM,itakapojizika rasmi,na vizazi vijavyo,vitakuwa vinaisoma tu kwenye historia,kuwa kuna enzi nchi yetu iliwahi kuwa na chama tawala=dola kilichokuwa kinaitwa CCM!!
 
Ni wakati wa CCM to provide leadership. Lazima mfumo wa sasa ubaki ili kuunusuru muungano. Dola inaweza kuwadhibiti wahuni wanaotaka kuvunja nchi. Ni kosa la uhaini kuhubiri sehemu ya kujitenga! Haikubaliki duniani kote. Washabiki wa CCM watulie mambo 'yatadhibitiwa'
 
Ninashuku juu ya kile kilichofanywa na CCM usiku wa manene kuamkia leo.Nashuku kwenye mambo makuu manne.


1. Kwanza inadaiwa kwamba kilichofanyika ni kikao cha dharura (licha ya kwamba mada kuu ilikuwa ni rasimu ya katiba).BBC wameripoti leo asubuhi kwamba Nape anasema ni kikao cha dharura.Mimi najiulidha udharura huo unasababishwa na nini? Je! rasimu imekuja kinyume kabisa na matarajio ya CCM? Kama ndivyo basi; je! nini ambacho ccm walitaraji kukiona ndani ya rasimu na sasa hawakukiona? je! kwa nini hali imekuwa tofauti na jinsi ambavyo CCM walitaraji?(kwa hili tunajifunza nini!)

2. Kwa nini kikao kinafanyika usiku wa manane! nijuavyo mimi hakuna kitu chochote kile duniani kinachofanywa na mtu mwenye akili timamu bila sababu.Je! yopo anaeweza kujua sababu?

3. Kwa nini Nape kakataa kusema kilichojadiliwa ndani ya mkutano alipohojiwa (saa nane na nusu usiku ambapo ndio kikao kiliisha) na kinyume chake akasema atatoa maelezo leo mchana? Je! Ndo kusema kuna editing au timing!

4. Je! ikiwa tume ya katiba ni tume huru na imeonesha uhuru wake; Ni nini CCM wanataka kufanya?
 
ikumbukwe awali kabla ya mchakato wa katiba kuanza; msimamo wa CCM juu ya katiba ilikuwa ni "Hatuna haja ya katiba mpya.ya sasa inatosha.Inaweza kurekebishwa kidogo tu na bunge".
 
CCM imekula kwao.
Ninahisi CCM watapinga baadhi ya mambo muhimu ya Rasimu ya katiba hii hususani Serikali tatu.
Walifanya hivyo kwenye tume ya Nyarali, tume ya jaji Kisanga nk.
Safari hii tutegemee CCM nao wakiandamana, wakigoma kama sio kusambaratika.

Chezea katiba wewe!!!
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom