Nape awapokea wanachama wapya CHUO Kikuu cha Tumaini Kampasi ya SMMUCO - HIMO (Moshi) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape awapokea wanachama wapya CHUO Kikuu cha Tumaini Kampasi ya SMMUCO - HIMO (Moshi)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albano, Jul 23, 2011.

 1. A

  Albano Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM ndugu Nape Nnauye amewapokea wanachama Wapya wa CCM Tawi la SMMUCO Tawi la Tumaini HIMO.

  Jumla ya wanachama Wapya 193 wamejiunga na CCM na wamefungua Tawi lao rasmi leo.

  Pia RAIS WA serikali ya wanafunzi wa CHUO hicho ndugu Paul K. Laurent amejiunga na CCM. Mchana kutakuwa na Mkutano MKUBWA wa Hadhara Moshi Mjini katika viwanja vya Polisi mkutano unaosubiriwa kwa hamu sana.

  HUU utakuwa mkutano wa kwanza kwa Nape kuhutubia katika mkoa WA Kilimanjaro toka ateuliwe kuwa KATIBU WA Itikadi na Uenezi wa CCM.
   
 2. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ataambulia wale wafuasi wa mzee wa Kiraracha.
   
 3. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Si aliwatukana watu wa Moshi huyu?? Aliwaita wabaguzi na ndiyo wenye Chadema. Au wachaga wamesahau nini??
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  je wanajiunga na ccm kwa maslahi au kwa sababu ya Nape inabidi kujiuliza hilo swali ndo muhimu sana..
   
 5. Chromium

  Chromium JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 598
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  SMMUCO wana campus Moshi mjini (Zamani kiwanda cha Kibo), Mwika, na ofisi kuu ziko Kibosho. Hiyo campus ya Himo wamefungua lini? (Manake mpaka leo asubuhi haikuwepo kwenye orodha!)

  Sasa, kama hilo tu dogo limekutatanisha, je hizo tarakimu unazozijua wewe na Nape itakuwaje?
   
 6. A

  Albano Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM ni taasisi kubwa sana inautaratibu WA kuwa na matawi kamili katika taasisi ya Elimu ya Juu. So hao wameingia kwa maslahi ya Chama chao na siyo mtu.
   
 7. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Hao wanafunzi watakuwa wamedanganywa kupewa ukatibu wa matawi ya Magamba wakimaliza chuo. Waulizie wenzao wa UDOM walidanganywa wakatoa na hela kumchukulia fomu JK na baada ya ushindi wa JK wakapigwa marungu na mabomu na Polisi wa CCm, ndo ije hao na hicho chuo chao cha Kata ya Himo. Sisi yetu macho tu, ila Nape hana hoja za kuweza kuzungumza na wanafunzi wa Campus yoyote kwa kuwa yeye Nape kasomea ngumbalu.
   
 8. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani walivyopiga marufuku Siasa vyuoni walikuwa wanamaanisha nini! Au vyama vya Upinzani pekee ndivyo havipaswi kufanya siasa vyuoni!

  Wachaga wanachoangalia Nape amekuja na nini mkononi! na si mdomoni. Kwa leo anaweza kuwapata hata wachaga wote, so long as anamwaga za GST Account vinginevyo hampati mtu.
   
 9. Edson Zephania

  Edson Zephania Verified User

  #9
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndo yule aliyesema Cdm ni chama cha wachaga na kaskazini?, kaenda kufata nini huko?
   
 10. N

  Ndakilawe JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 4,084
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Kwanza wanafunzi wa Himo hawawezi kuwa makritiko, ni rahisi kwao kurubuniwa, pia hiyo namba ya 193 new members, ni ndogo sana, CDM huwa wanafagia, ndo maana ccm hawapendi wafanye mihadhara, utasikia waliojiunga 2845, mara 1909 n.k..

  Kweli nape kilaza hawezi ongea campus zenye kritiko akasikilizwa, si unakumbuka hata kwenye mjadala ya nafasi ya vijana katika Taifa (TBC-waliirusha), alikuwa anauma uma maneno, lugha kongana, kiingereza no).

  Mimi kuna chuo nasoma Masterz na Nape, cjawahi kumwona darasani, na tupo full time, ila kwenye exams namwona.. Tumekubalia akipata hata alama"C", TUNAANDAMANA! uwezo wake kitaaluma tunaujua!

  Moshi mfukuzeni huyo, alishawakosea adabu
   
 11. Chromium

  Chromium JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 598
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nina mashaka na ukweli wa habari hii. Idadi ya wanafunzi wanaodaiwa "kujiunga na CCM" hailingani na idadi halisi ya wanafunzi wa campus moja moja (ambazo hata hivyo hazipo kwenye orodha). Labda ili tuchambue ukweli wa habari hii, tuambiwe, tukio hilo lilitokea campus ipi, na saa ngapi ndipo tuendelee.
   
 12. T

  The Priest JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  kumbe anasoma masters?ni chuo gani hicho!
   
 13. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kampasi ya Himo ni ipi hiyo?

  Idara ya Uenezi yenye taarifa mbovu namna hii...
   
 14. Chromium

  Chromium JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 598
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Huyu aliyekuwa Rais wa campus ya Mwika Paul Laurent, ni kati ya wanafunzi 68 wa BED mwaka wa tatu wanaotarajia kumaliza chuo siku chache zijazo. Nadhani anatafuta "mradi" wake kwa mlango wa CCM.

  Kwa mtu ambaye serikali yake haikuisha tuhuma za ubadhirifu, si ajabu sana kusikia amejiunga na CCM.

  Hata hivyo, mbona idadi ya wanaodaiwa kujiunga CCM haiwiani na idadi ya wanafunzi wote wa campus ya Mwika? Walifikaje himo kuhudhuria mkutano huo (mbali kabisa na chuo chao kilichopo Mwika)? Walisafirishwa? Ufafanuzi unahitajika zaidi
   
 15. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Safi sana Said, Nape upo?
   
 16. V

  Vonix JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Wanaweza kuchakachua idadi ya watu ili kuonyesha wanakubalika.
   
 17. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  UDSM mbna haendi?
   
 18. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  Kweli nchi yetu haina wasomi, bali kufka chuo kikuu ni ulazma wa mfumo wa elimu. Hakika siamini wasomi wa chuo kikuu kurubuniwa na Nape, kama ni umaskini ni heri nif e nao.
   
 19. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #19
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Nilishasema wenye taaluma za mashaka usalama wao kisiasa na kimaisha upo CCM. Angeenda kufanyia mkutano Uwanja wa Mashujaa Moshi au Pasua ama Njoro kama angeshuka jukwaani akiwa Mzima.
   
 20. T

  Toneradio Member

  #20
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 65
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  KATIBU wa NEC, Itikati na Uenezi Nape Nnauye akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Silo Swai katika mapokezi yaliyofanyika Chekereni mkoani humo. Kushoto ni Katibu wa mkoa Stephen Kazidi


  [​IMG]
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipokea saluti kutoka kwa kijana wa CCM wakati wa mapokezi ya msafara wake, eneo la Chekereni, Vunjo mkoani Kilimanjaro. Wengine ni Mwenkeiti wa CCM mkoa wa Kili, Silo Swai na Katibu wa mkoa steven Kazidi
  [​IMG]
  Katibu wa NEC CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza baada ya kuzindua tawi la wanachama wa CCM la wasomi wa Chuo Kikuu cha Tumaini (SIMCO), katika mkutano uliofanyika katika mji mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro, jana. Wengine kutoka kushoto, wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Vicky Nsilo Swaijaro na kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kaidi na Mwenyekiti wa Tawi hilo Mijo Laizer
  [​IMG]
  Wanachama wapya wa CCM tawi la SIMCO wakila kiapo baada ya kupewa kadi na Nape mjini Himo, jumla ya wanachama 108 ktoka chuo hicho walikabidhiwa kadi
  [​IMG]
  Baadhi ya wanafunzi wa SIMCO wakiwa kwenye mkutano na Nape mjini HIMO, wapili kulia ni Rais wa SIMCO Paul Raurent
  [​IMG]
  Nape akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Silo swai katika mapokezi yaliyofanyika Chekereni mkoani humo. Kushoto ni Katibu wa mkoa
  CHANZO: ZIARA YA NAPE MOSHI MKOANI KILIMANJARO
   
Loading...