Nape atakapohamia Chadema ......CCM ......!

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
View attachment 127400 images.jpg images (2).jpg View attachment 127408
5149024.jpg images (4).jpg images (1).jpg images (3).jpg

Kuna dalili za wazi Nape jitihada zake za kusafisha na kukijenga chama cha kisiasa kilichoshika dola nchini CCM kugonga mwamba kwa miaka kadhaa, huku jitihada zake zikionekana kugtoungwa mkono kila kukicha na baadhi ya vijana wenzake waliotegemewa kuwa pamoja katika vita hivyo kuamua kutangaza hadharani kuunga mkono mmoja wa wale vinara watatu waliotakiwa kujiondoa la sivyo wapewe barua wa kuwajibishwa ndani ya CCM jitihada ambazo ziliungwa mkono na aliyekuwa Katibu Mkuu kipindi kilichopita Mukama.

Nape anaonekana dhahiri kubaki peke yake katika safu ya juu kupigania anachokiamini kwani Katibu Mkuu wa sasa kuwa mwanasiasa zaidi ya ukweli wa maisha yake, historia yake pamoja na mazira ya nafasi aliyokirimiwa.

Mahojiano kwenye moja ya chombo cha habari karibuni Nape anaonekana kushangazwa na vyombo vya usalama kutofanya jitihada za uvunjaji wa amani na mauaji yenye utata katika mikutano ya hadhara kwenye mikutano ya vyama vya siasa na nyumba za kuabudia, serikali ikiunda kamati za uchunguzi bila kuja na majibu kitu ambacho amekitafsiri kama ni vyombo vinavyoundwa kuficha uozo wa kile kinachoendelea.

Hali halisi ya jitihada za Nape zinaonekana kugonga mwamba na pengine kubaki peke yake kati ya viongozi wa juu chamani wanaohangaikia kuondoa ufisadi kwa kukisafisha chama, na wale walio pamoja naye pengine ni kundi kubwa ambalo halina sauti ya juu ndani ya chama, matoke ni viti vya peke yake.

Anachokipigania Nape ndani ya CCM kifalsafa hakitofautiani na kile kilichomo ndani ya sera zinazoimbwa na kuhubiriwa na Chadema katika mikutano yao na katika jopo lao kwa jukwaa la chama cha upinzani bungeni.

Nape alionekana kuwa na sauti ya kusikika mbali siku za nyuma kuisimanga Chadema na viongozi wake, siku za karibuni ameonekana kuwa mpole, si dalili wazi kwamba yuko likizoni ingawa anaendelea na mikutano kuzunguka sehemu mbalimbali nchini, kuna dalili ya kuafiki jitihada za wahasimu wa CCM ambao ni Chadema, jambo ambalo hawezi kuliweka wazi kwa vile atakuwa amefanya makosa makubwa kwa vile yeye ndiye msemaji mkuu wa chama cha CCM kwa sasa ingawa damuni mwake kuna dalili za wazi za kuwa na chembechembe nyekundu na nyeupe za Chadema.

Siku Nape atakapotangaza kuchoshwa na CCM na kuamua kujiunga na makamanda wa M4C dhoruba yake ndani ya CCM italeta mafuriko makubwa ambayo CCM itashindwa kuhimili kishindo hicho kuliko wale ambao CCM inawatumia kudhofisha upinzani toka ndani ya ngome ya upinzani.
 
Mkuu akija chadema huyo dogo atapokelewa kama mwanachama wa kawaida tu kwasababu kura yake tunahiitaji sana.

Ila nafasi ya uongozi asahau kwani huku watu kichwa box hawaitajiki kabisa. Tunahitaji vichwa kama kina Mnyika
 
Ndoto za asubuhi vipi umeshafika Ufipa kusaini?

Tatizo lenu hamwezi kusoma ishara za nyakati, kwamba mvua huwa hainyeshi bila mawingu kutanda, sasa mawingu yanapoanza kusogea ninyi mnashindwa kusoma kwamba mvua inakaribia kunyesha.

Nilipokuwa mdogo niliona wazee wakishaanza kusikia aina fulani ya ndege huko porini walisema majira ya mvua ni karibu, kwani kwao hawakuwa na kalenda isipokuwa kulikuwa na viashiria kadhaa na ilikuwa kweli wakiimba ndege hao zinabaki wiki chache tu mvua inaanza kunyesha.

Tatizo lenu mnashindwa kusoma viashiria kadhaa na pengine kwa kupuuzi baadaye mtajutia.
 
Tatizo lenu hamwezi kusoma ishara za nyakati, kwamba mvua huwa hainyeshi bila mawingu kutanda, sasa mawingu yanapoanza kusogea ninyi mnashindwa kusoma kwamba mvua inakaribia kunyesha.

Nilipokuwa mdogo niliona wazee wakishaanza kusikia aina fulani ya ndege huko porini walisema majira ya mvua ni karibu, kwani kwao hawakuwa na kalenda isipokuwa kulikuwa na viashiria kadhaa na ilikuwa kweli wakiimba ndege hao zinabaki wiki chache tu mvua inaanza kunyesha.

Tatizo lenu mnashindwa kusoma viashiria kadhaa na pengine kwa kupuuzi baadaye mtajutia.

CCM itatawala miaka 800
 
Mkuu CS

Niliwahi kuandika makala hii hapa chini, huu utabaki kuwa ndio mtazamo wangu kwa siasa za ccm.


Ni asubuhi na mapema, anga likiwa na makunyanzi,huku magimbi yakitanza kwa ukelele na rangi ya kahawia inalitanda anga,

Nyuso za magwiji wa falsafa za mlengo wa kati na hekima ya utawala wa nera zimeshamiri tabasamu mwanana kabisa,

Ndio ni tarehe ileile ya 05/02/1977 siku tukufu kwa wahafidhina wa CCM, nasema ni tukufu kwakuwa wazalendo wa leo hawaamini kuwa ungano lile la saa nne mchana wa 05/02/1977 leo ndilo hili walionalo leo!

Chama cha TANU kikiwa na nguvu thabiti na kikiwa ni miongoni mwa vyama vyenye nguvu barani Afrika, kiliamua kwa kauli moja kuungana na Chama cha Kizalendo/cha weusi ambacho ni kikongwe zaidi barani Afrika cha ASP,

Hilo lilitimia baada ya Muungano wa nchi mbili huru yani Tanganyika iliyopata Uhuru chini ya Shujaa wake Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Zanzibar iliyopata uhuru wake kupitia MAPINDUZI matukufu chini ya Shujaa wake John Okello (Fiel Marshal) lakini kipindi cha muungano Zanzibar ilikuwa chini ya Sheikhe Karume mkubwa,

Ni zama ambazo bara la Afrika lilishuhudia chama cha siasa imara kikizaliwa katika ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara katika ardhi ya Tanzania mpya, chama kilichokuwa na nguvu ya kiushawishi, nguvu ya kiuchumi, na nguvu ya kijasusi!

Chama ambacho kwa msaada wacho kiliyaweka huru mataifa yote ya kusini mwa Afrika, hakuna nchi ya kusini mwa Afrika ambayo haikupita mikono mwacho, laa isingepata uhuru kwa wakati!

Si chama kingine bali ni mvumo wa alama ya kijani na njano, tokezo sahihi la Chama Cha Mapinduzi!

Kwa uimara wake, Tanzania palikuwa mahali pa sauti kuu ya mwafrika, Tanzania ilikuwa na SAUTI mbele ya UNO juu ya mambo mengi hasa UHURU kamili wa Mwafrika,

Kuingia kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa hasa baada ya kupigwa mweleka kwa Azimio la Arusha mwaka 1992 na kuzaliwa Azimio la Zanzibar, kulileta mageuzi mapya ya chama hii,

Sura na hadhi ya chama ilizidi kutia nyongo miongoni mwa wahafidhina hasa baada ya mabaka uchumi kujitwalia sauti na nguvu ya chama,

Lakini magwiji wa siasa zile walipotangulia tu mbele ya haki, mizani ya chama hii imekuwa ikipinda siku hadi siku,

Uchaguzi wa 2010 ulikuwa ni taswira halisi ya chama kubakwa, na wabakaji walidhamiria hasaaa na wamefanikiwa, mabaka uchumi yaliamua kuchota pesa hazina ya serikali (ya wanachi) na kutumbukiza katika uchaguzi huo yakipanda mtu wao wakulinda maslahi yao,

Hakika yalifanikiwa, pesa ilichotwa kupitia mlango uitwao EPA, na yakamuweka mnadhiri wao Ikulu, na hakika maslahi yao yanalindwa kama yalivyo maagano yao!

Hilo liliendelea kuwa angamizo kwa chama adhimu cha CCM, kwa mpasuko ndani yake uliendelea kuongezeka huku chama kikiacha majukumu yake stahiki na kugeuka KAMPUNI la biashara,

Bahati mbaya iliyoje kwa ccm, kwani licha ya kugeuzwa mgodi wa wajanja, bado kiliendelea kukubwa na dhahama ya karne hasa kwa chama kugeuka kuwa NGOs ya familia ya Mwenye Jamuhuri, Baba kashika Jumuiya ya Wazazi, Mama kashika Umoja wa Wanawake, na Mtoto kashika Umoja wa Vijana,

Hakika hapa wahafidhina ndipo walipokamatwa, hakuna pakufurukuta kata kugeuza ukope tu, ukitibuana na The Princess ujue umetibuana na Mwenye Jamuhuri, na ukitibuana na Bimkubwa ujue hulambi unga hata cheme ya haradali,

Mungu wangu!, huenda ndio kifo kiliita ccm yangu,

Kibaya zaidi mwenye kiti wa chama aliamua kupanga safu yake ya Uongozi baada ya Uchaguzi wa 2010 kwa kumpiga chini Yusufu Makamba na kuleta sura azitakazo ambazo kimsingi zingemsikiliza matakwa yake, naaam aliingia bingwa wa falsafa za kale za Kingwanamalundi, huyu kwa asili ni mtaalamu wa njama za siri na ni jasusi muhitimu mikononi mwa Julius Nyerere kama aliyo Yusufu Makamba, tofauti yao ni moja tu, Mkama ni mtaalamu wa mikakati ya siri aliyefuzu mafunzo ya kijasusi ipasavyo, Yusufu Makamba ni mtaalamu wa ujasusi wa kipropaganda aliyebobea na kuiva ipasavyo kutoka Mosco,

Katika siasa za leo huku chama kikizidi kutoweka mioni mwa Watanzania, Chama kilihitaji mtaalamu wa propaganda aliyebobea ipasavyo, na kilihitaji mtaalamu wa njama za siri mwenye kutembea katika lengo mahususi,

Lakini kumtoa Makamba na kumuweka Mkama lilikuwa kosa la karne, kwakuwa chama kilikuwa kwenye mfumo wa Analogi na kilihitaji kuingia katika mfumo wa Digitali ambamo vyama makaini vya mageuzi ya pili vimo,

Kama vile mungu ameandika kifo kwa ccm mikononi mwa Jakaya Kikwete kabla ya 2015, chama kilifanya mabadiliko tena ya uongozi na kurudisha "makapi" ya kale na si mwingine ni Abdulahiman Kinana mtanzania mwenye ASILI ya "KIGENI" RAIA wa Somalia,

Malengo ya mwenyekiti ni kutumia taaluma ya Kijasusi ya Kinana katika siasa mpya, lakini akisahau kuwa filosofia ya Kinana na Mkama ni moja kasolo hulka zao tu,

Kinana amekuja na aina mpya ya siasa za Tanzania, hasa kwa kuruhusu na kushinikiza vyombo vya Dola kutawala siasa za CCM, leo mwanaccm hawezi kuzungumza chochote bungeni bila kupewa maelekezo na Idara za Usalama za nchi,

Lakini hilo tisa, kumi ni pale chama kilipowaingiza vijana ambao hawajapevuka kiakili katika uongozi wa juu wa chama, lengo la CCM lilikuwa zuri sana kama lingelenga watu sahihi katika nafasi hizo kwakuwa hawa wangekuwa ni kiungo kati ya kundi la vijana nchini ambalo ndilo linalotawala karibu 98% ya wahanga na waamuzi wa siasa za nchi hii, Watu hao si wengine bali ni Mwigulu Nchema na Ndugu Nape Nnauye,

Hawa kwa political meker wa ccm alilenga kuwa wawe kiunganishi cha vijana wa Kitanzania, lakini matakwa na chaguo la Mwenye Jamuhuri ni ANGAMIZO kwa CCM na kwa NCHI kwa ujumla,

Wamegeuka kuwa ni maadui wa vijana wa kitanzania, hata wale vijana ambao hawakuwa na uamuzi wa haraka wa kuamua waende chama gani cha siasa wamejikuta wanaichukia CCM hata kabla hawajaamua pakwenda,

Leo taifa limesimama wima linastaajabu kuona ccm imeamua kutawala kwa damu dhahiri shahiri, siasa za majukwani na vitendo vya vijana hawa Mwigulu na Nape vinaliyumbisha taifa, wamekuwa na mamlaka makuu kuliko hata mwenye Jamhuri, wanaamrisha vyombo vya dola watakavyo,

Mauaji yametabakaa kila kona ya nchi, na yote chanzo ni siasa za nchi hii, manyanyaso kwa vyama vya upinzini yamekomaa kiasi cha kutishia usalama wa taifa hili hivi sasa, lakini yote haya ni ni siasa za majukwani za ccm kushindwa kushawishi Watanzania na sasa Watanzania wanalazimishwa kwa mtutu wa bunduki kuikubali ccm na maovu yake yote!

Bahati nzuri watanzania wanasema wazi hapanaaaaa! Hawataki siasa za damu, hawataki kumpenda mtu kwa lazima, hataki kudanganywa tena, hawataki raslimali zao kuibwa tena,

Wataka huduma bora na maisha bora huku raslimali zao kikilinufaisha taifa na vizazi vyao vya kesho!


Taifa linayumba kwa siasa CHAFU za CCM, tumekuwa kituko mbele ya uso wa dunia, taifa linanuka DAMU ya binadamu, taifa linaomboleza kila uchao,

Lakini waratibu na wauaji tunao mitaani, serikali haichukui hatua, na zaidi inabariki kwakusema "wapigini tu tumechoka"


Kwa muktadha huo chama cha cha siasa chenye mlengo wa fikra za mageuzi ni Chadema, na kimefanikiwa kubeba tumaini la Watanzania karibu wote, labda tu wale wahafidhina vipofu wa ccm!


Watanzania wanao uchaguzi wao wenyewe, wakuamua ama kuishi katika damu ama kuishi katika ukombozi mpya,

Mwenye macho haambiwi tazama!
 
CCM itatawala miaka 800

Tunatakiwa kupanda kiwango cha kujadili, dhana ya kuleta mada kuna viashiria vilivyonisukuma kufanya hivyo, kama waviona viashiria hivyo si sahihi, lete hoja zenye kuonyesha unalofikiria kuhusu Nape, mimi sijaweka mada ya CCM itakuwa madaraka kwa muda gani, kama una hilo la muda wa CCM kuwepo madarakani anzisha mada tutaijadili, usiyumbishe maudhui ya mada.
 
ni mchapakazi mzuri, tatizo ni mfumo anaofanya nao kazi hauwezi kwenda naye. Ajitahidi kabla hajahamia ule mradi wa 7000 lumumba urudishiwe fahamu zake ili uandike kinachostahili badala ya ilivyo sasa.
 
Back
Top Bottom