Nape awalipua Dr. Slaa na Mbowe, amtetea Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape awalipua Dr. Slaa na Mbowe, amtetea Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MJIMPYA, Jun 2, 2011.

 1. MJIMPYA

  MJIMPYA JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ndiye Waziri Mkuu pekee anayeishi maisha ya kawaida barani Afrika na gharama zake za maisha ni ndogo kuliko hata za baadhi ya viongozi wa Chadema.

  Nape alisema hayo jana akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja wa sekondari ya Msakila mjini hapa katika ziara yake ya kwanza mkoani Rukwa tangu ateuliwe kushika wadhifa huo.

  "Sisi sote Pinda tunamfahamu ... napenda kukuhakikishieni, kwamba Pinda ndiye Waziri Mkuu pekee Afrika anayeishi maisha ya kawaida, ni mwungwana kwa kauli na vitendo," alisema Nape na kuwataka wananchi hao kukataa upotoshaji wa viongozi wa Chadema.

  Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alipokuwa Katavi ambako Pinda ni Mbunge, alidai Waziri Mkuu alikuwa anafurahia anasa za cheo chake.

  Akiwa katika vijiji vya Majimoto, Mbende na Usevya alikozaliwa Pinda, Dk. Slaa alidai Waziri Mkuu na wasaidizi wake wanatembelea magari ya gharama kubwa wakati wapiga kura wana hali ngumu ya maisha.

  Nape alisema Chadema wanamtuhumu Pinda kuishi maisha ya anasa wakati viongozi wa Chadema, akiwamo Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, ambaye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, akiishi maisha ya gharama za juu kuliko Waziri Mkuu.

  Alidai kuwa Mbowe alipopata nafasi hiyo bungeni, aliilazimisha Serikali impe gari la kifahari aina ya Toyota Land Cruiser V8 ambalo alidai gharama zake ni mara mbili ya gari analotembelea Pinda.

  Nape alisema Serikali ya CCM inakusudia kupeleka muswada bungeni unatenganisha siasa na biashara ili wafanyabiashara wabaki kwenye biashara, kwa kuwa wanasiasa kujiingiza katika biashara kunachangia ukwepaji kodi na kuliingizia taifa hasara.

  "Wanasiasa kama Mbowe tutawabana, waamue kati ya siasa na biashara, kwani wanachangia kukwepa kodi ambao ni wizi huku wakijifanya wanatetea wananchi.

  "Kwa mfano namshangaa sana Mbowe, kwa kuamua kubariki mshahara wa Sh milioni saba anaolipwa Dk. Slaa kuwa eti ni posho!" alishangaa Nape.

  Alisema, baraka hizo za Mbowe kwa mwaka zinasababisha Taifa kupata hasara ya Sh. milioni 25 na kwa kuwa watendaji wengine wa Chadema pia wanalipwa posho badala ya mishahara, kwa ujumla wanaliingizia Taifa hasara ya Sh. milioni 487.

  Alifafanua kuwa, fedha hizo ambazo ni hasara hiyo inayosababishwa na Chadema kugeuza mshahara kuwa posho ili isilipwe kodi wakati wafanyakazi wengine wote wanatozwa kodi, zingeweza kununua vitabu vya Sayansi 48,000 kwa sekondari nchini na madawati mengi.

  Kuhusu tuhuma kuwa alitaka kuhama CCM na kujiunga na CCJ, Nape alisema, kamwe hawezi kukihama chama hicho kwa sababu ni cha waungwana, kwa kuwa kiliasisiwa na waungwana.

  Alisema mambo ya CCM ni ya kimungu, ndiyo maana Watanzania wameendelea kukiamini na kukipa ridhaa ya kuongoza nchi kwa amani na utulivu.

  Source: Habari Leo
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  So CCM itaua AZIMIO LA ZANZIBAR? KUNA WAFANYABIASHARA kama MBUNGE WA IGUNGA NDANI YA CCM Rostam Aziz

  INA MAANA UBIA KWENYE MAKAMPUNI AMBAYO MAWAZIRI WAMEJIUNGA WATAJIONDOA mfano Mwizi Mkuu Omar Abadalla Kigoda
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 59,960
  Likes Received: 37,451
  Trophy Points: 280
  Akili za Kimungu!? Mungu gani anayemzunguzia huyu? CCM ambayo inagawa rasilimali zetu kwa bei ya bure kupitia mikataba ya kifisadi, inayodhulumu mali ya Watanzania kupitia wale wanaojiita Viongozi ndani ya chama hicho cha mafisadi, inayoshindwa kutetea maslahi ya Watanzania na Tanzania kwa miaka mingi sasa na hata kusababisha nchi kwenda mrama!!!

  Nadhani alikosea hapa alitaka kusema CCM ni ya kishetani na hakuna Watanzania waliowapa ridhaa katika uchaguzi wa 2010, mlichakachua uchaguzi katika majimbo mbali mbali na pia katika uchaguzi wa Rais na hili wala siyo siri na Watanzania wengi wanalifahamu.

  Hebu acha kukufuru kwa kukifananisha chama cha magamba/mafisadi/majambazi na Mungu!
   
 4. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,510
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Huyu dogo ana matatizo gani? Ameambiwa akitaka kukoga nyoyo za watanzania aeleze ni jinsi gani serikali ya CCM inatekeleza ilani ya uchaguzi. Hii ya kuiimba Chadema as if CCM ndio chama cha upinzani haina mshiko hata robo na wala haitasaidia kurudisha mapenzi yaliyopotea kwa CCM. Just wasting his time for nothing!!!!

  Tiba
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,071
  Likes Received: 5,209
  Trophy Points: 280
  Really?

  Najilazimisha kuamini kuwa mdogo wangu huyu ana uchungu kweli na upotevu wa fedha za umma na kuwa kipimo hiki anchokitumia ataanza kukitumia kwenye PPF, ATCL, n.k na atatoa pendekezo kuwa posho na mishara ya Wabunge ipunguzwe kwa asilimia angalau 30 halafu tuone ni kiasi gani cha fedha tutaokoa halafu tukiziokoa tutafanya nazo nini.
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hizi sasa ndizo zinazoitwa porojo. Numbers don't lie, Ukija na numbers njoo na mchanganuo. Hizi vague statements imekuwa ni janja ya viongozi wa CCM kwa miaka mingi. Hawafahamu kwamba wananchi siku hizi japo hawatamki lakini wanataka specifics. Maswali kadhaa kwa bwana Nape

  1. Hiyo anayoisema hasara ya ml. 487 ameipataje na ni kwa muda gani?

  2. Hivyo anavosema vitabu vya sayansi 48,000 anapataje mchanganuo huu, ina maana vitabu hivi vinauzwa bei flat rate? Nape inawezekana hana idea kwamba kuna vitabu vya sayansi sekondari kimoja ni Tshs. 200,000.00

  3. Hayo anayoita madawati mengi ni mangapi?

  4. Anaweza kutufafanulia hayo anayoita mambo ya CCM ni ya kimungu?

  5. Tano na kuu kabisa, kama alivyoainisha Mkjj, Nape anaweza kuwa sincere na kutupa idadi ya madawati na vitabu vya sayansi kutokana na zile Bilioni 40 za Kagoda?

  Du! inaonekana sasa hawa wanaCCM hawana hata aibu, ujumbe mkuu wa akina Nape ni kwamba "UFISADI NINI BANA MBONA HATA CHADEMA UPO?''
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 36,440
  Likes Received: 14,750
  Trophy Points: 280
  du,wajinga ndio waliwao. Kwa hiyo hii hotuba ya huyu dogo watu waliipigia makofi? Haaaa.!!
   
 8. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Hivi nape hata alipokuwa Mkuu wa wilaya alikuwa anafanya nini???? Kwa kauli zake he didnt deserve kuwa katika government postion hata ya ukuu wa wilaya.

  Mtu kama huyu angepelekwa wilaya kama mwanza bukoba moshi wanachi wangemkataaaaa. U can tell kuna wilaya nyigine zinazaraulika


  Hajui hata kutafuta hoja ambazo zinamuweka huru. Kweli siasa za Tanzania ni propaganda na Nape is not serious. Angekuwa ni mtu aliyesomea U injinia kidogooo ningmueeelewa.
   
 9. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,009
  Likes Received: 3,649
  Trophy Points: 280
  Tumbaku mbaya sana!
   
 10. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 469
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jamani hizi porojo zingine ni dalili ya kuishiwa kabisa, kwani chadema wanapata RUZUKU kiasi gani kwa mwaka mpaka kodi ya mishahara na posho iwe milioni 487? kwa mwaka? ina maana chadema wanastahili kulipa kodi takribani nusu ya Mapato ya Ruzuku au mimi sina data nzuri?
   
 11. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,491
  Likes Received: 465
  Trophy Points: 180
  Sina la kusema kuhusu mizengwe pinda,ila I can't wait for CCM to incorporate Azimio!!...hii ni kitu muhimu sana!!! sana sana!!!....the rest is bullsh*t!
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Mbowe hata angekuwa na nyumba inayoelea angani ni kutokana na jasho lake, hakuna pesa ya mlipa kodi anayotumia Mbowe. Anakwepa kujenga hoja za uvujaji wa pesa za umma kwa kudandia ngamia asiyezoea kumwendesha yatamshinda.
   
 13. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #13
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,096
  Likes Received: 607
  Trophy Points: 280
  Nape ni bogus sana ingawa nilikuwa na matumaini naye wakati akigombea madaraka ndani ya CCM. Baada ya kupata madaraka hayo ameonyesha rangi zake halisi kuwa hakuna mwana-CCM mwenye akili. Vile vile kila ninapoona picha zake naona kama vile anazeeka kimaumbile kwa kasi ya haraka sana, inawezekana na akili zake pia zinazeeka haraka sana.

  Njia anayotumia ya kujenga chama chake ni kuwa:
  (a) anakubali kuwa chama chake hakifai kama ambavyo CDM wanavyosema,
  (b) anashambulia CDM kuwa nao hawafai zaidi kuliko CCM.

  Hiyo siyo njia nzuri ya kujenga chama cha kisisasa, kwani kama atafanikiwa basi wananchi wanaweza wakahamia chama kingine zaidi ya CCM na CDM.

  Ninamtegemea aje na hoja za kuonyesha kwa nini watu waipende CCM siyo atuambie kwa nini watu wasiipende CDM.
   
 14. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nape bado hajaelewa mada, hajajua nini maana wa ufisadi, anatakiwa apewe elimu. Inaonekana CCM haina la kuwaeleza wananchi wapiga kura inaowatawala. Kijana mdogo anashindwa kuunganisha dot na kutengeneza riwaya.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,071
  Likes Received: 5,209
  Trophy Points: 280
  Kobello hilo haliwezekani. CCM kama wanataka wavunje chama basi warudishe Azimio. Huwezi kuwa na Azimio la Arusha bila kufuata misingi ya Ujamaa wa Nyerere. Azimio haliwezi kusimama peke yake.
   
 16. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,491
  Likes Received: 465
  Trophy Points: 180
  Mzee mwanakijiji,

  Ukijaribu kuangalia kwa undani,Azimio la arusha nguzo yake kuu si utaifishaji,ni uongozi.Biashara si dhambi, ila kama unataka kujenga nchi kwa misingi ya ujamaa na kujitegemea kama katiba inavyosema, viongozi wa umma ni muhimu kuwa wakulima (peasants not farmers) au wafanyakazi. Hii ndiyo inatakiwa iwekwe kwenye katiba!

  Na mali zote ziwe reported and audited before and after your term as a leader (ingawa hii ipo sasa hivi) ila haishughulikiwi.
   
 17. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #17
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 135
  mtu makini, Nape anatuambia Mbowe aliilazimisha serikali impe gari, alafu serikali ikakubali
   
 18. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #18
  Jun 2, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,857
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Nape ! Hana tofauti na Tambwe Hiza , naona hata makamba yupo timamu .
  Kwahiyo Mbowe ndio anaidhinisha manunuzi ya magari kwa mbunge .
  Huo ni uthibitisho kua anaukenge ktk akili.
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,054
  Likes Received: 3,804
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa na matumaini na Nape, lakini naona hakuna la maana bora hata Makamba alikuwa na mvuto....
   
 20. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #20
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,054
  Likes Received: 3,804
  Trophy Points: 280
  .....majani..
   
Loading...