Nape atasafisha chama alichokuwa anakichafua? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape atasafisha chama alichokuwa anakichafua?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MVUA GAMBA, Apr 13, 2011.

 1. M

  MVUA GAMBA Senior Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi nashangaa sana hawa CCM na suala lao la kuvua gamba, kila siku asubuhi hadi jioni Nape kwenye page yake ya Facebook alikuwa na kazi moja tu ya kukishambulia chama chake sasa kapewa kazi ya kukizungumzia kwa mazuri na kukinadi ili kikubalike zaidi. Kweli huyu alikuwa ni chaguo halisi kwa kazi hii ama ndio kufa kwa CCM hadi kinatapatapa tu. Tuchangie
   
 2. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Watanzania mpewe nini mridhike?! Ukipewa mbingu unataka ardhi!
   
 3. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu utaendelea kushangaa kama jamaa aliyeingia DSM na kushangaa feri hadi ugutushwe!!
  Hivi wewe unafikiri Nape alikitukana chama chake au amekisaidia sana kulingana na yanayotokea?
  Watu kama ninyi ndo mkiambiwa inama , mtainama bila kujiuliza kunani katika vyama vyenu.
   
 4. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nadhani ulikua huelewi nini Nape alikua anafanya kwenye Wall Facebook yake! Yeye alikua anatoa maoni yake kama Mtanzania na alikua muwazi bila kuficha nini anacho ona hakiendi sawa! Na hii imempa Nafasi ya Kupata nafasi ya kuwa Msemaji Mkuu wa Chama! Viva forever Comrade Nape tunakutegemea sana kuipa sura mpya CCM!
   
 5. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sasa swali langu ni hilo, safari hii ataendelea na mawazo hayo ama atabadilika na kama akibadilika na kuanza kusema matamu tu ya CCM huoni sasa atakuwa anakiharibu chama kwa kuwa wananchi hawatakuwa na imani naye?
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Jk kacheza mchezo wa ajabu:
  -Nape amewekwa pale ili ionekane CCM inapambana na ufisadi na vigogo wanaojiita wapambana ufisadi waliomo ndani ya ccmwanyamazishwe.
  -January Makamba -huyo sisemi kwani is quite obvious kila mtu anajua amewekwa pale kuwakilisha genge la aina gani
   
 7. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mafisadiwote waludishemaliwalizo pora wapelekwemahakamani usani wakuibambeya unahamishiwa mbagara hatutaki
   
 8. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,088
  Likes Received: 883
  Trophy Points: 280
  hivi si kuna kipindi huyu nape alikimbizwa kwenye chama na makamba au nimesahau?
   
 9. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu andika kwa ufasaha tafadhali ili ueleweke!!!
  The sentense above sounds childish and gibberish.
   
 10. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Usiniraumu waraumu mafisadi walinisababishia nikoseelimu yakutosha hii yamitaani tuvumiliane nami niwasilishe hisiyazangu
   
 11. B

  Burigi Member

  #11
  Apr 16, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Mheshimiwa Nape nakuandikia ujumbe huu kwa niaba ya secreatriet nzima mpya ya chama chetu kipya kimechojivua magamba juzi, Mimi ni mwanachama hai mwenye mapenzi dhati ya Chama changu cha mapinduzi lakini yasiokuwa na matumaini tena ni miongoni mwa maelfu ya wana ccm tuliokata tamaa.

  Ndugu Nape nilikuwepo dodoma wakati zoezi la kujivua gamba na niliondoka siku 4 baadae nikifuatilia matukio mbalimbali yaliotokana na ujivuaji wa Gamba kwa chama chetu, Ukweli ni kwamba hakuna mabadiliko kwa wakata tamaa wote wa ccm walioyaona na hakuna ameoweza rudisha roho yake au mapenzi yake kwa chama kwa tukio la secreatariet ya makamba kujiuzulu kwa kifupi haina Imapct yeyote hadi leo.

  Mh. Nnauye madhara ya au matatizo ya chama chetu hayako ndani ya Magamba yapo ndani ya Damu Mwananchi aliopo Kibondo Tandahimba kaisho hateswi na ROSTAM AZIZI, CHENGE AU MAKAMBA sio Kweli anateswa na mfumo wa chama ambao ni DAMU NA SIO MAGAMBA kama chama hakitaki kujua hilo ni kwamba tusishangae 2015 tukapata 40% ya kura zote kutoka hizi 61%
  Usichokijua huko vijijini viongozi wote wa vijiji wa chama chetu walishinda kwa kuiba kura sio kwa kuchaguliwa na wananchi hii ni kuanzia serikali za vijiji madiwani hadi wabunge jambo hili limefanyika kwa kulindwa na dola wananchi huko vijijini wanateswa na hawa madiwani na viongozi wa chama chetu wa serikali za vijiji hawa nao ni Magamba kwani wananchi wameapa hawatafanyiwa ushenzi huu tena .

  Mheshimiwa Nnauye kujivua gamba na huku mnalindwa na dola tunaongeza wigo mkubwa wa uadui kwa wananchi hata wale wanachama wetu wanajiuliza kwanini tunalindwa kama kweli tupo sahihi na tunapendwa.

  Wakati nipo Dodoma ulitangazwa mkutano wa kutambulisha secretariet ya Chama chetu cha Taifa ilikuwa ni wazo zuri lakini kilichonishangaza azimio hilo lilipitishwa jumatano saa tisa mchana kama kutakuwa na mkutano wa kutambulisha secretariet ya taifa siku ya Alhamis saa saba mchana Nyerere square katika mkoa wa Dodoma na jukumu walipewa CCM mkoa dodoma ilikuwa ni kazi ngumu kwani mkutano ulikuwa unafanyika ndani ya masaa machache na kibali cha mkutano kilikuwa hakijaombwa kwani sheria inataka ndani ya massa 24 sina uhakika kama Kibali kiliombwa na kama kiliombwa hakikukidhi Haja kwani kiliombwa chini ya muda kwa sisi wananchi wanachama wapenzi wa kweli tunasema huu ni uhuni huwezi kujivua gamba ukaendeleza uhuni uleule hii inaleta shaka kwani CCM hivi kwani vitu vya kisanii kila mahali na kila wakati huwezi kusimama kwenye jukwaa unasema umejivua gamba waakti hata vibali vya mkutano umefoji au havipo huu ni uhuni jee tutendeleee kuongozwa na uhuni uhuni tuu wasa CCM wa sasa wana watoto wamesoma shule wanachambua wanaelelewa wanawafumbua macho hata wazee wao mbumbu yaani wanachama mazoea kwa hiyo nyinyi mtakipeleka chama pabaya kuliko hata mzee makamba.

  Ni aibu wewe na secreatariet yako yote kusimama na kuwadanganya watanzania eti watu watatu ndiyo wameleta matatizo ya kukiua chama huu ni utoto bwana Nnauye Rostam hawezi kubuni biashara atangaze tender yeye na ajipe tender yeye hao alioshirikiana nao wapo wapi mbona bado wanahodhi madaraka makubwa tu ndani ya chama na serikali hayo ndiyo magamba kuna watu waliopitisha document hizi wakasaini wakakaa vikao wakabariki vikao mbalimbali vya matukio ya ufisadi mbona huwataji hao wapewe siku 90 hao waondoke ndani ya serikali ndiyo kujivua magamba huko chama hakitajengwa kwa nyimbo za komba tulifikiri nyimbo za komba na makundi ya bongo fleva yangetuletea ushindi lakini wananchi wamebadilika ulishuhudia kipigo kitakatifu uchaguzi uliopita hawa ndio watanzania wa sasa Bwana NNAUYE nguvu yenu ni ndogo sana tukiwapima na vijana pinzani wetu toka chadema kama kina Zito kabwe, John Mnyika, Mbowe ,Dr slaa kama wanavyomwita mashabiki wake kama ni Dr Wa Ukweli ( mnyonge mnyongeni acha aitwe hivyo anauwezo wa kujieleza kwa hisia za maslahi ya nchi kuliko ma madr na maprofessor wetu waliojaa bungeni kazi kupiga makofi hata katika mambo yasiyofaa.

  Nikirejea safari yangu ya Dodoma nilishuhudia kiongozi mmoja akitoa Oda watafutwe vijana 800 jioni hiyo kwa ajili ya kuhudhulia mkutano huo wakutambulisha secreatatiet pamoja na watoto wa halaiki wa shule lakini ilionekana mda saa ya wa shule ni umeisha kwenda na uwezekano wa watoto wa shule ni mgumu kupatikana lakini watajitahidi ila walipatikana madalali wa 5 kwa ajili ya kumobilize watu hao 800 Nilishtushwa sana na jambo hilo kesho yake nilisikia watu mia 650 wamepewa kadi mpya, mheshimiwa NNAUYE mliopwapatia kadi hawawezi na hawatakuwa wanachama wetu abadan hao ni mamluki wakuletwa kwa ajili ya posho huu ni uhuni chama kinaendeshwa kihuni mnamdanganya mwenyekiti kama mmeingiza wanachama 650 lakini uongo hao wanachama hawapo hatutajenga chama kihuni namna wewe na sekreatarieti yako mnafanya mambo ya kihuni mzee mkama anamdanganya Nani Gamba ni kuwa wa kweli kama misingi ya chama navyotaka propoganda na hadaa itatusaidia tena .

  Mzee mkama wananchi wataipa CCM heshima iwapo utawaambia wazi mbunge wetu wa shinyanga mjini hafai anakichafua chama kwa sababu ameiba kura za wananchi Hili ni gamba kwa wananchi wa shinyanga tumepoteza chama shinyanga wana CCM wenyewe tunataka kuona tunashinda kwa haki na mwizi wa kura fisadi hatukai naye , NNAUYE mwambie makongoro Mahanga umeiba kura ukonga step down uchaguzi mpya uitwe CCM tushinde kwa uhalali tuweke watu safi huko ndiko kujivua magamba bila ya hivyo mtapokelewa nchi nzima na wanachama waletwao na magari kutoka sehemu mbalimbali na posho juu lakini mashabiki wetu watakuwa ni walewale mashabiki maslahi kwa sababu hata katika mikutano ya chama ya kata wanachama inabidi wapewe posho ya pesa au chakula au usafiri ndiyo wahudhurie mikutano yetu hili ni tatizo kwa hiyo gamba limevuka lakini saratani yetu bado ipo ndani ya damu.Ni upumbavu kujisifiaeti tumemchukua shitambala wa Chadema toka mbeya impact yake nini kwetu mtu ambae alikiuza chama chama chake kwetu an haaminiki tena kwenye chama chake huyu katika medani za kisiasa hafai hata kualikwa kwenye mkutano wa kijiji wa chama chochote

  Mheshimiwa Mkama na secretarieti yeko sisi ndio wanachama wenu ni rahisi sisi kuwa assess kuliko nyie kujipima tunasema UVCCM Inauwa chama inatakiwa kuvunjwa iundwe upya vijana hao kwa maadili ya kitanzania hawafai na wanapoendelea kusimama kwenye majukwaa mnazidi kuwakera watu wamepoteza mvuto kupita kiasi ni watoto wakosa adabu hawawezi kuwatukana mawaziri wakuu wastaafu wa nchii halafu bado wakaendelea kupewa majukwaa hilo ni kosa la kiufundi mnafanya kabisa umma wa wana ccm na hata watanzania wenye itikadi mbalimbali walifadhaishwa na vijana hao kuendelea kwao kuonekana kwenye majukwaa ni kukiua chama mzee mkama unaonekana umezungukwa na vijana wahuni wanapoteza mvuto wa chama badilisha UVCCM hARAKA kuwin vijana damu mpya.

  Mheshimiwa Nnauye nimefadhaishwa na hotuba yako ya kutambulisha secretariet yako darajani manzese umenikatisha tamaa kabisa na wewe kuongea propoganda sisi tu wasomi wenzako hatutaki propoganda za kama kuna watu wametumwa Tabora ukiwa na maana ya chama cha upinzani kumchafua Rais wetu na viongozi wa dini watatumika huu ni ujinga upumbavu katika karne hii tunataka kuona tunazungumzia secretariet mpya itafanyaje kazi kuibana serikali iwajibike kwa wananchi sbb nyinyi ndio chama tawala mzee makamba tuliweza kumsamehe kwa umri wake na elimu yake lakini hata wewe msomi unaongea pumba watu wanataka issues na upangue issues na challenge zinazosukumwa na opposition kwa mtaji huu 2015 chama kitakuwa kinatembelea mkongojo na kitakuwa hakijiwezi imekuwa kama tumelogwa kila anayepewa nafasi anakuwa bogus.

  Mh.January makamba nimesikitika sana kusema watu wana wadanganya wanavyuo kwenda kuzomea umekosea wanavyuo ni wanataluma kama wewe ingawa wewe umewahi kufika kabla yao na si kwa nguvu yako acha dhihaki ya kipumbavu tunajua ulivyoingia kwa kubebwa hadi kufika hapo tangu kikwete akigombea uraisi na wewe kuingizwa kifix hadi kufikia hapo sio kusema wewe ni intelligent kiasi cha kuwadhihaki watoto wa wakulima kuwa wanatolewa vyuoni kuja kuzomea unatakiwa kuomba radhi jumuiya ya wanafunzi vijana wanauwezo wa utambuzi mkubwa sana sio wana ccm wa zamani hawawezi tena kuunga mkono upumbavu tunatakiwa kuwa smart na chama kuweka thinkers kwa ajili ya strategic watu wapo kwa maslahi ya nchi siyo kwa ajili ya chama kama akili zako zinavyokutuma walichozomea wanachuo ni makosa ya wazi katika mswada wa sheria kwa ajili ya faida yao na vizazi vyao ni tofauti wazomeaji WA CCM tuliowaleta ccm kule karimjee tukidhani wanachuo wanazomea kwa kuwa mswada ni wa ccm mnatupeleka wapi kujivua gamba ni kubadilika kabisa kimaadili hata kimaisha tusijivue gamba kwa kufukuza wanachama 10 hiyo haisaidii wewe ni mbunge lakini umeona upupu unaofanywa na wabunge wa ccm hata kama kitu hakina tija wanapitisha na kuunga mkono kwa kuwa ni cha CCM huko ndiko kuua chama chama hakiuwawi na rostam pekee kwa makosa yake ya kijinai chama kinauawa na makosa ya kimfumo ndiyo maana bunge liliopita liliongozwa na chadema wakati nyie mkiendelea kupinga hoja za maana eti kwa kukua tu ni za opposition na kuunga mkono ujinga wananchi wakatuhukumu Gamba livuliwe bungeni wabunge wafanye kazi ya umma na sio ya ccm .lakini kumbuka kuwaomba msamaha wanavyuo uliosema wanaletwa kuzomea kumbuka watoto hao wengine wamefanya kazi ya kupigania uhuru wa nchi hii kwa uadilifu mkubwa na wamekufa maskini na heshima bila skendo viongozi wa sasa.

  Mheshimiwa mkama huwezi jivua Gamba kama Arusha watu wanasema meya hakupatikana kihalali na watu wameuawa kujivua gamba kama mtendaji mkuu wa chama mshauri mwenyekiti wetu na Rais wa JMT Mh. Kikwete uchaguzi urudiwe arusha nina imani CCM itashinda na hata kama ikishindwa itakuwa na heshima zaidi kuliko tulionayo kama tupo pale kwa wizi wakura au kwa mabavu na hujuma na kulindwa na dola huku ndiyo kujivua magamba lakini nimeshangaa mwendawazimu mmoja huyo kaimu wa vijana bwana Shigela anasema uchaguzi ni halali hata wakitoa saa moja uchaguzi haurudiwi huu ni uhuni ccm inakuwa chama cha kihuni nani anampa ruhusa ya kutoa kauli zenye kuhatarisha amani kiasi hiki na viongozi wa chama mnakaa kimya Mkama unakaa kimya, Nnauye january mwenyekti wa chama unakaa kimya kwa kauri ya uhuni namna hii wakati sisi CCM tu watuhumiwa kama tumeiba kura mimi ninakaa Arusha kwa sasa wana ccm leo hii hatuifiki hata 30% ya wananchi wa arusha wenye hasira ya upatikanaji wa meya kinyemela wakiamua wanaenda kumtoa Meya kwa Nguvu CCM hatutaweza kuwazuia hata polisi hawataweza kuwazuia nguvu ya umma kwa hiyo mtutolee hao wahuni haraka kabla hawajakimaliza chama chetu tunahitaji watu kwa ajili ya kufikiri na wananchi wa sasa wanataka watu wanaofikiri kwa ajili yao sio kwa ajili ya ccm kwa sbb nusu ya watanzania hawana vyama na ni wapiga kura.Huyu Shigela hajui tunisia iliondoka madarakani kwa ajii ya kijana mmoja tu wa kimachinga alienyanyaswa na mgambo wa city ,tunataka watu wenye kufikri Meya wa arusha anaweza akasababisha chama tawala kikaanguka na kutolewa madarakani kwa nguvu ya umma kama chama kitaendelea kukumbatia wahuni wa aina hii.
  Naomba tujivue gamba la ukweli na sio hadaa hii ya siku 90 za rostam, chenge, na lowasa hii haina impact hata ya 5% kwa mwanacnhi aliyoko kijijini huko songea anaenunua sukari kilo Tsh 2000 na petrol Tsh2300.
  NAWAKILISHA
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  MMh sihui kama watakusikia umewapa maneno ya busara sana
   
 13. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kife mara ngapi? May be wakizike achana nao we need changes.
   
 14. z

  zamlock JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  ndugu yangu mpendwa aufai kuwa ccm njoo kwetu tupambane yani ningependa kukufahamu ukawa rafiki yangu na tushirikiane kuokoa taifa, shigela amenisikitisha na matamshi yake mpaka nimeshanga siyo hapo tu naupe anasema ccm ndiyo wameishauri serikali irudishe mswada ukafanyie marekebisho yan nimeshanga sana wakati wasomi wanaharakati na wanazuoni na vyama vya upinzani ndivyo vimepambana mpaka mswada umerudishwa eti ccm wanasema ni wao yani wamechanganyikiwa
   
 15. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #15
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wabunge 19 wa CCM ni batili kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya Tanzania; Je hilo nalo mmeliona ninyi sekretariat mpya????? Ninyi ndiyo mtaimaliza CCM na kuizika kabisa!!!!!!!!!!!!!!!!!CCM imezeeka, inanuka!!!!!!! Usanii utaiua CCM! Eleweni matatizo ya msingi na kuyatafutia ufumbuzi!!!!!!!!!!!!!! Mwalimu alitumia kweli kujenga CCM; msidhani waTz ni mazuzu tena!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 16. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #16
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanza napenda kukupongeza mtoa mada kwa hii habari na mada uliyo iweka apa janvn, najua wausika wote kama si wao basi wawakilishi wao uchangia na kusoma mada mbalimbali, nivizuri wasome mada hii na kuangalia kwa undani maslai ya watanzania zaidi kuliko chama na wenye. Wazolangu ni wao kujua kwamba sswatanzania tumechoshwa na huu ni mwisho wa CCM kutawala tanzania. kama wasipo jirekebisha kwa mambo wanaoyo fanya ikiwa ni kuvunja haki za binadamum tutashindwa kuvumilia na inaweza kuleta adhari kubwa sana katika jamii yetu ya tanzana.
   
 17. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #17
  Apr 17, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Well said mkuu, lakini sijui kama watakuelewa hawa majamaa yenye magamba mpaka machoni!!!
   
 18. Josephine

  Josephine Verified User

  #18
  Apr 17, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hongera sana.maneno yako nimeyapenda namuomba Mungu yawaguse wahusika.
   
 19. Granton

  Granton Member

  #19
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 5
  Nakupongeza sana kwa Maneno mazuri, Umenena kweli mkuu, ila tatizo la hicho chama cha magamba si wasikivu. Usishangae haya wakaja kuona ukweli wake baada ya miaka kumi...
   
 20. data

  data JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,786
  Likes Received: 6,558
  Trophy Points: 280
  Yaaanii ningekua na hela ningekutumia japo upate supu..... UMEONGEA KWELI TUPU...sasa wa TZ chakufanya jamani... tufunge mkanda ....tuwaondoe 2015... CCM ni chafu .. haiwezi kuwa safi. hata wajisafishe vipi.... Kama tuna akili timamu tujiulize tu ni kwanin walimvua SITA .. uspika.. JEMEDARI ALIYEKUA AKIPIGANA NA UFISADI BILA WOGA.
   
Loading...