Nape atumia ziara zake mikoani kumwandama Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape atumia ziara zake mikoani kumwandama Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jul 2, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  KATIBU wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye anadaiwa kuwatisha wanachama wa chama hicho wanaomuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

  Chanzo chetu kilicho ndani ya chama hicho, kimesema chini ya mkakati huo, Nape amekuwa akiwatisha wana CCM hao wakiwamo wanaotarajia kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho.

  "Kuna mkakati mbaya unasukwa na Nape na amekuwa akitumia nguvu zote kuhakikisha wana CCM wanaomuunga mkono Lowassa hawapiti katika uchaguzi wa ndani wa chama chetu.

  "Katika kutekeleza hili, Nape anawatisha watu hao moja kwa moja kwa kukutana nao ama kwa kuwapigia simu na kuwaeleza madhara ya kuendelea kumuunga mkono Lowassa.

  "Katika hili, amekuwa akiwaambia kuwa, hawatakiwi kuwa upande wa Lowassa na kibaya zaidi anawaambia kuwa, kama wataendelea kuwa upande wa Lowassa, hawatashinda katika nafasi zozote watakazogombea au atakata majina yao pindi watakapogombea," kilisema chanzo hicho.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, Nape anatekeleza mpango huo katika ziara zake anazozifanya katika mikoa mbalimbali nchini, kwa kisingizio cha kukijenga Chama cha Mapinduzi.

  Chanzo hicho kimeendelea kusema kuwa, hadi sasa Nape ameshawatisha baadhi ya wana CCM walioko katika Mikoa ya Iringa, Mbeya na Ruvuma.

  Chanzo hicho, kimeendelea kusema katika utekelezaji wa mkakati huo, Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi, amekuwa akimtumia mmoja wa vijana walioko katika Idara ya Mambo ya Nje, aliyetajwa kwa jina moja la Nyakia. Kijana huyo yuko Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Dar es Salaam.

  "Nape anamtumia Nyakia katika mkakati huu kwa sababu kila anapokwenda, anakuwa naye na huyu kazi yake ni kufuatilia kila mkoa ni nani yuko upande wa Lowassa, kisha anampa taarifa Nape ambaye huwaita na kuwatisha au huzungumza nao kwa njia ya simu, akiwataka wasiwe upande wa Lowassa," kilisema chanzo hicho.

  Nyakia alipozungumza na MTANZANIA kwa simu juzi, alihamaki na kutaka aelezwe ni nani aliyetoa taarifa hizo katika vyombo vya habari.

  Hata hivyo, mwandishi wetu aliposema hawezi kumtajia aliyetoa taarifa hizo, alisema hana taarifa nazo na kutaka aulizwe Nape kwa kuwa ndiye anayejua jukumu lake ndani ya chama.

  Nape alipozungumza na MTANZANIA jana kwa simu alisema jambo hilo halipo kwa sababu katika dunia ya sasa, huwezi kumtisha mtu kwa kuwa hakuna sababu ya kufanya hivyo.

  "Kwanza kabisa jana ulizungumza na Nyakia, kisha ukazungumza na Chongolo, sasa nasema hivi, jambo hilo halipo kwa sababu mimi siwezi kuwatisha watu katika dunia ya sasa.

  "Nakwambia huo ni upumbavu, najua wanaoandaa mambo haya ni Lowassa na wenzake, tafadhali msijiingize katika mambo haya, kama mtaandika andikeni, lakini mwishowe tutaanza kuwapiga wao kisha tutawapiga nyinyi ambao ni rafiki zetu.

  "Mimi kazi yangu mikoani ni kuimarisha chama, yaani tukikaa ndani bila kutoka nje yanakuwa matatizo, tukitoka nje yanakuwa matatizo, nasema hayo mambo hayapo, waambieni welete hata mtu mmoja aliyetishwa na mimi au hata aliyetishwa na ofisa wangu.

  "Hili siyo jambo jema mnataka kutugombanisha, sasa kama mtaitumia tumieni lakini ipo siku tutaanza kuwapiga na nyingi," alisema Nape kwa hasira.

  CHANZO: Gazeti la Mtanzania
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nape anatapatapa tu, mzimu wa Lowasa unamtesa...
   
 3. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM dhaifu inamwogopa kweli Lowassa, walimtosa kwa Richmond ya Kikwete, ambae alimkataza Lowassa kuifukuza
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  nape asipoteze mda kushindana na lowassa yule ni kichwa wenzake wengi wamekuja na kuondoka yeye bado yupo
   
 5. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hivi kweli bado unaamini Lowassa ana lake katika nchi hii?kwishney!!!!!
   
 6. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nape hana jipya ameshiba pesa za Membe....lakini wasahau urais 2015 ni LOWASA AU DK.SILAHA tunataka watendaji si wapiga porojo.
   
 7. angedizzle

  angedizzle JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 560
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 80
  nape = gamba
   
 8. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,728
  Likes Received: 12,802
  Trophy Points: 280
  Nape nadhani anataka kufukuzwa na nyinyiemu!

  Kwanza nape hamuwezi lowasa kwa lolote

  basi amvue gamba kama anaweza
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Lowassa ni mwamba Yule hamna mtu wa kumfanya kitu
   
 10. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Vita kati ya Nape na Lowassa vimemuimarisha Lowassa na kumpa nape jina la vuvuzela!!!
  Nape hamuwezi lowassa,ataishia kufa kifo kibaya kisiasa
   
 11. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,897
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  Hivi siku 90 za kumvua gamba lowassa na chenge hazijaisha?alidakia kauli ya kisanii ya boss wake ambaye pia anamuogopa lowassa
   
 12. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  lowasa ni mnyama hatari hata JK anajua..NAPE kavamia gari liloko kwenye MOTION
   
 13. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sijampata vizuri anaposema "Tutawapiga"! Hiyo ndio imekuwa njia yao ya kuwanyamazisha watu wanaowapinga! Pole sana Dr. Ulimboka, laiti kama ungelijua hili mapema.
   
 14. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jk yupo nyuma ya kuchafuliwa Lowassa, wanajua akishinda atachapa bakora CCM nzima, Lowassa ni Uzalendo tu aloutoa Jeshini na si chama, ubilionea wake ni asilia na nyerere shahidi
   
 15. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,534
  Likes Received: 10,452
  Trophy Points: 280
  analake ndani ya ccm, nje ya ccm sawa na mamba nchi kavu hana kitu.!
   
 16. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #16
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,403
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Nape anampa shida sana lowassa....too bad hana cha kumfanya zaidi ya kumtungia uzushi
   
 17. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  waliishia kuzodoana tu!
   
 18. piper

  piper JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Simshangai, na magamba kutisha wanachama wao ni jadi ili kufanikisha jambo wanalolitaka
   
 19. a

  andrews JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  pole sana nape kwa kujua kuwa lowassa ni dume la mbegu na humuwezi kwa lolote 2013 ndio mwisho wako na lowasa na akina chenge wanapeta tu sijiu utafanya kazi gani maana unchokijua ni siasa tu si kingine
   
 20. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145  JUMATATU, JULAI 02, 2012 05:50

  NA MWANDISHI WETU - MTANZANIA  KATIBU wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye anadaiwa kuwatisha wanachama wa chama hicho wanaomuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.Chanzo chetu kilicho ndani ya chama hicho, kimesema chini ya mkakati huo, Nape amekuwa akiwatisha wana CCM hao wakiwamo wanaotarajia kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho.

Loading...