Nape: Ben Saanane amepotea, Clouds wamevamiwa, akina Roma wametekwa, Rais achukue hatua

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,227
5,270
Leo aliyekuwa waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo pia mbunge wa Mtama, Nape Nnauye anaongea na wananchi wa jimbo lake la Mtama. Amedai ataongea mengi ambayo hakuweza kuyaongea mjini Dar baada ya kutokea vurugu, kuwa nasi tukujuze yatakayojiri.
=========



Nape: Kwanza niseme nawapenda sana, nawashukuru sana kwa mapokezi makubwa mliyonipa, Kilichinitoa machozi ni heshma kubwa mliyonipa kina mama. Mlilala chini, mkataka nipite juu yenu, sio jambo ambalo nilitegemea, nawashukuru sana. Niwaahidi nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote, kuwatumikieni, usiku na mchana, ntaikumbuka heshima mliyonipa na hio itanisukumu.

Mmenipa heshima kubwa mpaka ntaenda nayo kaburini, pengine sikustahili, upendo wenu umegusa sana moyo wangu. Ntatumia mpaka senti yangu ya mwisho kuhakikisha jimbo la Mtama lina maisha bora. Niwashukuru Steve Nyerere na kundi lake, waandishi wa habari leo wote wamekuja Mtama.

Nilitaka kuongea Dar es Salaam, ikatokea fujo kidogo, Nimeamua kuja nyumbani na leo nitasema.

Mimi ni mtoto wa Kimakonde na nimefundishwa kusema kweli, nimshukuru Rais ambae nilipigana kufa na kupona kuhakikisha anakuwa Rais, nilipata ajali mabya usiku wa manane wakati natoka kutafuta kura. Watanzania wakatupa dhamana na nikapata heshma ya kuwa kwenye baraza la mawaziri moja kwa moja bila kuwa naibu waziri.

Sina mashaka kuwa nilifanya kazi nzuri kwa akili yangu yote kuhakikisha dhamana niliyopewa nameifanyia haki, kama yupo anadhani sikutenda haki asimame hadaharani. Wakati nateuliwa hakukuwa na majadiliano.

Karatasi ukiisoma haina sababu, yalikuwa ni mabadiliko ya kawaida kulingana na Rais. Wakati mwingine ukiwa na mchezaji mahiri na mkafunga magoli ya kutosha, mnampumzisha akacheze tena kesho.

Siku nne au tano kabla ya mabadiliko nilisema mambo kama hayaendi sawa mimi ntajiuzulu. Nilisema kazi hii ngumu na ikithibitika amevamia kituo cha habari, mimi waziri sitatakiwa kubaki madarakani, watu tunatakiwa kuishi kwenye maneno yetu, mimi no mtoto wa mzee Nnauye, ukifika mahali usiyombishwe na cheo.

Kocha ameamua, hakuna sababu ya kumnunia, mechi ikikamata ntarudishwa uwanjani, mimi ni mchezaji bora.

Kwenye sakata hilo kuna mambo ya kipuuzi, haya nitasema. Nikiwa njiani kurudi kutoka Arusha, kuna watu walisema kwenye mitandao Nape amekamatwa, baada ya kukanusha wakaenda kuwaondoa waandishi wa habari hoteleni.

Nilipofika nikakuta waandishi wa habari wamefukuzwa hotelini kwa ubabe, wakaenda nje na mwenye hoteli abaki na hoteli yake. Wakamwaga vijana wengi, nikisema vijana mnawajua. Mimi ninajua, nimekaa miaka 16 ndani ya CCM na nilijua kilichokua kinaendelea na bahati nzuri wanahabari wakaonyesha lile tukio live.

Nilivyofika nikawaona wale vijana, yule kijana mliemuona mpuuzi, akasogea karibu yangu, nikamnong'oneza tuko moja kwa moja vyombo vinaangalia, nikafikiri wana akili, nilisema kulinda sura ya nchi yangu, vyombo vya Dola na Rais wangu. Nilikuwa nasitiri nchi yangu, mpuuzi haoni, nikamwambia niliyonayo ni kubwa kuliko yako, sema nikaona wote tutakuwa wapuuzi.

Nikaingia ndani ya gari na kutoka juu ili aje, ilihitaji busara na nikiwaambia sina nia mbaya. Sikuwa na haja kuharibu kazi ya mikono yangu mwenyewe.

Hivi nani aliweka mguu, Edward asiende mbele? Wao walikuwa kwenye meza ndefu wanakunywa bia wakati wengine tunatafuta kura ndio maana nilikasirika na naamini mtanisamehe kwa kukasirika kwango, mimi ni banadaamu na nina nyongo, nilikumbuka mengi sana.

Kitenndo kilichofanyika hakikuwa cha kiungwana na namshukuru waziri wa mambo ya ndani kusema sina rekodi ya uhalifu.

Nilisubiri wamtafute, na wanasema sio polisi, leo nyoosha bastola hewani uone kama polisi hawajaondoka na wewe na pale alikuwepo RPC.

Siamini kama alitumwa kuonyesha silaha, mimi ukinitolea silaha naoa kama mic tu. Shida niliyonayo huyu jambazi alietoa silaha, vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya nae nini. Kama wameweza kumfanyia Nape, watanzania wangapi watafanyiwa huku mitaani. Vingenevyo wataonewa wengi, naamini wako wengi wametolewa huko, Kijana mmoja wa CHADEMA, Ben Saanane amepotea kwa miezi mingi, watu wamevamia kituo na wameonekana, tusema alieonekana sie yeye, nani alieagiza mtu akiwa na vyombo vya ulinzi na usalama kuvamia studio. Matukio haya yanawafanya watu waishi kwa hofu

Dar imevamiwa studio akiwemo Roma Mkatoliki, sikwenda CCM kwa sababu mzee Nnauye yuko CCM, nilienda CCM kwa sababu ya imani ilikuwa CCM, sema kweli fitna kwangu mwiko.

Kazi ya msingi ya kikatiba ya serikali, ni kulinda raia na mali zao, ombi langu kwa serikali na Rais aunde tume huru iyachunguze matendo haya ili yasijirudie tena. Mimi nimewasemehe ila haya matendo mengine, yanamjengea chuki yeye(Rais) na wananchi kwa sababu wanadhani ni yeye ndie anaewatuma.

Matendo haya yanachonganisha CCM na wananchi, huko mtaani watu wanasema, namshauri kama mwenyekiti wa chama changu, watu wachche wanaotumia mamlaka waliyopewa kuumiza watu, lazima tume iiundwe.
 
Nape analia na kufutwa machozi na wanawake waliomzunguka akiwa amekaa.

Rangi za njano na kijani kila kona, kama kawa.

Haya nimesikiliza mwanzo hadi mwisho kupitia Periscope

Kwa kweli Raisi hakukosea kumsimamisha kazi. Nape ana hasira sana naye tho ametumia ujanja kuficha kwa kumsifia ila haijafanya kazi kabisaaa kwa mtu ukingalia nje ya box juu ya maneno aliyotamka leo. Tena amejaa hasira sana sana kama vile CCM ni chama chake, amesema juu ya kufanya kazi kuteseka, anasahau alikuwa ameajiriwa na kulipwa mshahara.

Ana hasira sana sana kufikia kuanza kumuomba Raisi aunde tume, huku akiita viongozi wapuuzi haswa RC anamuita mpuuzi na kusema yeye mmakonde na RC mtoto wa juzi kaingia hajakipigania chama na anapata niseme hiyo kazi.

Nape ameonyesha hasira na chuki kubwa sana juu ya RC Makonda, yaaninile alisema Raisi kuwa vita ya madawa ya kulevya italeta mengi basi Nape kaonyesha hayo leo bila hata kuficha. Na hasira sana kama vile Chama ni cha familia yake. Amesikitisha sana maneno yake leo, yaani ni kama ameitisha mkutano kufanya kampeni, hivi kweli mtu tangy achaguliwe 2015 ndio leo anaenda kuongea nao, na kuhahidi mengi. Hapo ameipondea serikali kuwa haijafanya kitu Mtama na hawana cha kufanya bali yeye atatumia pesa zake na ahadi anazozidu kuwapa..kampeni fulani hivi amefanya leo. Haya ameyaongea hayo anamdanganya nani huku wanapewa ma milioni hadi sasa jama 70m sijui kwa mwaka or ( rudi kule JPM alipomshushua yule wa CUF juu ya pesa wanazopokea wabunge kuwasaidia) ajili ya amendeleo jimboni.

Nape ameonyesha kuwa ni kweli yupo na kuongea haya yote kwasababu ya maslahi yake binafsi na wenzake anayewajua yeye hawataki hii serikali kabisaaaa. Huwezi kusifia chama na kuponda serikali huku ni serikali ya chama chako. Kasema 2015 alipiga bao la mkono na 2020 hafikirii itakuwa hivyo ni kama kuna kugeuka au kuanzisha majanga huko ndani ya CCM ili kumuondia Raisi. In short Nape ni jarari kwa Chama na anavuruga leo ameongea kuchafua chama na serikali haswa.

Nape alipoomba Raisi aunde timu..akakumbuka kusema hana matatizo nae ila akasema na Mola atawapiga yao baadae wote hao...maneno siyakumbuki yalivyokuwa ila ni kwamba hao wote serijalini na JPM watapigwa bakola...halafu akaendelea kumuomba aunde tume ili akuondoe Makonda kazini.

Amemuita JPM ni kocha aliyemuweka kando kupisha mwingine, na kuwa ikipatikana cha yeye kufanya atarudi na atakuwa amepumzika na ana nguvu zaidi.ila hapo hapo baadae anaipondea serikali live bila aibu kabusa na huku kwingine anajibaraguza kwa kumpondea JPM hata kusema jinsibhaogopi hao viongozi wa Juu na wote as sasa anapata nguvu ya kupambana ndani ya chama humo humo hadi kieleweke.

Nape ana hasira sana, Nape ameguswa na maslahi yake binafsi anaisoma namba hadi amezidi kutoka nje ya pango na kwenda mbali.

Sikumshangaa kwa sababu alianza zamani kupinga ya serikali, ila Nape anamsifia sana Mwigulu nafikiri wapo pamoja.

Kamuongelea Lowassa jinsi wanavyopigiana simu etc. Kasema vyama vyote vifanye kazi pamoja. Nape ana hasira ya kuachishwa kazi kwa sabbau ambazo hakuweza kuzitaja, kapondea kuchaguliwa kuwa waziri bila kuulizwa na kutoka hata sababu haikuwekwa ila ameshindwa kuipondea na kumuuliza Raisi ampe majibu ya why tho aliambiwa na hataki kusema ana yake aligundulika.

Nape ametia aibu leo chama chake na anampango ambao sio mzuri kwa JPM ndani ya chama hicho. Ana mblackmail Raisi kuwa asiposhughulikia kumuondoa RC basi nchi itakuwa mbaya zaidi. Nape anataka Makonda aachishwe kazi lile lile alitaka kufanya tangu siku ile ya issue ya clouds.

Naoe anamchukia Makonda kwa sababu anaona ana cheo na kuwa hakufanya kazi kuinua CCM, inamuuma sana na kuwa Raisi anawashauri na anasikiliza hao wabaya na awaondoe.

Nape leo kachemka


Kaongea sana sana majanga mengi, tabu ni kajicholesha kwa kuonyesha hasira zimejaa za kuondolewa kwenye uwaziri na kumchukia Makonda na pia JPM huku akijaribu kuonyesha sivyo. Amejiuma ametoa picha mbaya na hatari.

Anaongea huku kama matukio yalivyojpanga ya kuteka ana sema yataanza kufanyika, hivyo akuondoe wa ulinzi hapo Dar. Cha kujiuliza mbina majambazi haswa dar wanavamia nyumba za watu na kuuwa hajawahi liongelea hili, kweli watu anasema wataanza kuogopa kutembea eti watatekwa na hivyo Raisi amuondoe RC wakati yeye anajua majambazi wapobna watu huwa wanatekwa bali hao wa habari aliowasimami hakutaka wayaongelee ili isichafue chama.

In short Nape pumzika na acha kuichafua serikali huko Mtama, jibadili kabisa na haufai kuwepo katika viongozi wa nchi una yako na hasira. Hao wanaokutuma na mnaokula wote mjue JPM anawajua ma atayapata tu.

Siamini ulifikiri uwaziri ni wako milele

Anataka tume na kurudia yale yale ya kuhukumu na yeye ndio anasema hukumu iweje kwa mtu anayetaka aondolewe, anajua ripoti wataweza kuichakachua na kujazia uongo ili kiongozi jembe atolewe...huu no ujanja mwingine wanataka kuutumia kumfukuzisha RC kazi as ananyoosha haswa haswa na JPM hawampendi pia kwa sana sana.

Nimechoka kuandikaaaaaa ni mengiiii
 
Naomba kuwakumbusha kuwa leo Mhe. Nape anahutubia mkutano wa hadhara jimboni kwake Mtama. Ninaomba waliopo Mtama watupe updates. Mods mnaweza kuubadilisha uzi huu uwe wa kupeana updates kwa yeyote aliyepo huko Mtama.
 
Kuna watu wanapenda umbea wametega masikio huko wakitarajia ataongea vibaya. Yule ni kiongozi haweze kuropoka hivyo yale mnayotamani mumuwekee maneno mdomoni aongee hayo ili muyaandike kwenye magazeti na mitandao muweze kuuza hayatajitokeza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom