Nape: CCM ikiendelea hivi wananchi hawatairudisha madarakani

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Nape Nnauye amesema serikali ilipoingia madarakani iliongeza mapato, kupunguza matumizi yasiayo ya lazima na tunaambiwa uchumi unakua kwa asilimia 7.2 lakini haya hayatakua na maana kama hayatatafsiriwa kwenye kuboresha huduma za jamii hasa maji
Amesema tunatakiwa tuone matokeo ya hatua hizi kwenye maboresho ya huduma za kijamii hasa maji la sivyo hazina maana
Amesema bajeti iliyopita imetengwa bilioni 900 na bajeti hii bilioni 600 hapo watanzania hawawezi kuilewa na ukuaji wa uchumi hauwezi kubaki kwenye makaratasi
Amesema ilani ya CCM ndio mkataba kati ya CCM na wananchi na wasiposhughulikia kama walivyoahidi basi wananchi hawatawarudisha

Anachosema ni kweli......kukua kwa uchumi kuendane na hali halisi ya maisha, binafsi nimeanza kilimo hivi karibuni so muda mwingi nakuwa huko kijijini kwangu, hali sio nzuri wakuu......tunaongea sana huku kwenye mitandao tukitetea na kuongea mambo yasiyo na tija kwa Taifa, ila hali halisi ya Mtanzania ipo huko vijijini......nakubaliana na Nape, kukua kwa uchumi kumfikie na Mwananchi wa kawaida, hasa mkulima.
 
PENAAAA.jpg

Mbunge wa Mtama ambaye pia alishawahi kuwa Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye ameliambia Bunge kuwa katika ilani ya CCM wakati wa uchaguzi waliwaahidi wananchi kuwa watatatua changamoto za maji lakini hadi sasa bado hatua stahiki hazijachukuliwa hivyo endapo tatizo halitoangaliwa na kutatuliwa CCM ijue wananchi hawatairudisha tena madarakani.

Full video ya mchango wa Nape Nnauye nimekuwekea hapa chini tayari…
 
Ni kweli mkataba kati ya CCM na wananchi ni Ilani...Hakuna shaka kuwa CCM itapimwa kwa utekelezaji wa Ilani.

Bungeni ndio mahala swadakta pa kuongelea changamoto za utekelezaji wa ilani ya ccm.
Uzuri wa CCM hairukii matukio bali inafanya yale yaliyoko kwenye mpango wa kitaifa wa muda mfupi na mrefu.

Swali Kwa Nape...Je bei ya Korosho ni sh. ngapi pale jimboni mtama?na ilikuwa sh ngapi hapo awali?

TUTAFIKA BILA SHAKA...[HASHTAG]#HAPAKAZITU[/HASHTAG]
 
Nape Nnauye amesema serikali ilipoingia madarakani iliongeza mapato, kupunguza matumizi yasiayo ya lazima na tunaambiwa uchumi unakua kwa asilimia 7.2 lakini haya hayatakua na maana kama hayatatafsiriwa kwenye kuboresha huduma za jamii hasa maji
Amesema tunatakiwa tuone matokeo ya hatua hizi kwenye maboresho ya huduma za kijamii hasa maji la sivyo hazina maana
Amesema bajeti iliyopita imetengwa bilioni 900 na bajeti hii bilioni 600 hapo watanzania hawawezi kuilewa na ukuaji wa uchumi hauwezi kubaki kwenye makaratasi
Amesema ilani ya CCM ndio mkataba kati ya CCM na wananchi na wasiposhughulikia kama walivyoahidi basi wananchi hawatawarudisha

Angekua WAZIRI angeongelea wapi?
Ukitaka kuwasemea wananchi BAKI NA UBUNGE WAKO.
Jana hata mzee wa Kolomije Sir Kitwanga ameongea
 
Anachosema ni kweli......kukua kwa uchumi kuendane na hali halisi ya maisha, binafsi nimeanza kilimo hivi karibuni so muda mwingi nakuwa huko kijijini kwangu, hali sio nzuri wakuu......tunaongea sana huku kwenye mitandao tukitetea na kuongea mambo yasiyo na tija kwa Taifa, ila hali halisi ya Mtanzania ipo huko vijijini......nakubaliana na Nape, kukua kwa uchumi kumfikie na Mwananchi wa kawaida, hasa mkulima.
Ila wakisema wananchi wa kawaida wanaambiwa WAACHR KULALAMIKA,WAFANYE KAZI.
NAPE SI mtu wa kwanza kubeza takwim za uchumi,even Jamaa Pale Mjini in 2o15 alikebehi hizi habar za uchumi kukua while watu maskini
 
Ka ongea ukweli kama uri ahidi na uja tenda unapewaje nafasi tena kiukweli ccm uchaguzi ujao mtashinda kupitia tume na si kwa kura za wanachi na jua ata wenyewe mnajua hilo kutoka mioyoni mwenu
 
Ni kweli mkataba kati ya CCM na wananchi ni Ilani...Hakuna shaka kuwa CCM itapimwa kwa utekelezaji wa Ilani.

Bungeni ndio mahala swadakta pa kuongelea changamoto za utekelezaji wa ilani ya ccm.
Uzuri wa CCM hairukii matukio bali inafanya yale yaliyoko kwenye mpango wa kitaifa wa muda mfupi na mrefu.

Swali Kwa Nape...Je bei ya Korosho ni sh. ngapi pale jimboni mtama?na ilikuwa sh ngapi hapo awali?

TUTAFIKA BILA SHAKA...[HASHTAG]#HAPAKAZITU[/HASHTAG]
nape akikujibu naomba uni PM
 
Back
Top Bottom