Nape atoa povu alipoulizwa CCM imekuwa chama cha Watoto wa viongozi kama yeye

sasa wewe ndio unataka kujishusha hadhi kuwa kulinganisha uwezo wako wa kufikiri na kujibu kuwa sawa na ule wa Nape.

Hivyo alivyosema ndipo uwezo wake unapoishia na hilo jibu ndio lililo wazi kuwa wao wanaamini kuwa hizo ndizo familia za kututawala na kinachotakiwa ni kuzaliwa tu kwenye hizo familia. Mkuu umesahau mzee Makamba alivyowahi kusema pia kuwa baba akiwa kwenye position na watoto watakuwa hivyo!?

Ujumbe ndio huo na kikubwa hapa ni jinsi gani tuta react ili kuondoa jamii ya hawa watawala wenye uwezo mdogo kufikiri huku wakijilinganisha na familia kama za akina Kennedy

hapo kwenye red pia namwongezea lusinde yeye ndo aliua kabisa "Msikubali kudanganywa ndugu zangu maswala ya mtoto kufata kazi ya baba yake, katika tanzania ni kitu cha kawaida, tunao wanajeshi na watoto zao wanajeshi uongo kweli?....kweliiiiii! tunao madereva na watoto wao madereva uongo kweli?.....kweliiii, tunao wapiga debe na watoto zao wapiga debe uongo kweli . . . kweliiii! kuna ajabu gani kwa sioi piga makofi kwake."
 
Jamaa ni vuvuzela. Lokipulizwa tu kama kawa halina mipaka wala kupambanua misingi ya hoja.
Nimeshangaa aliposema kuwa hoja ya ubadhirifu ni ya CCM. Wakati watu wote wanajua kuwa ni ya Bunge (Bila ya kujali imetolewa na mbunge wa chama gani). Pia eti wao wapo 78% wangetaka wangeimaliza.

Swali kama ni ya CCM kwa nini msiijadili kabla ya bunge na kutoa hayo maamuzi ?

Kimsingi yuko sahihi kusema hoja ya ubadhirifu ni ya CCM kwa maana kuwa ndicho chama na kinachoongoza kwa kuulea ubadhirifu na wizi wa mali ya nchi.
 
Inaelekea Nape aliulizwa maswali ya kustukiza na akawa hajajiandaa kuyajibu, hivyo akawa anabwabwaja yale yaliyo mdomoni mwake bila hata kufikiria. Kwa mfano Nape kutuambia kwamba amesoma kwa "kibatari" siyo kweli kabisa, maana anataka kutufanya tuamini kwamba kigogo Moses Nauye alikuwa akitumia vibatari, kitu ambacho si kweli kabisa.
 
In short amepigia mstari kuwa kama sio mtoto wa kigogo huna CHAKO CCM. I wonder anapata wapi kiburi cha kujibu maswali kama anavyojisikia. Na huyu ndo Katibu mwenezi wa chama ambacho kinaunda Serikali. This can only happen in Tanzania
 
Mzee Moses Nnauye alikuwa anaishi Sea View karibu kabisa na baharini, je watu wanaoishi sea view wanatumia vibatari majumbani kwao??????!!!!!!! wapiiiiiiiiiiiii

Huyu kijana anaonekana ni jinga kubwa
 
next time brother vuta subira kidogo, ji-compose, tafakari ndo uanze kubwabwaja kwenye runinga. wale watz waogawaoga hawapo tena. na kukushushua m-ccm ni kawaida na defence yako ni ndogo sana kwa madudu yanayofanywa na ccm. unahitajika kuwa na hulka ya yule waziri wa ulinzi wa saddam hussein kuweza kukitetea ccm hadharani leo tz!
 
Back
Top Bottom