Nape awapokea wanachama wapya CHUO Kikuu cha Tumaini Kampasi ya SMMUCO - HIMO (Moshi)

Nape Historia itakuhukumu muda utakapofika. Tutakapobadili vitabu vya kihistoria
 
CCM inampokea fisadi Paul K laurent!! Ama kweli ccm sio makini. Huyu fisadi aliyevuruga serikali ya wanafunzi na kuitafuna hivi sasa amejiunga ccm ili atafute cheo. Sipati picha huko atakakoenda, ni ufisadi kwa kwenda mbele na aibu kwa ccm.
 
Yaani Nape kasafiri umbali wote huo kwenda kuwapokea wanachama wangapi? I bet nusu ya hao wanachama wapya wamekodishwa na nusu ingine tayari ni wanachama! wamefanya show. Hata hivyo ni vugumu kuamini ccm imeshuka viwango kwa kiasi hiki.
 
Dah inaonekana ilikuwa ya mafanikio sana. Keep it up comrade Nnape.
Vijana wengi mlioko magamba na wale tunaoambiwa wamejiunga ni wale wanaotegemea kutumia uongozi kutafuta mali. Bali wenye wenye nia njema na taifa hili; wale wenye dhamira ya dhati ya kuondoa nchi katika lindi la umaskini na ufisadi wako kwenye vyama makini kama CHADEMA...
 
Ni ukweli kuwa Nape amepokea wanachama wapya kutoka katika chuo cha SMMUCO. Lakini wanachama hawa ni mchanganyiko wa wanachama wa zamani wasiopungua 50 hamsini na wapya takriban 20. Wanachama hawa baada ya zoezi la kuapa walienda kwenye chakula cha mchana na Nape pale mjini Himo na kukodishiwa mabasi mawili aina ya Hino ya kampuni ya mabasi ya Ibra Line ya mjini Moshi.

Lengo la kuwaleta wanafunzi hao mjini Moshi lilikuwa kuwapandisha tena jukwaani kupokea kadi za CCM na kwamba waliandaliwa kadi za CHADEMA watakazorudisha. Lakini hali ya mkutano ilivyokuwa ngumu kwao walilazimika kuachana na mpango huo.

Awali wanyetishaji wetu kutoka katika vikao rasmi vya CCM walituhabarisha kuwa kuna mpango wa kupokea wanachama wapya 240 hapa hapa mjini Moshi. Vijana wa CDM walitanda uwanja mzima wakisubiri kuona ni akina nani hao walio amua kuwa wasaliti na kwa kweli tunamshukuru Mungu kwamba hakuna aliyejitokeza kwani kungewaka moto leo.
 
Stendi watu walikuwa wachache mno, hakunaanachama wapya waliopokelewa
Mimi nilikuwepo pale stendi,kwa kweli kama ndiyo hivi basi CCM 2015 Kazi wanayo.Kwanza nilisikiliza hoja zilizotolewa na Nape kuhusu kujivua gamba kwa kweli sikutegemea kama katibu huyu anaweza kuongea pumba kiasi hiki!eti anasema wameshajivua gamba sasa hivi ni wapya kabisa mara afananishe nyoka na nyoka wa shaba aliyenyanyuliwa na Musa,mimi nikadhani labda alivuta bangi kabla hajapanda jukwaani,sababu nyoka wa shaba hana gamba sasa unawezaje kumfananisha na magamba?alipoharibu zaidi ni pale alipoanza kuzungumzia mwafaka wa madiwani huko Arusha!hapo watu wakaanza kumzomea wakimshinika kuzungumzia tatizo la umeme lilioathiri uchumi wa nchi,lakini Nape hakusikiliza hayo malalamiko aliendelea na kuzungumzia siasa za kivuvuzela alizozoea..ndipo nikaona ni namna gani huyu bwana alivyo bogas!
 
Ni ukweli kuwa Nape amepokea wanachama wapya kutoka katika chuo cha SMMUCO. Lakini wanachama hawa ni mchanganyiko wa wanachama wa zamani wasiopungua 50 hamsini na wapya takriban 20. Wanachama hawa baada ya zoezi la kuapa walienda kwenye chakula cha mchana na Nape pale mjini Himo na kukodishiwa mabasi mawili aina ya Hino ya kampuni ya mabasi ya Ibra Line ya mjini Moshi. Lengo la kuwaleta wanafunzi hao mjini Moshi lilikuwa kuwapandisha tena jukwaani kupokea kadi za CCM na kwamba waliandaliwa kadi za CHADEMA watakazorudisha. Lakini hali ya mkutano ilivyokuwa ngumu kwao walilazimika kuachana na mpango huo. Awali wanyetishaji wetu kutoka katika vikao rasmi vya CCM walituhabarisha kuwa kuna mpango wa kupokea wanachama wapya 240 hapa hapa mjini Moshi. Vijana wa CDM walitanda uwanja mzima wakisubiri kuona ni akina nani hao walio amua kuwa wasaliti na kwa kweli tunamshukuru Mungu kwamba hakuna aliyejitokeza kwani kungewaka moto leo.
Tehe tehe tehe tehe imenikuna hiyo post yako mkuu wametoka bila,saaafiiiiiii.
 
Ila Nape alishutumu CDM ni chama cha wachaga na hawezi kukaa na wachaga, Uko moshi anatafuta nini??? au anataka chasaka??
 
Back
Top Bottom