Nape: Ardhi ikimilikiwa na watu binafsi wanyonge watataabika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape: Ardhi ikimilikiwa na watu binafsi wanyonge watataabika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Jun 7, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  NAPE:ARDHI IKIMILIKIWA NA WATU BINAFSI WANYONGE WATATAABIKA

  Ataka umiliki ardhi uendelee kuwa chini ya serikali

  Asema wanapiga hilo ni mabepari

  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kusiistiza juu ya msimamo wake wa ardhi kuendeleakumilikiwa na serikali kwa maslahi ya taifa zima.

  Msimamo huo ulielezwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Turbo mjini Njombe. Nape alisema, tofauti na mapendekezo ya baadhi ya vyama vya siasa kwamba ardhi imilikiwe na wananchi, CCM inaona kwamba bado kuna ulazima wa ardhi kuwa chini ya miliki ya Serikali, kwa sababu kuwafanya hivyo kuna faida kubwa zaidi.

  "Sisi Chama Cha Mapinduzi, baada ya kutafakari kwa kina, katika rasimu yetu kuhusu katiba mpya ya Tanzania tumependekeza pamoja na mambo mengine, kwamba ardhi iendelee kumilikiwa na serikali kwa sababu tunaona kwamba utaratibu huu ndiyo unaifanya ardhi kuwa mali ya wanancho wote", alisema Nape.

  Alisema, madhara ya ardhi kumilikiwa na watu binafsi katika nchi ni jambo la hatari sana, kwa sababu inaweza kumilikiwa na mabepari wachache hata wasiozidi wanne nchi nzima kama ilivyo katika baadhi ya nchi jirani hatua inayowafanya raia kulazimika kuwapigia magoti mapepari wanapohitaji hata eneo dogo tu kufanyia shughuli zao.

  Nape aliwataka Watanzania kuunga mkono hoja ya CCM ya kuendelea kuifanya ardhi kuwa chini ya miliki ya watu binafsi na kuachana na ile ya Chadema inayosisitiza kutaka ardhi imilikiwe na watu binafsi.

  "Hawa Chadema wanatetea umiliki wa ardhi kuwa chini ya watu binafsi kwa sababu wana maslahi nalo, maana tunajua mwanzilishi wa chama chao ni mmoja wa matajiri wanaomiliki ardhi kubwa sana hapa nchini, sasa wanapendekeza hivyo ili mwanzilishi huyo wa chama chao asije akapokwa eneo hilo baada ya katiba mpya kutoa maelekezo kwamba ardhi ni mali ya umma kupitia umiliki wa serikali", alisema.

  Katika hatua nyingine, Nape amewataka watendaji wa mkoa mpya wa Njombe wanaohusika na upimaji viwanja, kuhakikisha wanafanya kazi hiyokwa kuzingatia haki ili kusitokee malalamiko kwa yeyote kunyimwa eneo kwa hila yoyote.

  Nape alisema, kupima vbiwanja kwa kuzingatia haki kutawezesha kila mwananchi kupata eneo analohitaji kulingana na sheria, lakini isipozingatiwa hivyo, wanyonge hawatapa ardhi kwa kuwa haki isipozingatiwa ni matajiri tu ndio watakaopata maeneo tena makubwa sana.

  "Mimi kama msemaji wa Chama Cha Mapinduzi kilichiunda serikali iliyopo madarakani, nawaagiza viongozi wa mkoa huu mpya tangu wa serikali na wa CCM ngazi zote, kuwa makini na hili kwa sababu ardhi ni miongoni mwa mambo ambayo huzusha sana migogoro jambo ambalo hatutaki kabisa litokee hapa", alisema.

  Akizungumzia uhai wa Chama Cha Mapinduzi, Nape alisema, CCM bado ni imara kutokana nna misingi yake, na itanedelea kutawala tangu jana, leo na kesho kwa sababu ya misingi hiyo, hivyo wana-CCM waendelee kutembea kifua mbele. Nape aliwataka wana CCM nchini kote, kupuuza propaganda za baadhi ya vyama vya siasa za kujaribu kuonyesha kwamba CCM imechoka kuwatumikia wananchi.

  "Si kweli kwamba CCM imechoka, bado ni imara na ndiyo maana kila mara tumekuwa tukifanya mageuzi kuhakikisha kinaenda na wakati, na kutokana na mageuzi tuliyomo sasa nawahakikishieni kwamba baada ya uchaguzi ndani ya chama mwaka huu, CCM itakuwa chama bora zaidi kuliko chama chochote cha siasa Tanzania na duniani kote", alisema na kuongeza;

  "Katika uchaguzi huo, CCM itahakikisha mafisadi na wala rushwa na wasio na uzalendo kwa nchi hii, hawapenyi na kujiingiza katika uongozi, kwa sababu atakayebainika kujaribu kutumia rushwa kujipenyeza ili apate uongozi wakati si msafi na hana sifa tunazotaka tutamshughulikia kwa nguvu zote.

  Aliwataka wana CCM kuhakikisha fursa ya uchaguzi ndani ya Chama unaofanyika mwaka huu, kuitumia vizuri ili kukifanya chama kiwe imara zaidi kwa manufaa ya taifa akinukuu kali ya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwamba

  "Bila CCM Makini Nchiye Itayumba'.
   
 2. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kwani nyumba za serikali walizozimilikisha kwa mafisadi binafsi sio kuwajali wananchi? Nonsense

  Sasa kama CCM ni imara yeye anaimarisha nini? Aache kudhurura carolite itamletea cancer na jua
   
 3. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Mbona nyumba za serikali tena Prime area walimilikishana mabepari hajarudisha?
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Je inapomilikiwa na wawekezaji wa kigeni nani anataabika?
   
 5. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Nape anajichanganya, mara aseme ardhi iwe chini ya milki ya serikali at the same time anasisitiza ugawaji wa ardhi kwa wananchi.
  Nnauye jr, hivi unajua by virtue of land and act kuwa ardhi yote ya Tanzania ni mali ya nani??
   
 6. t

  the horse JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 578
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Anasisitiza hili liendelee kwenye katiba ijayo..,kwa kuwa wengine wa CHADEMA wana maono tofauti ya suala hili.
   
 7. t

  the horse JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 578
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Nchi hii inawanyonge wengi kuliko matajiri, hatuwezi kuacha wanyonge hawa wajute kuwepo katika nchi moja na matajiri.
   
 8. MANI

  MANI Platinum Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Umiliki wa ardhi kwa wananchi ni kupitia serekali za vijiji hilo ndilo lengo la CDM. Sasa yeye anaona ubaya gani kwa ardhi kumilikiwa na serekali ya kijiji?
   
 9. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Nape, tafadhali katika suala la ardhi, usiweke siasa! Hili ni jambo kubwa. Mfumo uliokuwepo sasa sio mbaya na hata kama ingebidi kubadilika ukawa kama unavyodai chini ya wananchi kwa maana 'private property' bado kuna mianya mingi ya kuendeleza matatizo na changamoto tulizo nazo katika sekta hii. Tatizo sio Mfumo kama Mfumo! Tatizo ni ukosefu wa maadili katika kazi, na wala sio kwa watendaji kazi katika idara hizo, bali kwa wanasiasa kuingilia na kudai wao kama waheshimiwa wana mamlaka ya kutengua na kugawa ardhi.

  Nina mifano mingi sana ambapo madiwani, wabunge, viongozi wa juu wa serikali wameingilia maafisa ardhi na kulazimisha kutwaliwa ardhi kutoka kwa mwananchi ili amilikishwe kiongozi au mfanyabiashara. Ofisi ya Raisi imetumiwa vibaya sana katika masuala ya ardhi. Hawa wasio na maadili wanapozidiwa kwa hoja na watendaji hukimbilia aidha kwa Waziri au Raisi ambaye hutengua maamuzi sahihi ya watendaji. Ndio maana maeneo kama ya Kawe Tanganyika Packers yalipoanza kumwegwa utakuta waliofaidika ni watendaji wakuu(wanasiasa serikalini- nenda tafuta nani anakalia zile ardhi za pale) na hata maeneo yanayozunguka kanisa la Kilutheri pale Tangi Bovu(eneo lililokuwa miliki ya Kiwanda cha Bia Tanzania).

  Watani wako wanapolilia kuondoa madaraka ya Raisi katika miliki ya Ardhi, wanafanya hivyo wakiamini itaondoa ile 'discretion' anayoitumia mara kwa mara kuwanyanganya wananchi Ardhi. Kule Moshi, uongozi wa Nchi ulimilikisha mfanaya biashara eneo la shamba likiwa na nyumba dhidi ya Chama Cha Ushirika, baada ya mfanyabiashara huyo kutokulipa kodi ya sehemu aliyokodishiwa kwa zaidi ya miaka 15(na huyu mmfanya biashara ni kada wa CCM, ni rafiki mkubwa wa wakubwa katika Chama na Serikali). Lakini kwa mtazamo wangu, bado sio Mfumo ila ni uadilifu unakosekana.

  CCM mlipoanza kuzungumza kujivua Gamba nilipata picha nzuri kwamba walau kuna mtu ameona haja na nia kubwa ya kurejea katika maadili, lakini Nape unavyolielekeza hili (vita ya kujivua gamba) kisiasa na kutazama kila kitu kwa macho ya watani wako, UNANITIA SHAKA, UNANIOGOPESHA! Ukitaka kuzungumzia mambo ya maendeleo, yazungumzia kimaendeleo na sio kimpasho- unadhani Mtei anaongoza bado CDM?
   
 10. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,380
  Likes Received: 317
  Trophy Points: 180
  "ccm itahakikisha mafisadi na wala rushwa na wasio na uzalendo kwa nchi hii hawapenyi na kujiingiza katika uongozi".
  We Nepi hivi Chenge aka mzee wa chenchi kachushinda kiti cha kamati gani vile???acha uongo na zile siku 90 hadi leo hazijafika tu???
   
 11. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nape hajui asemalo mkulu anazurura huku na huko kutafuta wawekezaji kwenye kilimo kwanza na juzi huko Arusha alidai "Tanzania is ready to do business" sasa hao wawekezaji watalimaje bila kumilki ardhi? Ni vigumu kuamini hawa ccm wajinga wametawala miaka 50
   
 12. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huwa nikiona mantiki za huyu bwana mdogo huwa napata kizunguzungu,hivi una maana gani kusema kuwa mwanzilishi wa cdm mtei anamiliki ardhi kubwa wakati katiba ya sasa na sheria zote zinataka ardhi iwe chini ya rais.Je wakati mtei anaipata hiyo ardhi kubwa hivyo huyo rais wenu alikuwa wapi?.ninajua watu unaokuwa unawahutubia ni wale unaowapa wali kabla ndio maana onaongea mantikiless kiasi hiki..............................
   
 13. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kama hiyo kwenye red imesemwa na Nape, naomba aje hapa aitolee ufafanuzi zaidi.
  Kitu kimoja ni kusema "kama mwanasiasa", nyengine ni kuona utekelezaji kwa vitendo kile mwanasiasa anachohubiri. Kwa ninavyojua sasa umiliki wa ardhi ni kwa mwenye uwezo wa kifedha na/au kiuongozi. Tunaona viongozi wengi na watu wenye fedha wanamiliki, kujimilikisha na kumilikisha ardhi. Serikali ya CCM, itasemaje kuhusu uuzaji wa ardhi kwa wanaojiita wawekezaji?

  Huwa ninapata mashaka ninapoona wabunge CCM wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kudai eti Wakenya wanataka ardi yetu wakati serikali inagawa ardhi hiyo hiyo kwa wageni. Ama kweli siasa ni mchezo mchafu.
   
 14. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  None sence, mnataka mmiliki ardhi ili muwauzie mafisa?:A S 20: hatawaamini.
   
 15. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Nape aliwataka Watanzania kuunga mkono hoja ya CCM ya kuendelea kuifanya ardhi kuwa chini ya miliki ya watu binafsi na kuachana na ile ya Chadema inayosisitiza kutaka ardhi imilikiwe na watu binafsi.

  "Hawa Chadema wanatetea umiliki wa ardhi kuwa chini ya watu binafsi kwa sababu wana maslahi nalo, maana tunajua mwanzilishi wa chama chao ni mmoja wa matajiri wanaomiliki ardhi kubwa sana hapa nchini, sasa wanapendekeza hivyo ili mwanzilishi huyo wa chama chao asije akapokwa eneo hilo baada ya katiba mpya kutoa maelekezo kwamba ardhi ni mali ya umma kupitia umiliki wa serikali", alisema

  mkapa ana hekari 2000 Morogoro

  Mwinyi ana hekari 1000 Morogoro

  Sumae ana hekari 500 Morogoro

  Riz Moko ana viwanja kibao Burka Arusha

  Mzee Bati ana maranch kibao Nchi Nzima.

  Hayo ni wanachama na viongozi wa chama gani???????

  Nepi ni kipofu.

  Nape njoo jibu hizi kwanza

  Wakati wa budget ya 2011/12 Mh Halima Mdee aliwataja, na Mama Tibaijuka akaahidi zitarudishwa na wananchi wanaotaka kulima watapewa.

  Je Nyinyiem si waongo, watapeli?

  Sasa mwananchi wa kawaida akitaka ardhi atapataje ili ajiajiri?

  Vijana wanazurura mitaani, lakini ardhi wanapewa Vigogo na mabepari wa nje ya nchi.

  Mabepari wa nje wanawapa viongozi wa serikali ya Nyiyiem 10%

  Kwanza Nape anza na viongozi wako kwanza, safisha serikali yako kwanza. Achana na CDM.
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,791
  Trophy Points: 280
  mafisadi yanatuzuga haya
   
Loading...