Nape aongea na vyombo vya habari, alalamikia masuala kadhaa!

Status
Not open for further replies.
Baada ya kukutana na kuzungumza, kila chama kitaamuwa kinavyoona sawa au pia kuna uwezekano mkubwa vyama vitapokutana vikakubalina kuwa na msimamo mmoja kuhusu suala/masuala yanayolihusu Taifa.
 
CCM wakutane na kufanya maamuzi yao na CUF ambao mpaka hivi sasa ndio walioamua KUUNGANA NA NGURUWE PORI kula mabua kwa pamoja. Hakuna malipo ya kitapeli kwa CCM Dowans kwa ajili ya kuja kununulia kura 2015.

Baada ya kukutana na kuzungumza, kila chama kitaamuwa kinavyoona sawa au pia kuna uwezekano mkubwa vyama vitapokutana vikakubalina kuwa na msimamo mmoja kuhusu suala/masuala yanayolihusu Taifa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame


na Mwandishi wetu


MPASUKO mkubwa umezidi kukikumba Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kuibuka makundi mawili makubwa na yenye nguvu kutuhumiana kwa uasi na usaliti dhidi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete.


Jana Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, aliwashushia tuhuma nzito baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho na kuwaita waasi na wasaliti dhidi ya uongozi wa mwenyekiti wao.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, Nnauye alisema kuna kundi lenye uwezo wa kifedha linaloendesha uasi kwa nia ya kutaka Kikwete ang'olewe uenyekiti wa chama na kubaki na nafasi ya urais tu.


Alisema kundi hilo la viongozi linalowatumia baadhi ya viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) limejificha, ingawa wao kama chama wanamjua kila mshiriki wa njama hizo.


"Kama nia ni njema kwa nini wasijitokeze hadharani badala ya kuwatumia watu na kama hii hoja ya kutenganisha kofia ina masilahi kwa chama na si kikundi kidogo cha watu kwa nini wanatumia nguvu ya pesa kutaka kuwashawishi wajumbe badala ya kuleta kikaoni?" alihoji Nape.


Alizidi kulishambulia kundi hilo akidai kuwa lilishiriki kukihujumu chama hicho katika uchaguzi wa Igunga, wakitumia kauli mbiu ya ‘Tushindwe ili tuheshimiane."


"Kundi hilo la waasi lilitaka chama hicho kishindwe ili kuweza kuhalalisha hoja ya kutenganisha madaraka na mamlaka ya rais na uenyekiti wa chama. Juhudi hizi zilifanyika bila kificho, tunajua hazikuwa na nia njema kwa chama chetu na zilisukumwa na uroho na ubinafsi zikiwa na ujasiri mkubwa wa kifisadi, bila kujali masilahi mapana ya chama kama taasisi na nchi yetu kwa ujumla," alisema.


Alisema kutokana na harakati hizo amewataka wanachama wa chama hicho watulie na wasibweteke, ila kundi hilo ni lazima lifahamu CCM inajua kila hujuma wanazozifanya.


"Nawataka hawa waasi niwakumbushe, CCM tuliamua, tuliahidi na tutatekeleza maamuzi yote ya kujivua gamba bila woga. Hakuna kinachobadilika kwa sarakasi za barabarani na wajue wanapoteza muda.


"Sasa pengine tujiulize, wana CCM na Watanzania wanaodai tunapotosha maamuzi ya NEC ni kina nani na kwa masilahi ya nani," alisema Nape.


Kauli ya katibu huyo imekuja siku mbili tu baada ya Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa, kuwashambulia baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho kwa kupotosha maamuzi ya kujivua gamba, maneno yanayoonekana kumlenga zaidi Nape Nnauye.


Kaulimbiu ya kujivua gamba ndani ya chama hicho imeleta msigano mkubwa ndani ya CCM, kiasi cha kuzuka kwa makundi yanayopingana waziwazi.


Mara tu baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kilichoketi miezi michache iliyopita, na kuilazimisha sekretarieti iliyokuwa ikiongozwa na Katibu Mkuu Yusufu Makamba kujiuzulu, chama hicho kilikuja na kauli hiyo iliyowalenga zaidi viongozi watatu waliotuhumiwa kukichafua mbele ya jamii. Hao walikuwa ni Rostam Aziz, Andrew Chenge na Edward Lowassa.


Hata hivyo, Nape ambaye amekuwa akishikilia msimamo huo amekumbana na mashambulizi makali kutoka kwa baadhi ya viongozi na wanachama wa chama hicho, akidaiwa kupotosha zana nzima ya kujivua magamba.


Hali yazidi kuwa mbaya CCM Tabora

Huko Tabora mgawanyiko mkubwa umezuka baina ya viongozi wa chama hicho ngazi ya mkoa.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho zimeonesha kuwa baadhi ya viongozi wa CCM na Umoja wa Vijana (UVCCM), wameunga mkono kauli ya Benno Malisa, kupinga upotoshaji na maana halisi ya kujivua gamba.


Mmoja wa viongozi waandamizi wa UVCCM mkoani Tabora (jina linahifadhiwa) alisema CCM inakosa mvuto kwa wananchi na hata ushindi wake wa ubunge Jimbo la Igunga umepatikana kwa nguvu za ziada.


Kiongozi huyo alisema Watanzania wamekichoka chama hicho kutokana na viongozi wengi kuacha kuzungumzia masuala mengi ya msingi na hotuba hizo hazina tofauti na nyimbo za taarabu.

Alisema badala ya hotuba za viongozi wa ngazi ya juu kukazania mambo ya msingi ya kitaifa, yakiwemo namna ya kutatua kero za watu, zimejaa vijembe, mipasho na maneno ya ajabu tu.

"Ninatoa onyo iwapo viongozi wataendelea kutoa hotuba za aina hii majukwaani na kuacha kutoa hotuba za msingi, wanachama wengi zaidi watahama," alisema kiongozi huyo.


Kutokana na chama hicho kwenda mrama, wanakubaliana na kauli ya Malisa ya kuwataka vijana kote nchini kuchukua jukumu na wajibu wa kushika nafasi za juu za uongozi nchini.

Wakati hayo yakijiri, habari za kuaminika zimebainisha kuwa zaidi ya wanachama wakiwamo viongozi wa ngazi za mashina 800, wanadaiwa kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Taarifa zinasema wanachama hao wa CCM wengi wao wakitoka vijiji vya kata za Ufuluma, Ibiri na Usagali, wameamua kujiunga na CHADEMA kwa madai ya kukatishwa tamaa ya maisha.


Taarifa hizo zinadai kuwa wanachama hao wamechukua hatua hiyo ya baada ya kucheleweshewa malipo yao ya tumbaku kwa miezi mitano sasa, huku wengine wakisema wamechoka kufanywa brudoza na viongozi wao wakati wa kampeni na kuwaacha wakiishi maisha ya shida.


Hivi karibuni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora, Hassan Wakasuvi, aliwashambulia hadharani kwa vijembe na mafumbo wanachama wenzake wanaosadikiwa kutoka kundi la aliyekuwa mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.


Katika hotuba yake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya sanamu ya Mwalimu Nyerere, mjini Tabora, Wakasuvi alikaririwa akisema: "Najua mpo mliotaka CCM ishindwe Igunga, nyie nawapa pole.


"Lakini natambua wapo waliopenda CCM ishinde Igunga, nyie nawapongeza na endeleeni kujipongeza, maana tumeshinda shangilieni," alisema Wakasuvi.

 
ccm wamemaliza uchaguzi igunga kwa ushindi, laikini wanaonekana hawana furaha kabisa........... sijui nini kimewakumba
 
oh yeah naona wameona kuwa Igunga ya 2010 na Igunga ya 2011 gharama kwa CCM imekufuru mara 7 na umashuhuri wa CCM Umeshuka sana na pia sio chama kinachopendwa - lazima waogope

Wanajuma Walifanya mabaya mengi ili kushinda na kama ni hivyo kwa Majimbo yote 2015 then CCM chini
 
Baada ya kukutana na kuzungumza, kila chama kitaamuwa kinavyoona sawa au pia kuna uwezekano mkubwa vyama vitapokutana vikakubalina kuwa na msimamo mmoja kuhusu suala/masuala yanayolihusu Taifa.
Msimamo wa cdm juu ya dowans unajulikana, mpaka wanaitisha maandamano ujue wanapinga hivyo ccm iungane nao kupinga malipo ikimaanisha kujipinga yenyewe au ccm iendelee kuunga mkono malipo ili kutimiza lengo lao kuu, ambao ni msimamo wa ccm(kulipa). Wanata wakae na cdm kubagain nini? Mimi nilitarajia ccm ikutane dowans ambaye walisha kana kumfaham(jk) na c chadema. Sitarajii cdm kukubali jambo hilo
 
Nape kama kweli unajiamini jiuzulu uokoe heshima kidogo uliyobakiza unazidi kudidimia ndugu yangu
 
Baada ya kukutana na kuzungumza, kila chama kitaamuwa kinavyoona sawa au pia kuna uwezekano mkubwa vyama vitapokutana vikakubalina kuwa na msimamo mmoja kuhusu suala/masuala yanayolihusu Taifa.

sera za vyama hivi zinatofautiana pia chama chetu ndio kimesababisha deni ili kuwa kubwa kwani wamechelewa kulipa
sidhani kama chadema watakuba labda katibu mwenezi na mwenyekiti akubali kujiuzulu nafasi yake kwani wameshindwa kuiokoa serikali na chama pia
 
NAPE KAMA KUNA KUNDI LINATAKA KUMPUNGUZIA RAIS KIKWETE MZIGO WA KOFIA NZITO 'UENYEKITI WA CCM' TAFADHALI KAWAPE ZAWADI HAO KWANI NI MARAFIKI WAKUBWA WA USTAWI WA TAIFA LETU!!!

Nape, kutenganisha kofia ya urais kuwa tofauti na kofia ya Uwenyekiti wa Chama cha siasa vyote kwa pamoja wala si kitu cha kusema ni njama bali hivyo ndivyo misingi ya Utawala Bora unavyotuelekeza.

Kwa kuku kumbusha tu kidogo, tangu muibe kura zetu mwaka jana - miongoni mwa mambo yaliopendekezwa na waangalizi wa uchaguzi wa Jumuia ya nchi za Ulaya kwenye ripoti yao, ambayo bila shaka wataifuatilia kwa karibu sana,
ni pamoja na KUTENGANISHA NYADHIFA ZA KICHAMA NA SHUGHULI ZA KICHAMA ili mipaka ya kiserikali ionekane wazi na ile ya kichama ikajitenge pembeni kabisa.

Kuna miaka fulani ijayo ambapo hata kazi za ukuu wa kata, wilaya na mkoa pamoja na ukurugenzi wa miji na halmashauri zitapata kuwa ni za ki-weledi zaidi, kuvaa sare nzuri, kusimama kwenye kofia ya kiserikali tu wakati wote na kurahishisha utendaji mathalan kunapotokea mvutano tuseme kati ya CCM na CHADEMA juu ya jambo.

Lakini kwa leo hii watu huwa tunajua hata aina ya majibu tutakayopewa pindi kunapotokea mazingira kama hayo hapo juu. Nasema kazi zote hizi zenye kugharamiwa na kodi za umma huko mbele ya safari zitakuwa ni kazi za kuheshimika sana za kutumiwa maombi na watu kupigwa usaili na taasisi huru na wala
hazitoendelea tena kuwa VICHAKA VYA KUWAHIFADHI AKINA MWANANZILA WALA NAPE baada ya kukataliwa na wananchi kwenye kura majimboni wala kujulikana kuwa ni nafasi za WATEULE WA CCM tu miaka nenda miaka rudi.

Kwa kweli ni huo muunganiko wa nyadhifa na shughuli za kichama katika mambo ya kiserikali ambayo imekua ikisababisha muingiliano mkubwa mno ki-utendaji na kusababisha mgongano wa kimaslahi kwa faida ya mshindani mmoja na kumpunja mwingine hasa pale uchaguzi unapoitishwa. Mfano hai ni kama vile Bi Fatuma Joseph Kimaro - mtu mmoja aliyeelezewa kuwa ni MKUU WA WILAYA YA IGUNGA anapoonekana kukipigia debe chama akipendacho moja kwa moja na kutekeleza mikakati yake kuorodhesha shahada za wapiga kura wa eneo husika huku kazi za kiserikali zikilala na vyama vya ushindani visivyopendelewa na huyo mama wao kujikuta hawana chao.

Isitoshe, huu mkanganyiko wa kuonekana ni busara rais asiunganishe pia uwenyekiti wa chama na shughuli za kiserikali zilijidhihirisha pale ambapo Rais Kikwete alipoonekana kutuacha hoi kwa kwa kutoa maelezo tata yanayokinzana kila anapobadilisha kofia zake zenye mamlaka za aina mbali mbali katika jamii yetu.

Mfano hai ni kufuatia kauli tata juu ya bei ya mafuta ya taa nchini. Akiwa kama kiongozi mkuu wa serikali Kikwete alitueleza kwenye bajeti kupitia kwa waziri wake wa fedha kwamba bei ya nishati hiyo ipande zaidi. Siku alipokua akiongoza kikao cha chama chake, Kikwete alisikika akipaza sauti kwamba wao kam chama wanakiagiza serikali ipunguze bei ya mafuta ya taa mara moja.

Lakini yeye kama mwanahisa mkuu na mmiliki wa kampuni ya kibiashara ya Lake Oils, tunashawishiwa kuamini kwamba bei kubwa wanazoendelea kutoza kwenye nishati hiyo nchini huenda ndio kielelezo cha maazimio ya kikao chao binafsi cha bodi ili kujitengenezea faida zaidi.

Nape hadi hapo, kama kweli ulihitimu na kisomo cha digri kama ulivyowahi kusema kwamba ndio urithi pekee ulioachiwa na Mzee Moses Nnauye (lakini vyanzo vyetu vinaelezea kuwa mlipa ada ilikua ni CCM kule UDSM) basi ungepashwa ukajiunge haraka na hao watu wanaotaka kumpunguzia Kikwete majukumu ya kichama ili angalau akaoneshe ufanisi zaidi kwenye zile kofia za kuiongoza serikali na vile vile kule katika kuongoza fikra za uendeshaji wa biashara ya familia ambapo nako Sheria za Miiko ya Uongozi katika ofisi za Umma huenda ukatuelekeza vingine na wao wanaharakati wakaona sababu za kumpunguzia nako kofia hilo lingine nalo.

Kwa kuhitimisha Nape, napenda nikujulishe ya kwamba ni wewe na watu wa aina yako ndani ya chama chenu huko ambao ndio mmekua maadui wakubwa wa Rais Kikwete kwa kutomueleza ukweli juu ya swala zima la utawala bora kwa ngazi yake yeye mwenyewe na kwamba wale mnaowaona kama wafanya hujuma vile ndio hasaaa wanaomtakia mema rais.

Tafakari na ukashauri moyo wako vizuri zaidi huku ukikumbuka ukweli kwamba CCM, CHADEMA, TLP, Rais Kikwete, Nape, Uwezo Tunao, FaizaFox ... wooote ni wa kupita tu ila Tanzania itaendelea kwepo hivyo ushauri wko siku zote uweke mbeeeeeele kama tai maslahi ya Tanzania kwa ujumla wake na wala si kwa kuzingatia maslahi binafsi ya mtu anayeitw Rais Kikwete wala chama cha siasa kuonekana kuwa ndio ya maana zaidi.

Nikipata nauli nitafika Lumumba na Magogoni kupokea marejesho baada ya wewe na huyo mwana-JF mwingine mashuhuri kumaliza kusoma taarifa hii hapa.
 
Sarakasi zinataka kuchezwa hapo!! Subirini kama hatujaishia kula mlo mmoja kwa siku ili deni lilipwe.
 
Una ushahidi gani?
Kwanza ushahidi wa kimazingira mara ya mwisho alionekana akiingizwa kwenye gari la CCM, pili matamshi ya kiongozi wenu Nape kuwa yatakayotokea tusiwalaumu, tatu si mara ya kwanza kuteka Igunga na Arusha, ukiongeza na sababu za kitaalamu moja kwa moja nyie ni prime suspect kwa hili hamtatoka kamwe.
 
Hayo ndiyo matokeo ya kukiendesha chama kisanii. Usilalame kuhusu mpasuko wa sisiem, mtoto umleavyo.... Jipangeni vizuri, la sivyo, sisiem yaweza kuwa chama cha upinzani in future. Si umeona Northern Rhodesia (aka Zambia), Kenya na Nyasaland (aka Malawi).
 
hapa nashindwa kuelewa yafuatayo;
  1. anayewalipa DOWANSI ni nani ?
  2. mlipaji akiamua kulipa hata mkiandamana mtafanyaje ?
  3. nini impact ya maandamano katika nchi hii ?
tafadhari naomba kujua hayo tu , nitarudi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom