Nape: CCM itashinda tu uchaguzi mkuu ujao hata kwa goli la mkono

Wizi wa kura tu hana la maana....nadhani mwaka huu Upinzani walinde kura zao kwa jasho na damu hadi kieleweke

Kwa dalili hizi za awali haionyeshi kama wanatafiti hata mbinu ambazo CCM huwa inatumia, ukiisha uchaguzi ndo utasikia malalamishi ya kuibiwa . you can't do the same thing the same way and expect different result.
 
Habari Jf..

Nape Nnauye Juzi akiwa Mkoani Kanda ya Ziwa aliwaambia CCM Ushindi ni Lazima hata kwa Goli la Mkono ili mradi tu Referee apulize Kipenga.

"Goli ni Goli tu Hata Kama ni la Kuotea"

Hapa Swali la Kujiuliza Je Referee wa Mechi ya CCM na UKAWA atatuvusha Salama?, Kwa Maana Team zote Zimejipanga Vilivyo na Washahabiki Safari hii Naona Hawanunuliki na Hawataki hata Jezi za BURE.

UKAWA Kazi Kwenu Sasa,Wananchi Hawatawasaidia Kulalamika na Kulialia Baada ya Mechi Kuisha Kwa Bao la Mkono wa Mungu.
hii ni nadharia ,misingi ilishabomoka hapa ni kujenga taswira ya kuwa vurugu zipo.ccm haijajenga mazingira huru ya kuruhusu mechi ichezwe ,kocha ,mshika kibendera ndio wanajua hatima ya mchezo ,kwa mazingira haya ukawa wamesikia ,wapiga kura wamesikia .
 
Nape alipokuwa Mwanza siku chache zilizopita, alitamka matamshi ya ajabu na ya kitoto sana.Ni matamshi ya kichochezi ambayo hayakupaswa kutamkwa na kiongozi wa ngazi za juu wa chama,tena chama tawala.Alisema,"CCM itashinda uchaguzi wa 2015 hata kwa bao la mkono.

"Kwa maneno haya,Nape anatufanye tuamini kwamba katika chaguzi zote zilizopita,CCM walishinda kwa hila na katika uchaguzi wa 2015,CCM itatumia hila tena ili kuhakikisha kwamba inashinda.Hata kama CCM ilishinda kwa hila,Nape hakupaswa kutamka hadharani.Alipaswa kutambua athari za matamshi yake.Kwa kutumia hila kushinda chaguzi, CCM inawatawala wananchi wa Tanzania kinyume na matakwa yao,na kwa kweli inawatawala kwa nguvu.Kwa mantiki hiyo, hakuna tofauti yeyote kati Pierre Nkurunzinza na CCM,na kwa kweli CCM haina uhalali wa kumnyooshea Nkurunzinza kidole.

Nape alipashwa kutambua kwamba maneno aliyotamka yalikuwa maneno ya kichochezi,ambayo katika serikali makini, yalipaswa kustahili adhabu kali, kwa kuwa yanaweza kuingiza nchi katika machafuko, na kwa kweli hata katika vita ya wenyewe kwa wenyewe.Kwa mshangao mkubwa, sijasikia akikemewa na chama chake.Kwa ukimya huu, sijui tuelewe nini.Kwamba katumwa na chama chake kutamka maneno yale ya kijinga?Kama chama chake hakijamtuma, wananchi tungependa kuona na kusikia akikemewa kwa nguvu zote.

Niseme wazi,kwamba wanaoitwa viongozi wetu wamepoteza kabisa mvuto kwa wananchi wanaowaongoza kwa sababu ya tabia zao zisizokubalika.Viongozi wa kitaifa wote ni lazima wawe mfano wa kuigwa na wale wanaowaongoza.Inapofika mahali kama ilivyo sasa, ambapo wanaoongozwa hawana cha kujifunza kabisa kutoka kwa viongozi wao, ni hali ya kutisha sana.Viongozi wetu wamepoteza moral authority kabisa.Sijui tunajenga taifa la namna gani,la waovu?Mungu atusaidie sana.
 
nape alipokuwa mwanza siku chache zilizopita, alitamka matamshi ya ajabu na ya kitoto sana.ni matamshi ya kichochezi ambayo hayakupaswa kutamkwa na kiongozi wa ngazi za juu wa chama,tena chama tawala.alisema,"ccm itashinda uchaguzi wa 2015 hata kwa bao la mkono."kwa maneno haya,nape anatufanye tuamini kwamba katika chaguzi zote zilizopita,ccm walishinda kwa hila na katika uchaguzi wa 2015,ccm itatumia hila tena ili kuhakikisha kwamba inashinda.hata kama ccm ilishinda kwa hila,nape hakupaswa kutamka hadharani.alipaswa kutambua athari za matamshi yake.kwa kutumia hila kushinda chaguzi, ccm inawatawala wananchi wa tanzania kinyume na matakwa yao,na kwa kweli inawatawala kwa nguvu.kwa mantiki hiyo, hakuna tofauti yeyote kati pierre nkurunzinza na ccm,na kwa kweli ccm haina uhalali wa kumnyooshea nkurunzinza kidole. Nape alipashwa kutambua kwamba maneno aliyotamka yalikuwa maneno ya kichochezi,ambayo katika serikali makini, yalipaswa kustahili adhabu kali, kwa kuwa yanaweza kuingiza nchi katika machafuko, na kwa kweli hata katika vita ya wenyewe kwa wenyewe.kwa mshangao mkubwa, sijasikia akikemewa na chama chake.kwa ukimya huu, sijui tuelewe nini.kwamba katumwa na chama chake kutamka maneno yale ya kijinga?kama chama chake hakijamtuma, wananchi tungependa kuona na kusikia akikemewa kwa nguvu zote.niseme wazi,kwamba wanaoitwa viongozi wetu wamepoteza kabisa mvuto kwa wananchi wanaowaongoza kwa sababu ya tabia zao zisizokubalika.viongozi wa kitaifa wote ni lazima wawe mfano wa kuigwa na wale wanaowaongoza.inapofika mahali kama ilivyo sasa, ambapo wanaoongozwa hawana cha kujifunza kabisa kutoka kwa viongozi wao, ni hali ya kutisha sana.viongozi wetu wamepoteza moral authority kabisa.sijui tunajenga taifa la namna gani,la waovu?mungu atusaidie sana.

tulishasema nape ni punguani lakini hatueleweki,kwa nchi zinazofahamu umuhimu wa utawala bora,leo hii angekuwa ameshafukuzwa kazi na kufunguliwa mashitaka,lakini hapa kwetu ni maneno ya kawaida sana
 
ImageUploadedByJamiiForums1435649183.486729.jpg
Wanachokifanya CCM na mawakala wake kuhujumu uchaguzi mkuu si halali na haikubaliki hata kidogo. Haya ni moja tu ya madhara ya kutokua na tume huru katika chaguzi zetu. Au ndiyo maandalizi ya goli la mkono?!
 
Ni hatariii! kuna watu wanatia shaka juu ya hawa waandikishaji, inasemekana wametokana na makada , utaratibu wa kuwapata ulikua tofauti sana na miaka mingine
 
Ndugu wadau, kama mjuavyo goli la mkono ni goli haramu zaidi katika mchezo!
Sasa mimi nawaza kauli ya Nape kuwa ccm itashinda hata kwa goli la mkono. Ccm ile ambayo zamani ilikuwa inashinda kipindi cha kwanza cha mchezo, leo inategemea goli la mkono ndyo ishinde? Tutafakari kauli ya Bw. Nape
 
Wanajua hawapendwi hawana sera, hawana nguvu ya hoja na pia ahadi za chungu nzima hakuna hata moja waliyoitimiza si maisha bora kwa kila Mtanzania, ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya, Big results now, Kilimo kwanza n.k. pia na wizi, upokeaji rushwa, ufujaji wa pesa za walipa kodi, ufisadi na ujangili uliokithiri. Ndiyo sababu wakaaamua kufanya kila wawezalo ili kuchakachua maoni yote ya katiba toka kwa Wananchi kwa kujua fika katiba ile kama ingepatikana ndio ingekuwa kaburi lao baada ya kuhamishwa toka ICU na kuzikwa rasmi ndani ya kaburi lao. Wote ndani ya chama chao cha mafisadi wanalijua hilo kwamba uchaguzi huru na wa haki kamwe hawawezi kushinda, ni lazima watumie hila na mbinu mbali mbali za udanganyifu ikiwemo kutumia vyombo vya dola na hata tume ya uchaguzi ili waweze kutimiza lengo lao la kubaki madarakani milele.

Ndugu wadau, kama mjuavyo goli la mkono ni goli haramu zaidi katika mchezo!
Sasa mimi nawaza kauli ya Nape kuwa ccm itashinda hata kwa goli la mkono. Ccm ile ambayo zamani ilikuwa inashinda kipindi cha kwanza cha mchezo, leo inategemea goli la mkono ndyo ishinde? Tutafakari kauli ya Bw. Nape
 
Magoli ya mkono ya CCM yako mengi hata uandishaji wa wapiga kura kwa BVR ni goli la mkono,kuteka mkakati wa kupata katiba mpya,ni goli la mkono,kuongeza bei za mafuta ni goli ya mkono,msururu wa watangaza nia ni goli la mkono,elimu duni kwa watanzania ni goli la mkono,kuchakachua kilimo ni goli la mkono,ESCROW nk.nk.List ni ndefu mno. Nape anayajua yote haya.Alibwata kama msukule bila kujijua, na nadhani kama ni timamu anajutia matamshi yake.
Ndugu wadau, kama mjuavyo goli la mkono ni goli haramu zaidi katika mchezo!
Sasa mimi nawaza kauli ya Nape kuwa ccm itashinda hata kwa goli la mkono. Ccm ile ambayo zamani ilikuwa inashinda kipindi cha kwanza cha mchezo, leo inategemea goli la mkono ndyo ishinde? Tutafakari kauli ya Bw. Nape
 
Hivi karibuni katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha majambaz(ccm) akiwa kwny ziara ya chama hicho alitamka kuwa hata kwa goli la mkono watashinda. Tafsiri yake ni kwamba hata kwa njia zisizo halali na zenye hila watashinda tu. Kwa wapenda futiboli goli la mkono haliruhusiwi kulingana na kanuni za mchezo huo. Sasa sijui magoli ya mkono yanaruhusiwa kwny uchaguzi wa raisi wa nchi na wabunge kwenye nchi kama hii ambayo ipo nyuma kiuchumi, huduma za afya, elimu na maji. Kauli kama hiyo aliwahi kuitoa aliekuwa mbunge wa Mbeya mjini kupitia ccm bwana Mpesya ambae kwa sasa na mkuu wa wilaya ya kahama. Kauli hiyo ya goli la mkono iliwaboa wana Mbeya na kuamua kufanya maamuz magumu na kuamua kumpiga chin na kumpitisha jembe lao Mh. Joseph Mbilhnyi kupitia chadema. Nitoe wito kwa watanzania wenzangu hasa vijana kujitokeza kwa wing kwenda kupiga kura tar 25 oct na kufanya mabadiliko katika nch yako. Imefika wakat watanzania wamecho na ufisadi, elimu mbovu, huduma mbaya za afya na maji. Goli la mkono mtaji kwa UKAWA.
 
Kwa matamshi yale nilimpenda Nape kwa kuwa hakuonesha unafiki. Alisema ukweli wa moyoni na wa mikakati, tena ukweli mtupu! Golo la mkono ni option iliyo mezani! Plani zingine zikigoma, hiyo lazima itekelezwe kwa kuwa ushindi kwa CCM ni lazima!!!
 
Mipango ya njama za ushindi katika chaguzi mbalimbali"goli la mkono"ambayo huwa mnafunga wenzenu litawakuta ndani ya Ccm au Mkiingia Upinzani.Kwa kuwa mmeshiriki kupanda hiyo mbegu mtakuwa wakali sana maana mnajua goli la mkono namna linavyofungwa.CCM mnajisahau mnadhani kuwa Wapinzani sio Watanzania.Ona Wale Waliokuwa Ccm wakahamia Upinzani walivyopata taabu kushinda ubunge kama yule Wa Chadema Pale SEGEREA nk,jinsi Makongoro Nyerere Alivyopigwa zengwe ndani ya CCM hadi kuhamia NCCR.Sasa zamu ya Lowasa na huyu alikandamiza sana upinzani hasa jimboni kwake na anaelewa namna magoli yanavyofugwa na hadi sasa kafungwa moja na atapigwa lingine la mkono japo naye anacheza kwa mikono.
Nakupa pole Lowasa kwa kuwa Umefanywa ngazi ya kukamilisha ndoto za wenzako,ulitumia mbinu hizohizo kumfikisha JK.Wewe so wawa kwanza Jaramongi Odinga alifanya hivyo kwa Kenyatta,Laila alifanya hivyo kwa raising aliyepita.Kwahiyo kizazi chako chote kitakuwa ngazi.
 
Haueleweki, weka vizuri hoja yako. Wapo humu wataalamu wa kudadavua maswala ya nyanja zote
 
dah!,siku hz za jana leo na kesho ni mbaya sana kwa baadh ya watu,na hlo ndiyo kosa la sisi tulio wengi kwenda na matokeo
 
JF rudisheni accessibility ya JF kwa guest? Kwa nini muda huu tu?, mbona siku zingine access ipo?
 
Back
Top Bottom