DR. MWAKABANJE
JF-Expert Member
- Nov 7, 2012
- 1,976
- 3,122
Ni kwa muda mrefu sasa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa kikilalamikia tabia ya CCM kuingilia chaguzi mbalimbali nchini kama vile chaguzi za mameya wa majiji na manispaa kama ilivyotokea Arusha na Mwanza.
Hivi karibuni kuliibuka mgogoro mkubwa kati ya CHADEMA na CCM, juuu ya uchaguzi wa meya wa manispaa ya ilemela ukiachiliambali mgogoro mwingine wa mipaka ya halmashauri ya manispaa ya ilemela, mgogoro huo pia ulipelekea baadhi ya madiwani wa CHADEMA kuwekwa rumande kwa sababu eti walikiuka maagizo halali ya mahakama ya kuwataka kusitisha uchaguzi wao wa ndani ya kumteua mgombea wa umeya wa ilemela bila ya kuwepo diwani mwingine Henry Matata ambaye alikuwa alisimamishwa uanachama na kamati kuu ya Chadema hivyo kukimbilia mahakamani hivyo kuendelea na wadhifa wake wa udiwani, nadhani hakuna haja ya kuyaongelea mengi juu ya matata kwani mengi yamekwisha semwa kwenye jukwaa hili.
Sasa basi juzi tu Katiku wa itikadi na uenezi wa ccm Nape, alikuwa akihojiwa na kituo kimoja cha redio cha METRO FM cha jijini Mwanza kinachosemekana kumilikiwa na kada maarufu na tajiri mkubwa Gachuma, pamoja na mambo mengine nape aliulizwa kuwa kama ni kweli CCM ilishiriki kuhujumu uchaguzi huo kama inavyolalamikiwa na wengi hasa CHADEMA, alisema "ndiyo CCM tulimteua matata agombee umeya wa ilemela na naibu meya atoke ccm ili kuondoa hali ya kisiasa iliyokuwepo ili kulete maendeleo".
kwa maneno machache haya ya nape, inaonyesha bila shaka yoyoyte jinsi CCM wanavyokiuka misingi ya Demokrasia na utawala bora kwa kujiuliza maswali yafuatayyo:-
1. inaonyesha ni jinsi gani wamekuwa wakivuruga chaguzi hizi na kutuletea maafa kama yale ya Arusha kwani hata sheria za uchaguzi zilikiukwa wakati wa kumchagua meya huyu (idadi ya wajumbe).
2. Inaonyesha jinsi ambavyo wamekuwa wakiingilia mihimili ya dola kama mahakama kwani Nape anatuonyesha jinsi gani ambavyo inaonyesha wallingilia hata maamuzi ya mahakama ya kuwakamata madiwani wa CHADEMA kwa maslahi yao.
3. Mwisho, bila shaka yoyote ametueleza wazi kuwa diwani matata ni wa CCM na wala si wa mahakama kama yeye anavyojiita, na pia kwa kiasi kikubwa hawakilishi wananchi waliomchagua kwani hakuchaguliwa na idadi ya wajumbe inayotambulika kisheria.