Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

CCM imesema imesikitishwa na iliouita usanii mkubwa unaofanywa na Chadema, kuwahadaa Watanzania kwa kufanya harambee kwa lengo la kuhalalisha mabilioni ya chama hicho yanayodaiwa kutolewa na wafadhali kutoka mataifa tajiri duniani.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliyasema hayo leo, Agosti 12, 2012, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijijni Dar es salaam.

“Itakumbukwa mara kadhaa Chadema wamekuwa wakiitisha harambee za kisanii kwa kujaribu kuwahadaa baadhi ya Watanzania kwa kuwaomba wakichangie chama hicho huku viongozi wa chama hicho wakijua kuwa tayari wameshapata mabilioni toka kwa wafadhili wao. Mfano mzuri wa usanii huu ni juzi siku ya Jumamosi, Agosti 10, 2012, kwenye hoteli ya Serena ambapo walifanyika kiini macho cha harambee na kurushwa moja kwa moja na kituo kimoja cha televisheni." alisema Nape.

Alisema ,umekuwa ni utamaduni wa Chadema kuhadaa watu kwa kuitisha harambee za kisanii kina wanapokuwa wameshapewa mabilioni ya fedha na wafadhili wao, ili mradi wahalalishe kuwa fedha wanazotumia zimetokana na michango ya watanzania wakati si kweli.

Nape alisisitiza kuwa CCM wanao ushahidi kuhusu zinakotoka fedha na mikataba wanayoingia Chadema na wafadhili hao na kudai kuwa kama hawatasema wenyewe basi yeye (Nape) ipo siku atawasaidia kwa kutaja wafadhili hao na kuanika hadarani mikataba hiyo.

“Tunao ushahidi wa kutosha unaoonyesha mabilioni waliyopewa Chadema juzi na wafadhili kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuendeleza operesheni zao mbalimbali nchini. Cha kushangaza badala ya kuwaambia wanachama wao na Watanzania kwa jumla mikataba na wanakoyapata mabilioni haya, wanawahadaa kwa kuwachangisha na kugeuza mapato hayo mtaji wa baadhi ya watu binafsi ndani ya chama”, Alisema Nape

Nape alidai kwamba, siri kubwa inayofichwa kuhusu mikataba na mabilioni wanayopewa Chadema ni kwa sababu wanaotoa fedha hizo wana ajenda ya kunyemelea rasilimali za nchi hii zinazoanza kuonyesha matumaini ya kuwepo kwa wingi ili wapate kizikwapua kwa urahisi kupitia mgongo wa chama hicho.

"Kwanini mabilioni hayo yanatolewa kwa Chadema wakati huu ambapo sasa Tanzania imo katika kufanya utafiti na ugunduzi wa rasilimali mbalimbali zikiwamo gesi na mafuta? Na Je ufadhili huu kwa Chadema licha ya kufichwa sana na kufanywa siri, una nia njema kwa nchi yetu na rasilimali za nchi yetu? Kwanini ufadhili huu wa mabilioni unafanywa siri ya watu wachache hata ndani ya chama chenyewe?", Nape alihoji.

Alisema, hatua hiyo ya Chadema itaitumbukiza Tanzania katika machafuko yasiyoisha, kama ambavyo inashuhudiwa katika baadhi ya nchi zenye rasilimali kama madini ambako nchi zenye utajiri wa fedha zilijipenyeza kupitia walioitwa wapambanaji wa uhuru na haki katika nchi hizo na hadi sasa hakuna amani.

"Migogoro mingi tunayoshuhudia hasa katika nchi zinazoendelea pamoja na kuwepo sababu zingine lakini moja ya chanzo kikubwa ni uwepo wa utajiri wa rasilimali mbalimbali ambapo mataifa makubwa huzitamani na njia pekee ya kuzipata kwa urahisi ni kuchochea migogoro ya ndani na hivyo kuwa rahisi kupora rasilimali hizo wakati wenye nchi wanahangaika katika migogoro na kuachwa wakiwa masikini wa kutupwa huku waadhirika wakubwa wa migogoro na vita hivi vikiwanufaisha wakubwa.” Alisema Nape.

Nape alitoa mwito kwa Watanzania kuwa ni muhimu macho na ulaghai huo wa Chadema na wafadhili wao na kukitaka chama hicho na wafadhili wao kama kweli wana nia njema na Tanzania, waweke wazi mashariti ya ufadhili huo wa mabilioni ya fedha ili Watanzania wote wajue kama yana manufaa kwao au la hasa ikizingatiwa kuwa vyama vya siasa hapa nchini vinaendeshwa kwa fedha za walipa kodi, hivyo Watanzania wana haki ya kujua.

Pamoja na kuwataka kuweka wazi mashariti yanayoambatana na mabilioni hayo Nape aliwataka Chadema waseme hadharani wenyewe kwamba wamepewa mabilioni hayo, na kuwataka waache mara moja kuwahadaa Watanzania na kujaribu kujipachika kuwa ni Chama cha wanyonge kinachotegemea kujiendesha kwa michango ya watanzania huku wakiendelea kuchukua mabilioni kwa siri kutoka nje.

“ Wasipowaeleza watanzania ukweli , tutawasidia kuwaeleza watanzania ukweli wa kiasi halisi cha mabilioni haya, walikozitoa na mikataba waliyoingia. Lengo la hili ni kuhakikisha kuwa nchi yetu haiwekwi rehani kwa uroho wa madaraka wa baadhi ya wana siasa.” Nape alisema.

Nape akawaasa wanasiasa, kuendesha siasa za nchi kwa kuzingatia uzalendo na kukwepa kudumbukia kwenye tamaa za madaraka kujisahau na kuwa tayari hata kuweka nchi rehani, hasa kipindi hichi ambapo ugunduzi wa rasilimali mbali mbali hasa madini, gesi na mafuta vikiwa vinashika kasi nchini na kwamba ugunduzi huo uwe baraka kwa nchi badala ya laana na kuwa chanzo cha kuiuza nchi.

SOURCE : Mjengwa blog.

My take, kama kweli kuna hao wafadhili nadhani wangekipa chama kilichopo madarakani ili kiweze kujiimarisha na kutengeneza mikataba yenye masharti magumu kuvunjwa hata kama kitaondoka mararakani.
 
Nape naye analalamika!!
kweli hali si nzuri ndani ya CCM, kuna kila dalili kwamba Nape atabaki mwenyewe ndani ya CCM, haya maji yamezidi unga.
 
Eti ccm hawaitafuni nchi wala hawana nia ya kujitafutia utajiri, KAGODA, DOWANS, RICHMOND, KIWIRA, SAMAKI WA KINANA (MAGUFULI) LOLIONDO GAME CONTROL....
 
Nape bwana, yani rasilimali zote tulizo nazo CCM wameshindwa jinsi ya kuzitungia sera ili zinufaishe nchi, kama haitoshi ccm wameshiriki kuziiba mchana kweupe, wameuza mpaka ardhi kwa waarabu halafu leo anasema CDM wanataka kuuza nchi. Aanze kwanza kudai rasilimali zinazoibwa kuanzia madini mpaka wale wanyama 400.
 
Vuvuzela nape, mpaka sasa wananchi wanauwawa hovyo huko Nyamongo, bila kufaidi rasilimali zao, Huko Longido nyumba zimechomwa moto kumpisha mwekezaji wa kiarabu. Amesahau Mirerani ni watanzania wangapi wanakufa? hivi amesahau wale waliofukiwa buzwagi? ni udhalimu gani unaoendeleahuko Selous? Hayaoni au yote hayo wanafanya CHADEMA?
 
Your take is not logical mkuu, hebu fafanua jinsi chama tawala wanavyopata misaada kutoka sehemu mbali mbali achilia mbali zile loopholes zinazofanya nchi isiweze kukusanya fedha nyingi kwa ajili ya kuhudumia watu wake.
 
carolite at work

nakubalina nawe mdau cream ya carolite ni mbaya, ndo maana zimepigwa marufuku , sababu zinaharibu akili.Ni jambo la kuhuzunisha kiongozi mkubwa , tena wa chama tawala mwenye cheo nyeti cha itikadi cha kutoa na kutetea mwelekeo wa chama, anakosa utulivu, badala yake anakuwa mropokaji, inatia shaka.Nashindwa kuelewa kwa chama chenye kujivunia mtaji wa wanachama kibao, hakuna mtu mweledi, mwadilifu, msomi , mzoefu na mtaaluma wa siasa kuliko NAPE?je chama kinasababu gani kumwacha akiue huku chama kinaitwa dume?propagada anzozitoa NAPE ni za kizamani sana, katika karne na muda huu, hazitumiki tena.
Uchambuzi na hoja anzozitoa hazina mashiko, mfano;"chadema kupokea pesa kutoka kwa wafadhiri nje na uhusiano wa kuruhusu kupora rasilimali"kwa uzoefu TANZANIA tuna kitengo cha chakuchuguza fedha chafu,inayoingizwa hapa nchini, kwa wamemruhusu kuwa msemaji wao?na je wao wamesemaje kuhusu fedha hizo?na pia kuhusu rasilimali, nani mdhibiti na msimamizi wa rasilimali hizo ?je ni lini chadema wamepata kibali kusimamia na kutoa idhini ya uporaji?serikali kwa kutumia sheria na sera kuhusu rasilimali ndo msimamizi mkuu wa rasilimali, je NAPE anajua mgawanyo huu?kivipi CDM ikurupuke kwenda kusaini mikataba ya kupewa fedha kwa misingi ya kuruhusu kuporwa rasilimali wakati , utekelezwaji wake lazima ufuate sheria, taratibu, na kanuni;je ikifikia hatua hiyo, je vyombo vya dola havitajua na kuzuaia?je je serikali itakubali ikae kimya?huyu nape aache kutapatapa, huu mziki wa M4C unatisha ,na hasa kwa yeye ambaye hana mkakati wa kuyafanya hayo.Mtu mjinga ni kumwacha aropoke, mpaka achoke.Ujinga wake yeye anajua carolite tu.hata hivyo kama CDM imepata wafadhili si dhambi, hata ccm inao wafadhili wengi tu,hoja ya msingi propagada chafu zisizo na mshiko hazimsaiddi nape, jamii ya sasa ni ya waelewa wanamwona mropokaji , roho ya kushindwa na ya kwanini ndo inamsumbua.na hamasa kubwa ambayo inaonyesha kuna dira ya utekelezwaji
 
Hivi wale maninja wa igunga walipatikana? Huu kwa wenye akili na busara unaitwa uzushi huru ni kwa wendawazimu tuu!
 
Naomba wadau msome huu uzi mtoe maoni yenu, kwa kuwa nimeshindwa kumwelewa huyu katibu mwenezi wa CCM, Kauli zake zimejichanganya.
 
JJ.Mnyika wala usipate shida ya kumjibu mtu mwongo mpuuzi na mtetezi wa mabepari.
Nape anajua kuwa kwa kelele zake za aina hiyo ndipo anajihakikishia kuiendesha family yake, japokuwa anasahau kuwa kwa enzi hizi hawezi kuwapata mapompompo wa kuwapaka uharo wake.
Ni kweli tunahitaji maendeleo ktk familia zetu, lakini hii hatua ya Nape ni kujivua suruwale na kubaki na boxer a.k.a UJINGA JAZZ.
 
Huyu jamaa ni boya sijawahi kuona. Anaposema kuwa sasa hivi ugunduzi wa gesi, mafuta na madini vimeshika kasi, anataka kutuaminisha kuwa tokea zamani hatukuwa na madini hapa nchini? Madini yetu si serikali ya CCM imewapa bure mabwana zao wa USA na UK, nani asiyefahamu hilo?

Nepi kama kweli ungekuwa na uzalendo na nchi yako, katika matukio yote ya hatari yanayofanywa na serikali yako ya CCM umetolea kauli gani? Mfano wa matukio hayo ni:-
-Utoroshwaji wa wanyama hai unaofanywa na serikali ya CCM
-Mabilioni ya fedha yaliyohifadhiwa huko Uswisi na viongozi wa serikali ya CCM
-Mikataba mibovu katika sekta za nishati na madini uliyosainiwa na viongozi wa CCM
-Mateso na mauaji ya raia yanayofanywa na wana CCM/serikali ya CCM
-Migomo isiyoisha makazini na ktk sekta mbali mbali
-Ufisadi wa EPA,meremeta, Kagoda, chenji za rada n.k

Hata kama CDM wanapewa hela na wafadhili wao, hiyo sisi hatujui na haituhusu kama wewe unawafahamu wataje kwanza wale wanaowaingizia hela viongozi wa CCM kule uswisi kwaajili ya kiwese chetu halafu baadae ndo uwataje hao wa CDM. Na pia tupe maelezo zile hela mlizoingiziwa Uswisi, in return mtawapa kitu gani hao wafadhili wenu ili tujue kama mtawapa maliasiri zetu au kuna vingine mnavyopeana na hao waarabu pamoja na akina Cameroon.
 
Back
Top Bottom