Nape atoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ziara zake za mikoani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape atoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ziara zake za mikoani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nhassall, Jul 18, 2012.

 1. n

  nhassall Senior Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  YAH; UPOTOSHAJI WA ZIARA ZA CHAMA MIKOANIToka tarehe 03/05/2012 nimekuwa na ziara kadhaa za kichama katika mikoa mbalimbali kwa lengo la kukiimarisha Chama. Baadhi ya mikoa niliyofanikiwa kufika ni pamoja na Ruvuma, Njombe, Iringa,Mbeya,Kagera,Rukwa na Katavi. Ziara hizi zimekuwa zikilenga kufanya yafuatayo kati ya mengi niliyofanya:1. Kukagua uhai wa Chama2. Kukagua maendeleo ya uchaguzi ndani ya Chama3. Kukagua miradi mbalimbali ya kiuchumi ya Chama4. Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCMKwa muda sasa pamekuwa na juhudi za makusudi za kupotosha nia na madhumuni ya ziara hizi na kujaribu kuonyesha kuwa kinachofanyika hakina baraka za Chama na hivyo kimesababisha mgogoro ndani ya Chama, hasa kati yangu na Katibu Mkuu.Juhudi hizi zimelenga kukatisha tamaa jitihada mbalimbali zinazofanywa na Chama za kuwa karibu na wanachama wake na wananchi. Kwa bahati nzuri vyombo vya habari vinavyotumika kusambaza uzushi na uongo huu vinajulikana ni vya nani, hivyo ni rahisi kujua kwanini wanafanya wayafanyayo.Kwa mfano, wanadai kuna pesa nyingi ninapewa mimi kama Katibu wa Itikadi na Uenezi na ninapewa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM bila Baraka za Katibu Mkuu wangu ambaye ndiye msimamizi wangu mkuu na kwamba hilo limezua malalamiko na migongano kati yetu.Huu ni uzushi wa kitoto sana, kwani wanataka kuwaaminisha wana CCM na wananchi kwa ujumla kuwa mambo si shwari ndani ya CCM. Huku wakipuuza ukweli kuwa Katibu Mkuu wa CCM ndo msimamizi wa mapato na matumizi yote ya CCM, hivyo kama kuna ziara au jambo linalohusu matumizi ya pesa ndani ya Chama, lazima liwe na baraka zake.Lakini wanafumba macho ili wasione kuwa, Katibu Mkuu wa CCM ndio mwenyekiti wa sekretarite ya Chama Taifa, hivyo sisi wajumbe wote wa sekretarieti tunafanya kazi chini ya maagizo na usimamizi wake wa karibu. Kama kuna mafanikio yeyote basi mwasisi wa mafanikio hayo ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa ndugu Wilson Mukama, kwani yeye ndiye kiongozi wa sekretarieti hii.Itakumbukwa kuwa nilipoanza ziara hizi, wapotoshaji hawa walituhumu ziara zangu kuwa zinalengo la kutisha baadhi ya watu wasigombee nafasi mbalimbali ndani ya Chama kisa wao na mimi tuna mitazamo tofauti ndani ya chama. Nilipowataka kulithibitisha hilo na wakashindwa, sasa wamekuja na tuhuma mpya.Nawaomba wana CCM, wapenzi na mashabiki wa CCM na wananchi kwa ujumla kuupuuza uongo na uzushi huu kwani hauna ukweli wowote. Umetungwa na watu wenye roho mbaya wasioitakia mema CCM, wanaotamani kuona CCM haitulii na hivyo mambo yasimame ndio furaha yao. Sasa wakiona mambo yanakwenda viroho vyao vinawauma.Nataka niwathibitishie sekretarieti ya Taifa ya CCM iko imara, thabiti, madhubuti na yenye mshikamano tukifanya kazi kwa pamoja na upendo chini ya uongozi imara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Mukama.Wanao yatunga na kuyasambaza haya wanapoteza muda wao.Nawathibitishia uzushi huu hauta athiri kasi yetu ya kujenga Chama chetu wala ari yangu binafsi katika kukitumikia Chama changu kwa nguvu zote. Hivi ninavyoongea tayari maandalizi yamekamilika ya mkutano mkubwa wa hadhara mjini Kigoma siku ya kesho tarehe 19/07/2012 kwa lengo la kuzungumza na wana Kigoma juu ya mafanikio na changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa wa Kigoma.Katika mikutano hii mingi nina ambatana na baadhi ya mawaziri wa wizara mbalimbali zenye maeneo ya utekelezaji kwenye mikoa husika. Kwa mfano Kigoma tutazungumzia hatua iliyofikiwa katika sekta ya Uchukuzi kwa maana ya reli, bandari na anga. Lakini mkoa huu una kero kubwa ya maji hasa mjini Kigoma. Kuna changamoto kadhaa kwenye serikali za mitaa, kuna mengi yanayoendelea ya ujenzi wa miundimbinu kama barabara nk.Staili hii tunayotumia kwenye mikutano mingi ya hadhara ambayo kwakweli inatutofautisha sisi Chama tawala na vyama vingine vya saisa nchini, tuliizindua pale jangwani kwenye ule mkutano mkubwa wa kihistoria mwezi Mei mwaka huu! Staili hii imepewa jina la AHADI NI DENI. Hivyo wana Kigoma na maeneo mengine kaeni mkao wa kula, AHADI NI DENI inakuja kwenu.Itakumbukwa tuliwaahidi katika mkutano wa Jangwani kuwa tutazunguka nchi nzima, lakini tofauti na wenzetu wanaotukana na kukashifu kila kinachofanyika na kilichofanyika sisi tunakwenda kupeleka majawabu ya changamoto mbalimbali kwenye maeneo yao. Na hii ndio tofauti ya vyama vya upinzani na Chama tawala. Wakati wao wanabeba matusi na kejeli kwenye mikutano yao, sisi tunabeba majawabu namtumaini kwa wananchi. Kwahiyo “ahadi ni deni” imelenga kuzipitia ahadi zetu kwa wananchi na namna spidi ya utekelezaji wake ilivyo.Nawataka sasa, hawa wanaozusha maneno na kujaribu kupotosha ziara nizifanyazo mikoani kuacha mara moja, kwani kukaa kwangu kimya haina maana kuwa siwafahamu. Nawaonya wakiendelea nitawasema hadharani bila kumumunya maneno. Nasema inatosha, upotoshaji mliofanya unatosha, sasa basi.KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZIImetolewa na;Nape Mose NnauyeKatibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCMItikadi na Uenezi
   
 2. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Nina admire courage ya nape,ya kumsifia kunguru kwa rangi yake nyeupe.No one can do it.Next time aweke paragraph ili asomeke vizuri.Otherwise keep it up hata yule waziri wa habari wa Sadam alijitahidi hadi Baghdadi ilipotekwa yote.
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu- Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  44. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  45. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  46. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  47. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  48. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  49. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  50. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  51. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  52. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  53. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  54. Kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  55. Kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  56. Kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  57. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kibandamaiti mjini Zanzibar
  58. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  59. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  60. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  61. Kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  62. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
  63. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  64. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  65. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  66. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  67. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha

  Tunasubiri utekelezaji wa haya sio porojo tuu za kupitisha siku sijui Ahadi ni Deni
  hizi ni ahadi za Mkuu wako na bado miaka miwili tuu amalize muda wake
  Sijui mtatuambia nini akishaondoka
   
 4. t

  tara Senior Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sidhani kama anakumbuka hata baadhi ya ahadi alizokuwa anatoa.....
   
 5. Gedeli

  Gedeli JF Gold Member

  #5
  Jul 18, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 452
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  nshindwa kuamini kama hii habari ameandika Nape, sikutegemea kwa wasifu wake aandike habari kama anarape bongo flave vile. hakuna Paragraph point zilizopangika nk. kama ni yeye kwenye mikutano yake nadhani ni bala zaidi.
   
 6. only83

  only83 JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Uwasilishaji wa mawazo namna hii bila kuzingatia kanuni za uandishi ni watoto wa darasa la kwanza na haufai hapa JF. Hivi umeshindwa hata kupanga vizuri li-habari lako ili liweze someka vyema?
   
 7. b

  beyanga Senior Member

  #7
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ​napita tu
   
 8. O

  Optimisticforchange Member

  #8
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Bro, yaani kwa ubabe wa chama sasa hata kuandika una-violate rules za uandishi? Wapi paragraph? By the way I did not like your single. If you ask me why? I don't know. Perhaps because I hate CCM and of course its members. We are going to show you guys on 2015 and that will be the lesson for you in future.
   
 9. Electron

  Electron Member

  #9
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mh! Attention seeker...! Baadae...
   
 10. b

  beyanga Senior Member

  #10
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ​kaambiwa apunguze safari naona analilia posho
   
 11. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,570
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 280
  Nape anajitahidi, ingalau unawezasoma alicho andika japo hakiigusi audiance, angekuwa shosti muuaji mwigula point zake!
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Posho Tamu Jamani. Nape Anamkaribia Komba sasa kwa Shavu LoL! Nape Maposhoooooooooooo
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nape bado anarudia makosa yale yale. Kwa kutoa taarifa maana yake ni kutaka umma usome na kutafakari, sasa Nape anataka watanzania wajadili ziara zake za siasa wakati watu wanazama huko Zanzibar? Kwa nini hakutoa hii taarifa jana au asubiri wkati mwingine? Watu wanahaingaika kutafuta taarifa za ndugu zao walioko kwenye boti yeye Nape anataka wasome ziara zake?

  Si muda mrefu kulikuwa na mjadala hapa kuhusu ziara yake kanda ya ziwa wakati wa maziko ya mmoja wa wapigania uhuru na yeye Nape kwenda kucheza golf wakati watu wanazika. Sasa leo anafanya blunder ile ile na hii inafanya watu wajiulize kama kweli he is really qaulified for the post!
   
 14. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
 15. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kuna mtu mmoja muhimu sana ahadi zake hatunazo.Kwa anayeweza kuweka ahazi Shein,maana walikua wanashindana na kaka yake kuahidi.Mpaka siku nikasikitika kwa jinsi Shein alivyokua amjejifunza kudanganya.Morogoro vijijini kabisa aliahidi barabara ya Lami.
   
Loading...