Nape aonja joto ya jiwe zomea zomea..

Earthmover

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
22,711
19,929
Makamanda Habari za jioni…

Leo katika kata ya Erelai kulikuwa na mikutano miwili moja wa ccm na mwingine wa Chadema ambao ulikuwa na nyomi ya kutosha na ule wa ccm kama kawa kikundi cha watu wachache.

Wakati mkutano wa Chadema ukiendelea katika shule ya msingi ya Azimio ghafla msafara wa Nape ulipita.Kabla ya kupita takribani kama mita 300 kutoka eneo la mkutano msafara huo ulisita kupita mfano wa mtu kukutana na simba. Jamaa kuogopa aibu ya kugeuza msafara wao ilibidi wapite kwa aibu.Walipokuwa wakipita zomea zomea huwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii na vilio vingine vililipuka kutoka eneo la mkutano mfano wa kiumbe cha ajabu kikipita!!! Zomea zomea hiyo iliwachukiza jamaa hao wa ccm na kuanza kuonyesha ishara ambazo hazikubaliki katika maadili ya Kitanzania.

CCM na CUF wanapata wakati mgumu katika kampeni zinazofikia ukingoni kwa zomea kila kona mfano wa kiumbe cha ajabu kikipita!!! Pamoja na ccm kutumia makada wenye majina makubwa wanaichi wa Arusha wamekuwa wakiwapuuza na kujaza nyomi yenye Herufi kubwa kuwasikiliza Makamanda wapambanaji kikosi maalum kanda ya kaskazini kwa kuvutiwa na hotuba zenye kusisimua na sera za uhakika zinazogusa maisha yao ya kila siku. Kampeni za Arusha zimekuwa zikiongozwa na G Lema Kamada Mpambanaji akishirikiana na timu ya makamada vijana chini ya usimamizi wa makamanda wazee wenye hekima kama vile Mzee Mpinga na wengine!!!

Kinacho onekana katika uwanja wa mapambano ni kwamba CCM na CUF wamezidiwa nguvu kwani vijana wadogo makamanda wa Chadema wamekuwa wakikubarika sana na wapiga kura kwa sera nzito wanazomwaga kufafanuwa umuhimu wa kuwapeleka madiwani wengi wa Chadema manispaa.

Nilipo wahoji wanainchi kwanini wanawazomea CCM walinijibu kwamba taabu za maisha yao zimesababishwa na CCM na hivyo kukifananisha na kiumbe cha ajabu…….

Mungu ibariki Chadema Mungu ibariki Tanzania

Earthmover kamanda kikosi cha ushindi...uwanja wa mapambano Arusha
 
Toka lini zomeazomea ikawa ni HOJA. Kama walizomea, so WHAT?

Wazomeaji (kama wapo) na pia wale wanaofurahia mtu akizomea (kama wapo) wote wanafanya hivyo kwa sababu hawana hoja mbadala ya kujibu hoja zinazoibuliwa na upande wa pili wanaouzomea na wale wanaofurahia kuzomea.

Hizi ni siasa zilizopitwa na wakati huwezi kusikia mwanasiasa na mwanachi makini akifurahia kitendo kama hiki.
 
Yaani nashangaa sana timu nzima ya SSM inahamia Arusha kwa ajili ya udiwani tu. Tena huku mkijua kuwa hakuna ushindi. Perdiem zinawasumbua ninyi!!! Msichezee kodi za wananchi. Kama kweli mngekuwa mnatekeleza sera kwa manufaa ya wananchi wote kungekuwa na sababu ya kuhamia Arusha kwa kampeni ndogo kama hizi? Aibu kubwa sana. Acha wazomewe hadi kule kunako...
 
toka lini zomeazomea ikawa ni hoja. Kama walizomea, so what?

Wazomeaji (kama wapo) na pia wale wanaofurahia mtu akizomea (kama wapo) wote wanafanya hivyo kwa sababu hawana hoja mbadala ya kujibu hoja zinazoibuliwa na upande wa pili wanaouzomea na wale wanaofurahia kuzomea.

Hizi ni siasa zilizopitwa na wakati huwezi kusikia mwanasiasa na mwanachi makini akifurahia kitendo kama hiki.

...arusha...chadema yatosha....
 
Toka lini zomeazomea ikawa ni HOJA. Kama walizomea, so WHAT?

Wazomeaji (kama wapo) na pia wale wanaofurahia mtu akizomea (kama wapo) wote wanafanya hivyo kwa sababu hawana hoja mbadala ya kujibu hoja zinazoibuliwa na upande wa pili wanaouzomea na wale wanaofurahia kuzomea.

Hizi ni siasa zilizopitwa na wakati huwezi kusikia mwanasiasa na mwanachi makini akifurahia kitendo kama hiki.
Hivi ndugu katika political sphere unapoona watu wankuzomea unajisikia kuwa wewe unakubalika na kundi hilo? wakati mwingine hata ushabiki muwe mnaangalia siyo kuja na hoja zisizo na mashiko
 
Makamanda Habari za jioni…

Leo katika kata ya Erelai kulikuwa na mikutano miwili moja wa ccm na mwingine wa Chadema ambao ulikuwa na nyomi ya kutosha na ule wa ccm kama kawa kikundi cha watu wachache.

Wakati mkutano wa Chadema ukiendelea katika shule ya msingi ya Azimio ghafla msafara wa Nape ulipita.Kabla ya kupita takribani kama mita 300 kutoka eneo la mkutano msafara huo ulisita kupita mfano wa mtu kukutana na simba. Jamaa kuogopa aibu ya kugeuza msafara wao ilibidi wapite kwa aibu.Walipokuwa wakipita zomea zomea huwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii na vilio vingine vililipuka kutoka eneo la mkutano mfano wa kiumbe cha ajabu kikipita!!! Zomea zomea hiyo iliwachukiza jamaa hao wa ccm na kuanza kuonyesha ishara ambazo hazikubaliki katika maadili ya Kitanzania.

CCM na CUF wanapata wakati mgumu katika kampeni zinazofikia ukingoni kwa zomea kila kona mfano wa kiumbe cha ajabu kikipita!!! Pamoja na ccm kutumia makada wenye majina makubwa wanaichi wa Arusha wamekuwa wakiwapuuza na kujaza nyomi yenye Herufi kubwa kuwasikiliza Makamanda wapambanaji kikosi maalum kanda ya kaskazini kwa kuvutiwa na hotuba zenye kusisimua na sera za uhakika zinazogusa maisha yao ya kila siku. Kampeni za Arusha zimekuwa zikiongozwa na G Lema Kamada Mpambanaji akishirikiana na timu ya makamada vijana chini ya usimamizi wa makamanda wazee wenye hekima kama vile Mzee Mpinga na wengine!!!

Kinacho onekana katika uwanja wa mapambano ni kwamba CCM na CUF wamezidiwa nguvu kwani vijana wadogo makamanda wa Chadema wamekuwa wakikubarika sana na wapiga kura kwa sera nzito wanazomwaga kufafanuwa umuhimu wa kuwapeleka madiwani wengi wa Chadema manispaa.

Nilipo wahoji wanainchi kwanini wanawazomea CCM walinijibu kwamba taabu za maisha yao zimesababishwa na CCM na hivyo kukifananisha na kiumbe cha ajabu…….

Mungu ibariki Chadema Mungu ibariki Tanzania

Earthmover kamanda kikosi cha ushindi...uwanja wa mapambano Arusha

jana ccm walikuwa kaloleni hali yao ni mbaya.mwanri na medeye walikuwa walikuwa wanatoa macho uwanja ukiwa mtupu.jana usiku nape,mwigulu na mwanri walikuwa natroni hotel wakikuna vichwa poleni
 
Toka lini zomeazomea ikawa ni HOJA. Kama walizomea, so WHAT?

Wazomeaji (kama wapo) na pia wale wanaofurahia mtu akizomea (kama wapo) wote wanafanya hivyo kwa sababu hawana hoja mbadala ya kujibu hoja zinazoibuliwa na upande wa pili wanaouzomea na wale wanaofurahia kuzomea.

Hizi ni siasa zilizopitwa na wakati huwezi kusikia mwanasiasa na mwanachi makini akifurahia kitendo kama hiki.

Kaka zomezomea inafanyika kwa sababu CCM hawataki kukaa katika mdahalo mmoja na CCM ili kuuza sera na kwa sababu hiyo njia mbadala ni kuzomea zomea
 
Hivi ndugu katika political sphere unapoona watu wankuzomea unajisikia kuwa wewe unakubalika na kundi hilo? wakati mwingine hata ushabiki muwe mnaangalia siyo kuja na hoja zisizo na mashiko
Wewe vipi?. Utaiona vipi hoja yangu ina mashiko wakati unachokifikiria hakina mashiko katika ulimwengu wa hoja mbadala.

Toka lini zomea ikawa ni kipimo mbadala cha kisiasa kama unakubalika au hukubaliki zaidi dalili ya kukosa hoja.

Demokrasia kisiasa inajengwa kwa hoja na hoja mbadala zinapatikana palipo na political tolerance. Kinyume cha hivyo ni uhuni na vulugu.
 
Mleta mada Unafurahi Taifa letu liwe Taifa lenye Demokrasia ya Kuzomeana??? Mungu tunusuru na janga hili la kugeuka taifa la mazezeta(wazomeaji)
 
Back
Top Bottom