Nape, CCM Kujivua Gamba Haiwezekani ila Chama kufa inawezekana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape, CCM Kujivua Gamba Haiwezekani ila Chama kufa inawezekana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jnuswe, Jun 23, 2011.

 1. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nimeona ni vyema nimpe angalizo K/mwenezi wa chama cha CCM ndugu Nape, Ni ukweli kwamba CCM ilipofikia sasa kujivua Gamba haiwezekani ila ninaloliona mbele ya chama hiki ni kifo cha mende.

  Nimesoma Gazeti la mwanahalisi tuhuma nyingi wanazorushiana waheshimiwa mbalimbali wanaowania kiti 2015 kupitia chama hicho ni dalili ya kujiangamiza kabisa. Membe against Lowasa, Uswahiba wa Lowasa , Kinana, Membe, Rostam na Sita uliokuwepo awali umegeuka kuwa wadui miongani mwao.

  Mara tunasikia Lowasa amedhamiria 2015, Sumaye asemi lolote lakini bado yumo, Sitta, Membe mwenyewe, Mwandosya japo yuko kimyakimya, Uwezi ukaacha kumzungumzia Kigoda maana alikuwa swahiba mkubwa wa Beni, na pengine bado anauchungu wa kudondoshwa na wengine wengi. Kinachoendelea sasa ni kupigana vijembe ndani ya Chama hicho. Nakumbuka Msekwa alipojaribu kumunyooshea kidole EL kuwa harakati zako za 2015 zitakiharibu chama, yeye alijibu kwani kuna dhambi kufanya hivyo au kuna mtu mumemuandaa ? Msekwa akanyamaza

  Hayo machache tu, leo hii Nape unazungumzia kujivua gamba kwa kuondoa mafisadi ndani ya chama chako wakati jambo dogo la kukijenga chama ili kitengamae limekushinda ?

  Yapo mengi yanayoonyesha chama hicho kuendelea kuwa Imara ni jambo lisilowezekanika, mtafanyeje ili CCM iaminiwe na watanzania ?
   
 2. a

  allydou JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 1,485
  Likes Received: 572
  Trophy Points: 280
  unapowaeleza ukweli magamba, unawashtua, watabadilika hawa waendelee kutusumbua, washahili walisema, ukimuasha alielala................ waache hivyo hivyo,
   
 3. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  nimekupata ,
   
 4. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Haya tena. Yule rafiki yetu (Nape) baada ya kuchemka mkakati wa kumnyanyua Lowasa toka CCM, sasa anajidai kusahau hilo na ametangaza kuwa chama chake kitaanzisha chuo kikubwa cha kufundisha itikadi ya chama kama ilivyokuwa miaka ileeee!
  Kwamba wataanzisha pia madarasa ya itikadi mikoani.
  Mtindo wa kutoa kadi za papo kwa papo utapigwa marufuku.Eti uliwaletea maumivu kwa kudhani wana w/chama wengi kumbe mamluki.
  Wanachama watapewa kadi baada ya kupata mafunzo rasmi.
  Source TBC

  My take: Bila shaka jamaa atatueleza mafanikio ya mkakati wa mwanzo kuvua gamba kabla ya kuanza mkakati No. 2
   
 5. I

  Ismaily JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu dogo anakurupuka sana,atazeeka mapema,mana ana fikra finyu na mgando,hawezi kupambana hata siku moja na LOWASSA,CHENGE,NA ROSTAM,nadhani propaganda zake na siasa zake ni za maji taka.
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Dogo mchomvu na uwezo wake wa kuwaza umefikia kikomo.Njaa sana jamaa na tamaa kibao ila hajui afanyalo.
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  kweli mafisadi wameamua kutoiachia hii nchi.. Nina uhakika hadi damu imwagike ndio wataondoka.. Hawa si ni kama komrdi Mugabe?,Museveni na wengineo wanamapinduzi..wanajua kuwa hii nchi ni yao.shule za kata wamezishindwa sasa wanakuja na mikakati ya kichama.. Sasa hizi shule zitasaidia nini kama umeme hamna na mifoleni kila kukicha?ondoeni kero kwanza kila mtu atawakubali automatically. Nawakilisha
   
 8. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  anataka kututoa kwenye mjadala aliouanzisha wa kupambana na waliomuweka rais wake ikulu,.tunakumbuka tarehe 10 julai 2011 ndio siku mliojishaua mtawapa barua mafisadi wenzenu,..mapacha watatu huwawezi labda umpe barua patel aliyekuonjesha hela ya epa..siku tisini hizooooo zinaisha,tutaona kama una ubavu,nyambaf
   
 9. M

  MVUA GAMBA Senior Member

  #9
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wana Jf Nimepata Taarifa ambazo ni za Uhakika ni Kwamba Ziara inayofanywa na Muheshimiwa Nape na Mukama kati Vyombo vya Habari hawatatembelea Kampuni ya Mwananchi,Free media na New Habari kwa Sababu zifuatazo.

  1)Mwananchi Communication inaonekana Ni kampuni ya Wakenya lakini Vile Vile ni Magazeti ambayo hayaungi Mkono Chama Cha Mapinduzi,Na kubwa Zaidi ni kwamba MCL ambao huchapisha Magazeti ya Mwananchi na Mwana Spoti,The Citizen Muhariri wake Denis Msacky anaaminika Ni Shabiki wa Chadema,kwahiyo Nape katika ushauri alilimuandikia Katibu Mkuu wa CCM kumshauri Kuwatosa katika ziara ambayo leo walikua Nipashe,kwakuwa Nape anadai Nipashe inakisaidia sana Chama Cha Mapinduzi na wanaunga Mkono Agenda ya Kuvua Gamba.

  2)Free Media nayo imetoswa kwa Hoja kwamba chombo Hiki ni cha Chadema na Hakimuungi Mkono Nape katika Harakati zake,kutokana na watu wa Karibu wa Chombo Hiki Nape amedai angelikua Muhariri Mkuu ni Bwana Martin Malela ambae ni swahiba Mkubwa wa Bwana Nape CCM wangelienda kupatembelea lakini Uwepo wa Absolom Kibanda,Hansbert Ngurumo na Kwakuwa Gazeti ni Mali ya CDM wao hawataenda kuyatembelea.

  3)New Habari amabao ni magazeti ya Mtanzania ,Rai,nao wametoswa katika ushauri uliotolewa na Nape chombo hiki hakitatembelewa na Vigogo hao wa CCM,kwanza kwasababu Magazeti haya yamebadilika sasa na yamekuwa yakiishambulia CCM na hasa Nape,lakini Gazeti la Mtanzania kwa Sasa Ndani ya Makao makuu ya CCM linaonekana sawa na Tanzania Daima,Mwananchi limekuwa likishambulia serekali na kuibeba CDM hasa limeonekana ni Gazeti linalombeba Zitto kabwe na Kauli ya Nape katika kikao cha sekretariti ya CCM wiki iliyopita alidai Uhusiano wa Hussein Bashe na Zitto kabwe umepelekea mabadiliko ya kimtazamo ya chombo hicho tangu Mwishoni mwa mwaka Jana,na hili la Gamba limepelekea Magazeti hayo kutoibeba Tena CCM

  Kwahiyo wana Jf baada ya kuzipata Usiku huu nikiwa Hapa Dom nikaona nizilete hapa Jamvini,Ziara ya Mkuu Nape imedhamiria kujenga Mahusiano na IPP,TSN,UHURUna TBC na kuwatosa MCL,Free Media na New Habari,na CCM wametoa Maelekezo wizara zote Matangazo ya Bajeti yaenda TSN,halafu Uhuru,kama kuna chombo Binafsi basi itakuwa Nipashe na Guardian vingine hawatapata. Naomba kuwasilisha.
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Nilishasahau habari za vuvuzela. Mliteta tena jamvini?
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nchi nyingine wanawekeza kwenye science & technology yeye Nape anaona fahari sana kutangaza azma ya ccm kuanzisha chuo cha kujifunza nidhamu ya woga! Hivi wale vijana wanaouza maji, viberiti, korosho barabarani watafaidikaje na hiki chuo? Hivi kinachotakiwa ni watu kujifunza itikadi au ni viongozi kuishi na kusimamia sheria?
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mwanachi linaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya readers (swahili newspapers) na kama sikosei kwa siku wana-circulate around 30,000 copies.

  Sasa kama si upungufu wa akili inakuwaje kiongozi mzima uache kujenga mahusiano na newspaper yenye readers wengi zaidi, yenye kuaminika, na yenye kusomwa na opinion makers wengi, badala yake unaenda kutembelea 'internal newsletters'. How bizarre?
   
 13. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nape hafai kabisa kupa nafasi ya kufanya kazi serikalini He is too political Sijui hata huko masasi alikuwa anafanya nini. Kweli kuna sehemu nyingine zinazarauliwa kama huyi anasema hivi do alikuwa mkuu wa wilaya mhhhhhhhh

  Atanisamehe but siku zinavyoenda ndivyo navyoona zile credit nilizompa mwanzoni hazikuwa sahihi. Anazidi kuji expose bora wangemuacha huko kijiweni masasi.

  Sasa chuo kitasaidia nini hani hata Radio uhuru ni mfano tosha kuwa ni mzigo. Karne hii Chama kianzishe chuo cha itikikadi teh teh teh
   
 14. x

  xman Senior Member

  #14
  Jun 24, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nape kuna msemo wa kiingereza unasema "keep your friends close and your enemies closer" sasa kama wewe unaamini hao mwananchi,rai,raia mwema wamewaacha c.c.m then its high time uwaweke closer uaccomplish your objectives
   
 15. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  uhuru yanasomwa ktk ofisi za wilaya, mikoa na halmashauri tu, ambapo husambazwa na kulipwa juu kwa juu, isingekuwa hivyo leo yasingekuwepo maana mtu huwezi nunua eti ukasome upupu wa nape. ebooo!
   
 16. c

  chelenje JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sina hakika kama magazeti ya uhuru na mzalendo bado yapo. Magazeti bora ya kiswahili ni Mwananchi,Mwanahalisi,Raia Mwema,Tanzania Daima.
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kazi anayoifanya Nape siyo kujenga CCM. Ni kumuingiza Mwandosya Ikulu. Basi!
   
 18. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  si kweli kwamba mwananchi ni ya wakenya...... mwananchi ni mali ya agha khan ambapo pia anamiliki magazeti na tv ya citizeni ya kenya.....
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mtanzania,rai yataendelea kua kama yalivyooooo
  pili who is NAPE BY THE WAY.......kwani asipotembelea itakuaje??????yaan haingii ubongoni kabisaaaaaa.........wanawapa ruzuku za kuendeshea hizo kampuni?????TBC FM,TBC1,TBC TAIFA ni TSN ni vyombo mama vy ccm,huku UHURU,MZALENDO NA RADIO UHURU NI VYOMBO BABA VYA CCM.......nyi ,wananchi chapeni kazi.....ndio gazeti linaloongoza kwa mujibu wa afsa masoko wa mcl......nalipenda na ntazid kulipenda na kulinunua.........
   
 20. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Yani ktk m2 mwamuluki ktk ngazi ya siasa! Hakika huyu Nape ndiyo wa kwnz. Mi nafsi yangu amenichafua NDEFU KABISA.
   
Loading...