Nape asema Korosho ipo ICU Kuna watu lazima wawajibike au kuwajibishwa

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,876
7,366
Dodoma. Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema zao la korosho liko chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) na kutaka mkakati wa ununuzi wa zao hilo kupitiwa kwa makini.

Waziri huyo wa zamani wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Mei 20, 2019 bungeni jijini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo mwaka 2019/2020 na kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua udanganyifu wa mauzo ya korosho.

Amesema waliohusika kwenye udanganyifu wa mauzo ya korosho wawajibike wenyewe vinginevyo atapeleka kusudio la namna ya kuwawajibisha.

Amesema baada ya ukaguzi huo wa CAG taarifa ipelekwe bungeni ijadiliwe kwa maelezo kuwa kinachoelezwa kuhusu ununuzi wa korosho ni uongo.

"Nia ya Rais ilikuwa njema kabisa lakini waliokwenda huko wamefanya mazonge na mambo ya hovyo, hapa tukubaliane siyo Serikali yote imeharibu bali wako waliofanya mambo ya hovyo, ni vema wakawajibika ama kuwajibishwa," amesema Nape.
Mbunge huo amesema waziri wa Kilimo na naibu wake hawahusiki katika sakata la korosho, kwamba wapo wanaotakiwa kuwajibika.
 
Mbona anapiga danadana kuhusu nani awajibishwe?

Amesema waziri asiwajibishwe wala naibu wake ambao tungesema ni prime culprits kwenye sakata hili.
ukiwaondoa hawa 2, prime culprits waliobaki ni wajeda na amiri jeshi wao mkuu... sasa Nape anashindwa nini kuwataja hawa directly??
 
mbona anapiga danadana kuhusu nani awajibishwe?

amesema waziri asiwajibishwe wala naibu wake ambao tungesema ni prime culprits kwenye sakata hili.
ukiwaondoa hawa 2, prime culprits waliobaki ni wajeda na amiri jeshi wao mkuu... sasa Nape anashindwa nini kuwataja hawa directly??
Nadhani amemlenga Prof Kabudi aliesaini mkataba na kampuni ya wakenya

Waziri wa katiba na sheria
 
Kuna kitu anatafuta huyu kijana wa mtama
Ajifunze kutulia kama Gullo Shumbi
 
Ha ha ha, you are strangled. Kimewakaba rohoni. Mnataka kusema kitu lakini hamwezi. Kaeni tu kimya.
 
Wa kwanza ni mwanachama mwenzie wa ccm na mkuu wake ,huwa anajiita jiwe au kichaa huyo awe wa kwanza
 
Aliyeifikisha 'Coral show' ICU ni magu aliyeamuru inunuliwe toka kwa wakulima wa style hiyo. Labda angemsikiliza PM badala ya alivyomfanya hadharani, hii activity ya 'Coral Show' isingefikia katika halihiyo. Nape aache kumung'unya maneno!

Back
Top Bottom