Nape: CCM itashinda tu uchaguzi mkuu ujao hata kwa goli la mkono

Natanguliza hoja hii muhimu sana ingawa aliesema anaonenakana kituko ila kama mtaapuuzia mtajua alichokuwa anasema maanayake

wakati wa kupeana hints za.kukabiliana na goli la mkononi

mwakajana kimara mwisho kuna.mawakala walikamata mzigo wa kutosha wakakibali kubadilishwa matokeo na kupewa mshindi wa chama kimoja toka tawala

na habari nilizozipata tume ina.mpango wa kutoweka wakala yoyote kusimamia kura za chama chake..nakama n kweli basi tujiandae na hili neno la goli la mkononi..naamini wapinzani hawatakubali hii

kingine mnapojiandaa na mabadiliko .mabadiliko n kura ..n vyema watu wakahimizwa kujiandikisha kupiga kura ..nasema hivi nakumbukukia ya aliekuwa naibu wazirimkuu a.l.mrema ya kusukumwa ubungo mpaka jangwani..kwenye kura mnakumbuka yaliyotokea...
Saaafari ya matumaini nje ya chama ndio imeanza mjiandae
 
Natanguliza hoja hii muhimu sana ingawa aliesema anaonenakana kituko ila kama mtaapuuzia mtajua alichokuwa anasema maanayake

wakati wa kupeana hints za.kukabiliana na goli la mkononi

mwakajana kimara mwisho kuna.mawakala walikamata mzigo wa kutosha wakakibali kubadilishwa matokeo na kupewa mshindi wa chama kimoja toka tawala

na habari nilizozipata tume ina.mpango wa kutoweka wakala yoyote kusimamia kura za chama chake..nakama n kweli basi tujiandae na hili neno la goli la mkononi..naamini wapinzani hawatakubali hii

kingine mnapojiandaa na mabadiliko .mabadiliko n kura ..n vyema watu wakahimizwa kujiandikisha kupiga kura ..nasema hivi nakumbukukia ya aliekuwa naibu wazirimkuu a.l.mrema ya kusukumwa ubungo mpaka jangwani..kwenye kura mnakumbuka yaliyotokea...
Saaafari ya matumaini nje ya chama ndio imeanza mjiandae
hii id imeingiliwa, huyu sio pdidy original.
 
Mpwa.n pdidy origin wala sipepesi macho mb tu ndio shida....endelea na maombi kufunga kuna raha
 
"Prevention is better than cure". Sikuwahi kusikia tume ya uchaguzi, viongozi wakuu wa CCM wala vyombo vya usalama vikimkaripia wala kumhoji Mh. Nape kuhusu kauli yake ya bao la mkono aliyoitoa hivi karibuni kuhusu uchaguzi wa October 2015. Hii ni kauli nzito sana isiyopaswa kuachwa ipite hivi hivi bila kutolewa tafsiri sahihi na Nape au CCM.

Uchaguzi mkuu ni chanzo kikuu cha uvunjifu wa amani duniani, pia ni chanzo kimojawapo chenye gharama kubwa kukiandaa na kukitekeleza. Bao la mkono ni tukio kwenye mpira wa miguu ambalo linaambatana na adhabu kubwa kwa aliye na waliolifanya, na mara nyingi halimo kwenye kanuni na sheria za mpira wa miguu duniani.

Iweje Nape afananishe ushindi wa CCM wa October 2015 na bao la mkono? Nape sio kichaa na CCM inafahamu hivyo pia bila shaka kuna kitu chenye ukweli alichokidhamiria.

Kinachoshangaa Tanzania na vyama vya upinzani kuna wanasheria wengi wenye uwezo wa kumvalia njuga Nape hadi atoe ufafanuzi wa kauli yake ile ambayo ina uwezo na hadhi ya kuweza kusababisha uvunjifu wa amani kama ikitekelezwa kama alivyoitamka Nape.

Sote tunafahamu kuwa Mwenyekiti wa CCM ndo Rais na Amirijeshi mkuu wetu nchini, lakini hata yeye hakusikika akimuonya Nape kuhusu kauli yake hii.

Nashauri wanasheria wote muungane dhidi ya kauli hii ovu kwenye vyombo vya sheria na taasisi mbalimbali. Kauli hii iwasilishwe rasmi kwenye tume ya uchaguzi, vyombo vya usalama, mahakamani, jumuiya ya east africa, AU, ICC, UN, EU na Marekani ili Nape akahojiwe na kueleza alichokuwa amekimaanisha kuhusu ushindi wa bao la mkono kwenye uchaguzi.

Hii itasababisha dunia nzima ione kiashiria muhimu cha uvunjivu wa amani kwenye uchaguzi wetu ujao hivyo kujiandaa na kubaini matuo yasiyofaa kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania.

Haitoshi kulalama tu kwenye majukwaa ya siasa kuhusu kauli hii, nendeni hatua nyingine zaidi mbele. Wanasheria chukueni nafasi yenu kwenye jamii.
 
Nimekuwa nikiona goli la mkono likisababisha mpira kuwekwa kwapani na timu kutoka nje ya uwanja hiyo ni zamani....siku hizi hakuna hiyo tena,uamuzi wa refa ni wa mwisho na unatoa ushindi.
Iliyobaki wavumilie tu kama wana uwezo wasiruhusu mtu kuingia katika 18 zao.Mbona mfano wa katiba pendekezwa uko wazi....?????
 
...Nape sio kichaa na CCM inafahamu hivyo pia bila shaka kuna kitu chenye ukweli alichokidhamiria.
Nape alivua unafiki wote na akasema kitu cha kweli, kilichopo mezani kama plani ya CCM. Kama msemaji mkuu wa chama haiwezekani kumchukulia kama mtu aliyekurupuka. Tume kama refa ipo chini ya control ya serikali ya CCM kwa hiyo Nape anasema wazi kuwa Tume itawabeba.

Kwa maana nyingine pamoja na kutano kubwa la Chadema jana Mwanza ambayo ni ishara ya kukubalika, pamoja na kuwa tutawapigia kura ya ndiyo, lazima wajiandae kuwa atakayetangazwa na tume kuwa ameshinda ni Pombe Makufuli. Msibishe jamani! Nape kasema!!
 
Kushinda ccm ni ngumu maana hakuna msafi, nisawa na kutafuta bikra wodi ya wazazi wasubirio kujifungua
 
Sina shaka kwamba kwa nguvu hii ya UKAWA kufuatia ujio wa Lowassa ushindi Octoba 2015 ni dhahiri... Lakini nina wasiwasi na dhamira ovu ya CCM kufuatia kauli ya Nape kwamba CCM ni lazima itashinda na kuendelea kutawala hata kwa goli la mkono. Hii inaonesha jinsi gani CCM walivyojipanga kuiba kura na kupindua matokeo kupitia tume ya uchaguzi kwani kauli hiyo siyo ya bure na kimtokacho mtu ndicho kimjazacho. Nape na wenzie ndio wamepanga hivyo kwani hilo ndiyo goli la mkono lenyewe, kuiba kura na ama kupindua matokeo. Sasa ninajiuliza, viongozi wetu wa juu wa UKAWA wamejipangaje kuhakikisha kura haziibwi na wala matokeo hayapinduliwi na CCM wakishirikiana na usalama wa taifa bilashaka na hiyo tume ya uchaguzi?!! VIONGOZI WA UKAWA TAFADHALI, HATUTAKI KURA ZETU ZIIBIWE WALA MATOKEO KUPINDULIWA NA CCM... Vipi mmejipanga kuhakikisha hawafungi goli la mkono na wakijaribu kufanya hivyo walimwe kadi nyekundu na kutolewa nje na kufungiwa kucheza kabisaaaa?!!! Mimi ninachotaka CCM out kwanza mambo mengine baadae
 
Wadau, napenda kuwatahadharisha kuiogopa CCM kama Ukoma na kuikataa. Kauli ya Nape kuhusu goli la mkono, maana yake ni kuiba kura za Urais, Wabunge na Madiwani kwenye uchaguzi mkuu 2015. Nape kaanza na kuiba kura za maoni za Ubunge kwenye jimbo lake.
CCM JIKATENI WOTE MTUACHIE NCHI YETU.
 
Nimekaa nikajiuliza kwa kina kuwa kabla ya kuropoka ni vizuri ukajiuliza mara mbili dhidi ya kile kinachokutoka kinywani. Kauli kama Goli la Mkono hata kama haikutolewa kwa nia mbaya ni dhahiri endapo patatokea chochote cha kuvunjika kwa amani kutokana na utata wa matokea ya uchaguzi hii kauli inaweza kuchukuliwa kama kiashiria kilichochangia. Ni vema basi kila mtu akajichunga sana kauli zake hasa kipindi hiki cha lala salama. Nakumbuka kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda, moja wapo ya wahanga waliofungwa ni kutokana na kutoa kauli zenye utata.
 
Kushawishi wananchi wakae vituoni kulinda kura hilo,ni kosa la kushtakiwa ICC Wala sio kauli ya goli la mkono ,na ilitolewa Mara moja tu lkn kulinda kura ni hatari mno kwani ni kuhanasisha watu kuvunja amani ,na Siku hizi mnaitwa makamanda mnaandaliwa kwa vita ,ni hatari mno
 
Back
Top Bottom