Nape asema CCM itatangazwa MSHINDIi Kimandolu

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,182
2,304
Katika Kampeni za uchaguzi wa Diwani Kata ya Kimandolu hapa Arusha NapeMnauye amesema hakuna "HAKUNA JINSI NI LAZIMA MGOMBEA WA CCM ATANGAZWE MSHINDI'.
Hii ni katika hotuba aliyomaliza dakika 10 zilizopita hapa CORNER BAR Kijenge juu kata ya Kimandolu. Nape amesema ikiwa kutatokea fujo akikamatwa mtu na green guard atashughulikiwa kwanza kwa masaa 3 kabla ya kumkabidhi Polisi kwa sababu wanaona Polisi hawawezi kuwashughulikia ipasavyo.

Hofu imetanda kwani ni mara mbili CCM wamesema Edna lazima atangazwe mshindi na vijana wa CCM watalinda kura hadi mwisho. Ajabu ni kwamba WEZI NAO WANAIGIZA KULINDA VITU VYAO HATA KAMA HAKUNA MWIZI. Kama CCM watalazimisha ushindi watakuwa wamefanya jaribio baya ambalo matokeo yake yatakuwa na athari mbaya ambazo zitaepukika kama kila mtu atakubali kura ziamue mshindi. Baadaye nitawarushia picha na video za Nape akijikaanga.
 
Asante sana mkuu kwa taarifa ya msingi sana.
Ni wakati wa makamanda hapa Arusha kujipanga kupambana na hila za CCM na serikali yake kwa umakini na haraka sana.

Mbinu zilizotumika na CHADEMA kudhibiti hila za CCM wakati wa marudio ya uchaguzi wa Arumeru mashariki na Kata ya Daraja mbili ni lazima zitumike tena hapa Arusha.

Kuna mbinu chafu kadhaa CCM wamepanga, soon nitazieleza hapa.....
 
Amesema G.Lema ni kichaa na anakunywa viroba kabla ya kupanda jukwaani; hii imeniudhi sana kwani kwa mtu anayejidai anao ufahamu na busara huweza kunadi uzushi badala ya sera.
Tumemsikiliza akiongea mambo ya kijiweni bila kuonyesha kama anajua tatizo lolote la wana Kimandolu
 
Polisi ongezeni risasi maana sisi kama chadema hatutakubali uhuni wowote wa CCM na polisi.....na Nape Mwadosya awaulize hao green guard wake moto wa chadema Arusha..
 
Hata vichaa huwa wanaringa wakiwa wamebeba mafurushi yao, mwacheni nape aringie ukichaa wake
 
Amesema G.Lema ni kichaa na anakunywa viroba kabla ya kupanda jukwaani; hii imeniudhi sana kwani kwa mtu anayejidai anao ufahamu na busara huweza kunadi uzushi badala ya sera.
Tumemsikiliza akiongea mambo ya kijiweni bila kuonyesha kama anajua tatizo lolote la wana Kimandolu

Kwa jinsi alivyoropoka uwongo uliopitiliza lazima atakuwa ameongeza hasira za wananchi wa kimandolu, ambao wanamfahamu Lema hatumii kilevi cha aina yoyote!
Tatizo ccm wanashindwa kujua jinsi ya kutoka Arusha!
Wamejiharibia wenyewe!
Hawa ccm wangekuwa na akili at least wangewateua watu wafuatao kugombea kata za Arusha!
1. Benjamin Mkapa - Kimandolu
2. Ally Hassan Mwinyi - Elerai
3. Jakaya Kikwete - Themi
4. Nelson Mandela - Kaloleni

Hapo wangeambulia japo hata kata moja ya Kaloleni!

Lakini hivi walivyo imekula kwao mazima!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hahaha masihara hayo kamanda Mungi. Hao watatu wanamuogopa sana Lema kiasi cha kutokubali uteuzi.
 
Last edited by a moderator:
Polisi ongezeni risasi maana sisi kama chadema hatutakubali uhuni wowote wa CCM na polisi.....na Nape Mwadosya awaulize hao green guard wake moto wa chadema Arusha..

Mbona yale maeneo ambayo CCM inakubalika hawafanyiwi fujo? Hao green guards kwa nini wanawapeleka maeneo ambayo CCM hawakubaliki na kuanzisha fujo? Mie naona hao washughulikiwe kama vibaka wanavyoshughulikiwa maana inaonyesha Polisi wetu wanawatambua kama jeshi halali la CCM na pengine wamelisajili kimya kimya
 
Back
Top Bottom